Kyela: Mgomo wa maduka ni balaa, Wananchi waiomba serikali iongee na Wafanyabiashara wayamalize

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,745
239,396
20240627_172430-1.jpg


Mgomo unaofanywa na Wafanyabiashara kwenye Mji wa Kyela unaochukua siku ya 3 sasa umeanza kuumiza wananchi

Inawezekana mgomo wa eneo hili ukawa ndio mgomo kabambe kuliko yote nchini Tanzania, ni vigumu kyela kupata hata kiberiti au mafuta ya kula, karibu kila mwenye duka amefunga duka, duka pekee lililowazi ni la SAULI PATAYA ambaye aliwahi kuwa mbunge wa ccm huko Rungwe (Haijulikani kwanini yeye hajagoma), hata hivyo yeye anauza vifaa vya umeme na Ujenzi ambavyo si mahitaji ya lazima kwa wananchi.

Lakini maduka karibu yote yamefungwa na kusababisha uhaba mkubwa wa bidhaa jambo lililosababisha Wananchi kuiomba serikali imalize utata huo.

Haifahamiki itakuwaje ikiwa mgomo huo utamaliza wiki .

Hakika hali ni ngumu mno!
 
Back
Top Bottom