Kwanini watu wa imani wana uthubutu mdogo kwenye mambo ya maendeleo kuliko wapagani na wanaoamini Uchawi?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
7,591
18,356
Tukiangalia kwenye vitabu, watu wa imani wanamsitu wa ushahidi wa taarifa za kijasiri za watu kufanya mambo makubwa wakiwa na Mungu.

Cha ajabu katika uhalisia, hasa kwenye maendeleo tunaona no asilimia ndogo sana ya watu wanaotumia imani yako kuleta maendeleo ya kusisimua.

Leo ukienda makanisani na misikitini, wale matajiri wakubwa wanaotegemewa na kutukuzwa Wengi ni watu wenye makandokando, watu wenye tuhuma, uzurumati, etc. Na ajabu kabisa wengi wanaimani za miungu ya kijadi kisirisiri kuliko Mungu wa Kanisani/Msikitini.

Hata mtu akianza kufanikiwa katika jamii ya imani hawatakimbilia moja kwa moja kuona Mungu wao kamuwezesha, utasikia

Anafanya wapi siku hizi?
Muangalieni kwa makini?
Atakuwa katoa kafara ndugu yake aliyekufa?

Kimsingi kwenye suala la Maendeleo hata Prayer Worriers wengi wanaamini ushirikina kuliko uwezo wa Mungu.

Unadhani ni kwa nini imekuwa hivi.?
 
Weka orodha hapa ya ugunduzi na mafanikio yao kwa majina, ndipo uanze kuropokwa.

Kama huna data, huna haki ya kuongelesha kadamnasi.
 
Simple tuu,wanatafuta ufalme wa mbingu na sio ufalme wa Duniani.
Ufalme wa Mungu unahusisha.

Kuwa na nyumba bora za ibada

Kula vizuri ili akili ziwe safi kuweza kung'amua mema na mabaya.

Kusaidia masikini, yatima na wajane

Kulipa kodi ( Kaisali mpeni kaisali)

Kutoa Sadaka na zaka

Kufanya kazi za dunia (ajira na ujasiliamali) siku sita kwa wiki.

Kusafiri etc

Mambo yote hayo hayahitaji maombi au miujiza. Yanahitaji mtu awe na uwezo wa kumaendeleo na kiuchumi. Kumbuka kama hufanyi haya Yesu atasema ondoka hapa sikujui. Hauingii kwenye huo ufalme.
 
Kwa Sababu Sisi Ufalme Wetu Na Milki Yetu sio Ya Dunia Hii Sisi Ufalme Wetu Upo kwa YESU KRISTO.

MARAN ATHA - BWANA WETU ANAKUJA
 
Mathayo 25:37
Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

Mathayo 25:38
Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

Mathayo 25:39
Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

Mathayo 25:40
Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
 
Kwa Sababu Sisi Ufalme Wetu Na Milki Yetu sio Ya Dunia Hii Sisi Ufalme Wetu Upo kwa YESU KRISTO.

MARAN ATHA - BWANA WETU ANAKUJA
Akija ataanza na Interview ambayo moja ya utekelezaji wake ni matumizi ya pesa ulizopata katika harakati zako za maendeleo.

Kulisha wenye njaa, kutembelea watu magerezani, kuwavika wasio na nguo etc. Mambo hayo hayahitaji maombi au kusoma neno, yanahitaji pesa kuyatekeleza.
 
LIKUD Mzee wa kuamini uchawi na miti

Si bora hata Miti inatupa oxygen kuliko Mungu wako asie sikia maombi yako.

Ni miti hiyo hiyo ndio aliitumia Mtume wako kujitibu aliporogwa.

Miti hiyo hiyo ndio iliyo tumika kutengeneza majahazi yaliyo leta dini yako Africa .

Ni miti hiyo hiyo ndio iliyo tumika kutengeneza kitabu cha dini yako.

Bila hiyo miti mungu wako.asingeweza kuleta dini yake huku na wala usingeweza kuijua.

Bila miti hakuna uislamu ila miti imekuwepo kabla ya uislamu na itakuwepo baada ya uislamu na haihitaji uislamu ili kuwepo.

Ni miti hiyo hiyo ndio aliitumia ostaz wako wa madrassa kukupiga bakora ili ukariri mafundisho ya dini yako vizuri halafu leo unainyanyapaa miti

Unajua hata mungu wako.anakushangaa aisee.

MUOGOPE mungu mkuu.
 
Tukiangalia kwenye vitabu, watu wa imani wanamsitu wa ushahidi wa taarifa za kijasiri za watu kufanya mambo makubwa wakiwa na Mungu.

Cha ajabu katika uhalisia, hasa kwenye maendeleo tunaona no asilimia ndogo sana ya watu wanaotumia imani yako kuleta maendeleo ya kusisimua.

Leo ukienda makanisani na misikitini, wale matajiri wakubwa wanaotegemewa na kutukuzwa Wengi ni watu wenye makandokando, watu wenye tuhuma, uzurumati, etc. Na ajabu kabisa wengi wanaimani za miungu ya kijadi kisirisiri kuliko Mungu wa Kanisani/Msikitini.

Hata mtu akianza kufanikiwa katika jamii ya imani hawatakimbilia moja kwa moja kuona Mungu wao kamuwezesha, utasikia

Anafanya wapi siku hizi?
Muangalieni kwa makini?
Atakuwa katoa kafara ndugu yake aliyekufa?

