Kwenye biashara wahalifu hawapo mbali, uliwahi kupigwa tukio gani hutasahau?

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
564
1,719
Unaweza kujichukulia poa una biashara yako inakuingizia visenti kadhaa lakini jua kwamba wahalifu wapo bize kujaribu kubuni mbinu za kukupiga wapate chao bila kuvuja jasho.

Nakumbuka kuna kipindi kulijengwa frem mpya mahala, nikaona ile sehemu kwa jinsi ilivyochanganya nichukue frem, niliweka duka kama min market, kalikuwa kaduka kanavutia, binti wa kazi nae alikuwa anajituma.

Siku ya siku natumiwa picha whatsapp na kijana wa binti wa dukani kuna tundu kubwa sana limetobolewa ukutani pamoja na majirani wawili, duka limesafishwa lote wameacha viti.
 
Niliwahi pigwa vocha za m3! Kidogo nizimie na haikuwa biashara yangu nilikuwa nasimamia tu mshahara waenyewe laki Kwa mwezi aseee yule boss mbingu ataiona hakunitoza hata hata sent wala kunifukuza kazi ndo kwanza nilikuwa na wiki tu

Asubhi na mapema nafungua duka jamaa akaja akiwa na begi anahitaji vocha za Jumla yaani tigo za 875k
Voda na Airtel za pesa hiyo! (Sikumbuki vzr kama bei ilikuwa hiyo) Lkn Kwa thamani ya vocha zilikuwa za m3.

Baada ya kumpa maana zilikuwa zinakuja kwenye vibox fln za tigo kwenye karatasi zimewekwa kama wembe..

Halow sijui muda Gani alibadirisha na akapigiwa simu akiambiwa vocha usinunue tumepata huku muda huo anahesabu Hela anipe sikujua hata alibadirisha vipi akanipa vocha zilizo tumika! Cha ajabu ni kwamba zile vocha hazijakwqnguliwa kabisa Asee !!
 
Back
Top Bottom