GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,806
- 9,634
Sijawahi kufika kwenye hizo nchi, lakini naamini nitafanya hivyo muda si mrefu.Lakini kwa stori za hapa JF, wengi wa wadau wanashauri kutokupita Zimbabwe kwa safari za kwenda Afrika Kusini.
Natamani, katika safari yangu, niende kwa ndege, lakini wakati wa kurudi, nitumie usafiri wa usafiri wa gari binafsi. Lengo ni ili kufaidi mandhari ya Mataifa mbalimbali, hasa Namibia, Botswana, Zimbabwe, Zambia, na Malawi, kama hakutakuweko na kizuizi cha kupita huko.
Kama ninazo nyaraka zote zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na za kununulia gari South Africa, bado kutakuwepo na ulazima wa kukwepa kupita Zimbabwe?
Kama itawezekana kutumia route itakayoniwezesha kupitia nchi zote hizo, ni mambo gani ya kuzingatia ili kuepuka usumbufu usio wa lazima?