Kimsingi kwenye suala la Maendeleo hata Prayer Worriers wengi wanaamini ushirikina kuliko uwezo wa Mungu.

Unadhani ni kwa nini imekuwa hivi.?
wale ni walimu wana kupa wewe usio na Imani na uliokata tamaa mbinu na ujasiri ili ukatoboa maisha 🐒
 
Mafundisho manyonge ndio sababu ya tatizo.
Sasa imagine mtu toka anapata akili anahubiriwa "nyumbani kwetu mbinguni,duniani tunapita tuko safarini kwenda mbinguni"
Yan wao mindset zao ni kwenda mbinguni tu now imagine huyu mtu atathubutu nini na wakat anaambiwa daily "vyote tunaviacha hapa duniani"

Yan mtu amezliwa, anasuburi 50 years hapa duniani kwenda tu mbinguni.

Pathetic preachers.
Idiotic mindsets za waumini wao as a result
 
Akija ataanza na Interview ambayo moja ya utekelezaji wake ni matumizi ya pesa ulizopata katika harakati zako za maendeleo.

Kulisha wenye njaa, kutembelea watu magerezani, kuwavika wasio na nguo etc. Mambo hayo hayahitaji maombi au kusoma neno, yanahitaji pesa kuyatekeleza.
SEMA NINI KAMA NIMEELEWA HII
 
Si bora hata Miti inatupa oxygen kuliko Mungu wako asie sikia maombi yako.

Ni miti hiyo hiyo ndio aliitumia Mtume wako kujitibu aliporogwa.

Miti hiyo hiyo ndio iliyo tumika kutengeneza majahazi yaliyo leta dini yako Africa .

Ni miti hiyo hiyo ndio iliyo tumika kutengeneza kitabu cha dini yako.

Bila hiyo miti mungu wako.asingeweza kuleta dini yake huku na wala usingeweza kuijua.

Bila miti hakuna uislamu ila miti imekuwepo kabla ya uislamu na itakuwepo baada ya uislamu na haihitaji uislamu ili kuwepo.

Ni miti hiyo hiyo ndio aliitumia ostaz wako wa madrassa kukupiga bakora ili ukariri mafundisho ya dini yako vizuri halafu leo unainyanyapaa miti

Unajua hata mungu wako.anakushangaa aisee.

MUOGOPE mungu mkuu.
Nadhani bora uabudu mtu anayetumia miti, kuliko miti.

Kimsingi kiwango duni kabisa cha kiibada ni kuabudu viumbwa badala ya aliyeviumba.
 
Mafundisho manyonge ndio sababu ya tatizo.
Sasa imagine mtu toka anapata akili anahubiriwa "nyumbani kwetu mbinguni,duniani tunapita tuko safarini kwenda mbinguni"
Yan wao mindset zao ni kwenda mbinguni tu now imagine huyu mtu atathubutu nini na wakat anaambiwa daily "vyote tunaviacha hapa duniani"

Yan mtu amezliwa, anasuburi 50 years hapa duniani kwenda tu mbinguni.

Pathetic preachers.
Idiotic mindsets za waumini wao as a result
Hapo nakuunga mkono kuna tatizo.
Yesu alisema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na mengine mtaongezewa sio hayafai au yatapungua.

Hapo alikuwa anamaanisha mavazi, chakula, na vitu vya dunia hii. Injili dunishi ni mkakati wa ibirisi pia.

Petro aliuliza tutapata nini tukifuata.
Yesu akaweka wazi kwanza tuaanza kupata vya duniani kisha uzima wa milele. Ufalme wa Mungu sio mbadala wa kuwa na vitu ambavyo kitakusaidia kubariki familia na wale wanaouhitaji.

Mimi huu ndio msimamo wangu wa sasa. Kwanza mbinguni ninajua ni haki yangu ya kimkataba nilioingia na Yesu siku nilipomuamini.
" Yeyote aniaminie amevuka kutoka hukumuni na kuingia uzimani".

Nakushukuru sana.
 
Tukiangalia kwenye vitabu, watu wa imani wanamsitu wa ushahidi wa taarifa za kijasiri za watu kufanya mambo makubwa wakiwa na Mungu.

Cha ajabu katika uhalisia, hasa kwenye maendeleo tunaona no asilimia ndogo sana ya watu wanaotumia imani yako kuleta maendeleo ya kusisimua.

Leo ukienda makanisani na misikitini, wale matajiri wakubwa wanaotegemewa na kutukuzwa Wengi ni watu wenye makandokando, watu wenye tuhuma, uzurumati, etc. Na ajabu kabisa wengi wanaimani za miungu ya kijadi kisirisiri kuliko Mungu wa Kanisani/Msikitini.

Hata mtu akianza kufanikiwa katika jamii ya imani hawatakimbilia moja kwa moja kuona Mungu wao kamuwezesha, utasikia

Anafanya wapi siku hizi?
Muangalieni kwa makini?
Atakuwa katoa kafara ndugu yake aliyekufa?

Kimsingi kwenye suala la Maendeleo hata Prayer Worriers wengi wanaamini ushirikina kuliko uwezo wa Mungu.

Unadhani ni kwa nini imekuwa hivi.?
Dini inafubaza ubongo
 
Back
Top Bottom