Kwenye sakata la mchanga wa dhahabu, nafahamu ukweli wa ndani

Ikena

JF-Expert Member
Oct 24, 2007
553
397
Naomba ni declare interest kuwa, mimi ni mmoja wa wataalam wanaouhusika na ishu iyo ya mchanga.

Kifupi naomba nieleze kile ambacho kipo kwenye makontena. Kilichopo kwenye makontena kwa asilimia kubwa ni copper(Cu) , ifufuatiwa na silver (Ag) na dhahabu (Au) haizidi asilimia 0.05.

Yule Afisa wa Bandari aliyesema kuwa zaidi ya asilimia 90 ni dhahabu ni muongo na anapaswa kuiomba radhi ACACIA na watanzania kwa ujumla na atumbuliwe kwenye nafasi yake.

Kiwango kilichopo kwenye yale makontena zaidi ya 256 ni kati ya sililimia 0.012 -0.02, g/t

Mh spika alidhani kiwango cha asilimia 0.02 kuwa ni kidogo na hauwezi kupata faida iwapo utalisafirisha kontena kutoka mgodini mpaka China, Japan au Ujerumani.
Naomba nimuulize, anajua gharama ya kusafirisha hilo kontena? Kifupi haizidi milioni 8.

Nikija kwenye mchanganua wa hiyo asilimia 0.02 kwa contena, naomba nimfafanulie mh spika kama ifuatavyo:-

(1) 0.02% hii ni gram kwa tani, kwa maana hiyo hii ukiizidisha kwa tannage zilizopo (eg 20.5tn), utapata 0.41%.
(2) Hii 0.41 ili upate ppm, unatakiwa uizidishwa kwa 10000, utapata 4100ppm au g/t.
kwa maana nyingine, yule mtaalam wa TMAA aliwaambia kwenye kila container kuna takriban kilo 4.1. sasa hii ni ndogo?
(3) Kwa sasa kilo ya dhahabu ni takribani mil 90. 90x4=360m.
sasa iwapo utasafirsha container moja kwa 10m, huoni kuna faida?

Pia Kamati ya Bunge kupitia Spika alidai kwa mwaka ACACIA, Buzwagi na Bulyanhulu huzalisha takribani idadi ya makontena elfu 50, na kwa maana hiyo contena milioni moja yameisha safirishwa. HUU SIO UKWELI.

Ukweli ni kwamba hizo ni tani za mchanga wa dhahabu na sio idadi ya kontena.

Mpaka sasa, migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi wameisha safirisha makontena yasiozidi elfu 50.

Mpaka sasa Bulyanhulu peke yake wamesafirisha contena sizizozidi elfu 42. Sasa hizo contena 1m, zimetoka wapi?

Mh. rais kuna wanakupotosha, na hili utalithibitisha kupitia sample zilizochukuliwa na Mh Waziri Mkuu jana katika mgodi wa Buzwagi, kwani kati ya makontena aliyochukua sample, moja wapo ni kontena ambalo lililkua na seal na document zote za serikali na lilikua tayari kusafirishwa kwenda Ujerumani. Baada ya tamko la rais kontena hilo lilirudishwa mgodini pamoja na makontena mengine 3, yakiwa tayari yamefika Isaka.

My take:-

Kwenye hili sakata la mchanga, mihemuko isitumike. Wawekezaji wa ACACIA hawamuibii mtu kwani hata kama kungekua na 90% ya dhahabu, TMAA huchukua sample pia, kiasi kwamba wangeweza kuiambia serikali kuwa ACACIA wanawaibia kwa kutoa takwimu za uongo.

Iwapo mikataba haiwafaidishi watanzania, ifanyiwe review kwani ACACIA hutumia mikataba hiyo hiyo kufanya calculation zao.

Iwapo itathibitika kuwa ACACIA pia hawawaibii watanzania kwa kuficha dhahabu kwenye mchanga, basi pia Katibu Mkuu aombwe radhi.
 
