Kwenye biblia uafrika umetajwa mara nyingi 56 kwenye agano la kale ila mzungu ndo anapewa hatimiliki ya biblia na ukristo

Mpigania uhuru wa pili

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
2,811
5,327
Katika jamii ambayo watu ni rahis kuwa brainwash basi ni waafrika

Mfano:- neno kush likimaanisha mwafrika limetajwa mara nyingi sana mke wa musa alikua ni mwafrika, sefania alikua ni mwafrika na malkia wa sheba alikua ni mwafrika
Ila ni kawaida sana kukuta mwafrika anawapa umiliki wa ukristo wazungu

Baada ya Yesu kupaa kuna yule mtu aliyetoka ethiopia ni watu wa kwanza kabisa kubatizwa na filipo kabla hata paulo hajapata wito kumbuka kipindi hiki alikua mwasi Matendo Ya Mitume 8:26-40 ni ajabu sana mtu anakuambia waafrika wameletewa ukristo

Huku mwafrika tokea zama za Musa tayari ametajwa kwenye biblia yaani biblia iko afrika miaka mingi sana kabla hata yesu hajazaliwa ila anaibuka mtu anakuambia biblia imeletwa na wazungu ni ajabu sana

Kama nilivyosema kuna character nyingi sana za waafrika kwenye biblia kuliko wazungu mfano;- mke wa musa, yethro, sefania hizi ni baadhi ila yote haya mwafrika hayaoni anaishia kusema biblia ni ya wazungu ila cha ajabu hakuna character ya mzungu kwenye agano la kale lote

Mzungu ni bingwa wa kuiba historia yaani yale mazuri yote amejimilikisha na yale mabaya amewapa watu kama waafrika

Katika hii dunia ni rahis sana kumdanganya mwafrika kuliko mtu yeyote yule labda kwa sababu uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo
 
Kush ni ufalme wa kale maeneo ya Sudan Kaskazini.Ufalme huu ulipakana na ufalme wa Khemet(misri) na chini ya mfalme Kikianus Uarabuni yalikuwa makoloni yake.Pitia Yoshua 10:13 katika biblia kisha ukitafute kitabu cha Yashari.Nyakati hizo mzungu alikuwa bado giza na hivyo habari zake hazikutambulika.Miaka hiyo ya 1700-1300KK watu weupe wanaotajwa ni 'hyksos' ambao waisraeli waliwahi pindua utawala wa Khemet ambapo jenerali Ahmose naye akawapindua tena.Hii biblia iliyokusanya hekaya yatosha kuwa wongozo wa maisha yako ndugu?
 
Back
Top Bottom