Kwann vichaa hawadhuriki na magonjwa?

The redemeer

JF-Expert Member
Jan 28, 2025
2,389
4,360
Unaweza kumkuta mtu kichaa anaoga, anapiga mswaki, anakula majalalani, analala popote nje kwenye mazingira machafu, lakini yupo fresh tu na hapati magonjwa. Jibu ni kwamba hajui kama kuna magonjwa, hivyo hana hofu.

Kiroho, kichaa ni mtu ambaye nafsi yake imechukuliwa.

Nafsi ni mwili wa ndani wa mwanadamu, kama hewa – huwezi kuishika wala kuigusa. Nafsi ndiyo inayoota ndoto na kusafiri; ukiwa umelala Dar, inaweza kwenda Mbeya.

Baadhi ya vichaa ni misukule iliyokosa pa kwenda baada ya mmiliki wake kufa, ndiyo maana mara nyingi hatujui ndugu zao ni kina nani.

Kuna vichaa wengine wanaojitambua kiasi na kuomba pesa – hawa mara nyingi ni wachawi waliotunguliwa. Huwa wanahangaika kutafuta nauli ili warejee makwao, iwe mikoani au nje ya nchi. Hawa bado wana nafsi na kumbukumbu.

Wengine ni wachawi wanaolipa adhabu kwa kukiuka miiko ya kazi katika vyama vyao. Hawa hawana nafsi, ni miili mitupu kama makopo.

Pia, kuna waliopata changamoto za afya ya akili kwa sababu mbalimbali. Hali zao hubadilika mara kwa mara, kama nusu mwezi, kwani nafsi zao huondoka na kurudi.

Kwa hiyo, hofu ya magonjwa ndiyo ugonjwa wenyewe. Tunaumwa kwa sababu tunahofia magonjwa, kwa sababu tunajua ugonjwa upo.
 
Kuna jirani yetu alikua kichaa nilikuwa namuonaga anaumwa na ndugu zake wanampeleka hospital na alikuwa anatumia dozi Kama watu wengine. Ila kumuuguza Wana pata nae Tabu.
 
Back
Top Bottom