Mkuu upo sahihi, ila napenda nikueleze kuwa mkuu sio kwamba anadhani tunaibiwa ila nilivyomuelewa anamaanisha yale madini mengine ambayo hayachukuliwi mrabaha tunarekebisha vipi.Kumbuka kwenye makinikia tunalipwa gold, silver na copper tu, je vipi kuhusu chuma, sulfur, na madini mengine. Nafikiri hicho ndicho mkuu anataka kujua.Nipo tayari kusahihishwa
 
Umeongea kisomi kabisa na ukweli mtupu mkuu nendeni mahakamani kukomesha huu ubabaishaji na kuharibu majina ya wawekezaji sio kila jambo lazima lifanywe kisiasa.wanakurupuka kwa mambo ya kitaalamu
Mkuu pia kwenye ishu hii kuna watu wanadai Tanzania haiwezi kuweka kiwanda kwani wanaumeme mdogo.
Hiyo sio kweli, umeme uliopo unatosha iwapo kiwanda kitakuwepo.
Umeme sio hoja hoja ni je kiwanda kikiwekwa, kitaleta faida?

kwenye teknolojia ya uyeyushaji, kitaalamu kuna material ambayo yanatumika kushusha boiling point
Mkuu upo sahihi, ila napenda nikueleze kuwa mkuu sio kwamba anadhani tunaibiwa ila nilivyomuelewa anamaanisha yale madini mengine ambayo hayachukuliwi mrabaha tunarekebisha vipi.Kumbuka kwenye makinikia tunalipwa gold, silver na copper tu, je vipi kuhusu chuma, sulfur, na madini mengine. Nafikiri hicho ndicho mkuu anataka kujua.Nipo tayari kusahihishwa
Hayo yapo kwa kiwango kidogo sana ukiyacheki kupitia ICP au XRF kiongozi.Ni takribani 0.0017 na kuendelea.
 
Ebu ngoja ni subscribe huu uzi, ili niwe na akiba ya maneno. Pili naomba nikukosoe kwenye idadi ya makontena.

Muheshimiwa spika alisema, makontena 50 elfu husafirishwa kwa mwaka. Hii ni Sawa na makontena takriban 1 molion tangu migodi hii ilipo funguliwa.

Pia tutajuaje kama watumishi wasio waaminifu wa TMAA walilikua wakichukua mlungula ili wakae kimya...?
 
Kwanza hizo kontena zingekuwa na hata asilimia 50 ya dhahabu, zisingesafirishwa kwa njia ya barabara.

Miaka ya 2005-2008, contena zaidi ya 72 za mgodi wa bulyanhulu zikiwa na hizo asilimia 0.03 zilitolewa mchanga zikiwa njiani kuelekea bandarini maeneo ya tabora, na kesi bado ipo mahakamani, sasa sembuse 90%.
 
Mkuu upo sahihi, ila napenda nikueleze kuwa mkuu sio kwamba anadhani tunaibiwa ila nilivyomuelewa anamaanisha yale madini mengine ambayo hayachukuliwi mrabaha tunarekebisha vipi.Kumbuka kwenye makinikia tunalipwa gold, silver na copper tu, je vipi kuhusu chuma, sulfur, na madini mengine. Nafikiri hicho ndicho mkuu anataka kujua.Nipo tayari kusahihishwa[/QUOTE
Alisema tunaibiwa ndio maana akasema kama watanzania wangejua kilichomo mle ndani wangelia... Read btn the lines
Alisema tunaibiwa bhana ndio maana akaongea kwamba kama watanzania wangejua kilichomo mle wangelia... Read btn the lines joh
 
Ebu ngoja ni subscribe huu uzi, ili niwe na akiba ya maneno.
Pili naomba nikukosoe kwenye idadi ya makontena.....
Muheshimiwa spika alisema, makontena 50 elfu husafirishwa kwa mwaka. Hii ni Sawa na makontena takriban 1 molion tangu migodi hii ilipo funguliwa.
Pia tutajuaje kama watumishi wasio waaminifu wa TMAA walilikua wakichukua mlungula ili wakae kimya...?
Mkuu naomba nikuambie mpaka leo Bulyanhulu peke yake hawajafikisha makontena elfu 50. Naomba uniamini tu mkuu kwani mimi sifaidiki kwa chochote kuwatete Acacia.

Hizo ni tonne kwa mwaka na sio idadi ya kontena tena kwa migodi yote miwili.
 
Hizo ni tonne kwa mwaka na sio idadi ya kontena tena kwa migodi yote miwili.[/QUOTE]
Kwa hili upo sahihi. Ila viwango vya madini mengine, bado siwezi kuamini
 
Back
Top Bottom