Kwann TBC haikulipa kipaumbele tukio la uvamizi Mkuranga

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Wana jamvi

Kituo cha Taifa cha televisheni yaani TBC haikuitendea haki taarifa yenye majonzi kwa uvamizi na kuuawa kwa askari wa jeshi la polisi Mkuranga, hili ni tukio lenye sura ya kitaifa kwa maana ya kupoteza askari wetu, lakini kituo cha tbc tunachokitegemea sana kutuhabarisha kimelipa kisogo tukio hilo lilnalopingwa na kulaaniwa na wadau wote wa amani nchini, TBC walichotakiwa kufanya ni kuwatafuta wasemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani na vyombo husika ili tujuzwe hali ilivyo, hii ni tofauti kwa vyombo vya habari vya nchi za Ulaya na Marekani vituo vyote vya ulaya na Marekani vinaweka vipaumbele vya matukio hatari kama hayo kwa kuandika "Breaking news" za mara kwa mara kuhusu matukio yenye sura za kivamizi na mauaji
 
"Kwani TBC ndo walileta"

majambazi TBC pigeni kazi in mkulu voice
 
Mkuu, TBC wanaamini kwamba wao pekee ndiyo wenye uwezo na nguvu ya kufika maeneo ya vijijini na hivyo kukaa kwao kimya katika matukio kama haya kunawafanya wananchi waliopo vijijini au pembezoni wasipate habari zenye kushitua kama hizi na kuwafanya wawe na maswali au mashaka na utendaji na umakini wa serikali yao. Rejea mkasa wa meli kule Nungwi TBC walikuwa wanapiga taarabu huku habari ikisambaa kama moto hadi vijijini. Binafsi tukio la kuuwawa kwa askari huko Mkuranga nimelisikia kwa mara ya kwanza kutoka kwa ndg yangu aliyeko Nanyumbu tena kijijini kabisa.
 
Mbona Sizonje tukio la njaa hakulipa kipaumbele huku akikanusha kabisa hakuna njaa mpaka Leo hii.Huwezi jua huenda ni maelekezo toka juu!
sasa we umeiona hiyo njaa uchwara ya tundu lissu.
au gharama chakula tu iko juu?
 
TBC ni kituo cha habari ambacho kinaonekana kipo lakini kama hakipo.
na kwa misingi hiyo inamaana TBC sio
kituo cha kutegemeeka kupata habari.
 
Jibu ni rahisi sana. Ni chombo cha habari cha kitaifa.
Habari kama hiyo haina tija kwa taifa bali huleta taharuki.
Ili kuepusha mengi ni heri kunyamaza. Kila nyumba ina SIRI zake za ndani
 
May be kuna mtu katumwa kwenda kumuuliza mkulu iwapo waitangaze hiyo habari au laa na huyo mtu Bado hajarejesha mrejesho
 
Walishapigwa chini na serikali kitambo tu ndio sababu..
 
hili tukio mamlaka husika zimekataa kulizungumzia ukiwa kama mwandishi mweledi huwezi kurusha taarifa ambazo mamlaka husika hazijazitolea ufafanuzi utakuwa unakiuka misingi ya uana habari.....ukisoma kwenye taarifa zinazosambaa utaona wameandika mkuu wa polisi hakupatikana kutoa ufafanuzi. Sasa we mwandishi ndio aende mochwari kuthibitisha kifo?
 
Dahh mmnamoyo.. kumbe bado mnaitazama hii channel inayotoa habari kimkakati!!?
 
When you try so hard to consile the truth in belief of protecting the goverment from "bad image" you might end up failing to report an important incident. That is what the TBC ya Ryoba has become...shame on him
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…