Kwanini watu walio kwenye ndoa wanahangaika na wasio na ndoa?

Sean Paul

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
1,311
3,239
Habari za asubuhi wana JF

Bila kupoteza muda, moja kwa moja kwenye mada. Hivi kwanini watu waliooa wanahangaika na watu wasiooa? Mwanaume asiyeowa anaonekana kuna jambo analiepuka bila sababu. Kwanza muelewe kila mtu ana sababu zake.

Maneno yamekuwa mengi kwamba wanakimbia majukumu, hawajakuwa bado kiakili mpaka watakapoowa, wana tabia za umalaya, hawajielewi, hawana hofu ya Mungu, ongezea na nyingine unayoijua wewe.

Tukianza kuchambua hoja moja baada ya nyingine unagundua hoja zote ni dhaifu. Kwa sababu kuna watu mashuhuri sana duniani waliishi na wengine bado wanaishi bila ndoa katika kila ya hoja hizo hapo juu. Ninaposema mashuhuri namaanisha ni icons za dunia na idols kwa watu wengi. Lakini pia kuna ndugu zenu wengi huko mnawajua wanaishi safi kabisa bila ndoa. Hivi kwani hakuoni pia ndoa imekuwa sababu za maanguko ya wanaume wengi sana kisaikolojia, kiafya, kiuchumi, kijamii kama vile mparaganyiko wa kifamilia au kutengwa/kuchukiwa na familia, kesi za mirathi n.k. Mifano ipo, na wenyewe mnaijua huko mnakoishi, angalau kuna watu wawili katika ukoo wenu hawaelewani kisa NDOA, yao wenyewe au inawahusu kwa namna fulani. Sasa shida zote za nini?

Katika dunia ya sasa, ndoa kwa mwanaume imebaki na sababu kuu mbili tu kama sio moja. Watu wanafata ndoa just to acquire social status-MARRIED, nothing else. Hao wanawake mnaotuhimiza tuwaoe wana mission zao zinazowafanya waingie kwenye ndoa.....once the mission is completed we mwanaume mwenzangu hauna maana yoyote kwake.

Sababu ya pili ambayo haina nguvu ni hitaji la kidini........kwamba dini zinahimiza kufunga ndoa. Lakini hoja hii ni dhaifu kwa sababu watu hawatekelezi mambo ya msingi ya dini ionekane hapa ndio wameamua kuabide with the law? Hell, no, kwa sababu mtu ameowa lakini bado mzinzi (michepuko) anakula rushwa, mwizi, mfiraji, anakula/anatoa riba (kwa waislam), mlevi n.k mnataka kuniambia huyu ameoa au kuolewa kwa kuheshimu dini? Uongo huo.

Kwanza mtueleze kwanini ikitokea ndoa imevunjika kwa sababu yoyote ile mnakuwa wagumu kuoa tena?

Vijana tuendelee na kampeni yetu KATAA NDOA. Ndoa ni utapeli.

Ndimi,
Sean Paul
Capripoint, Mwanza.
change-of-marital-status-unmarried-red-pencil-crossed-out-the-word-married-and-wrote-the-red-w...jpg
 
Wakilalamika lazima tuwashauri waachane na ndoa , na sisi single tukilalamika tushaurini tuoe , kwa apa tu jf kwa utitiri wa nyuzi la kulialia utajua wapi kuna vuja .
Kelele tu na matatizo ya akili usipoteze muda wako kumwambia mtu usioe sijui oa sababu mwisho wa siku mambo ni yale yale yapo vile vile na hutoyabadilisha kamwe.

Watu kila siku wataoa na kuolewa, wataachana wataoa tena na kuolewa.

Wanaojiita single wataishi kinyumba kama mke na mume wakishindwana wataachana na kwenda kuishi na mwingine.

Wewe ukijipa kazi ya mahubiri sijui oa mara usioe ujue umejipa kazi ya kujaza maji kwenye gunia lililotoboka. Dunia ipo kama ilivyo.
 
Yote ni sawa kabisa ,fanya yote ila ogopa pingu za maisha kma ukoma watu wapo kwenye mission zao .
 
Wengine huanza kupakaza eti hana nguvu za kiume. Wanaudhi sana. Watu hawaoi kutokana na sababu zao. Wengine hawataki pressure na stress kutoka kwa mwanamke, wanaona wako peace kuishi single
Mambo si magumu hivi, hutaki mke, kaa nawanaofanana na wewe mtaambiana mnayotaka kusikia. Una mke kaa na wenye ndoa mtaambiana mnayotaka kusikia.

Sasa hutaki ndoa, unaenda kubadilishana mawazo na wenye wake. Unategemea nini zaidi ya kuambiwa uoe.
 
Iv huwa ni mtu ataki mwanamke au ataki ndoa? Kwa sababu wanaotaka ndoa wana wanawake na wasiotaka ndoa wana wanawake pia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom