Kwanini Watanzania hatuwazi vitu nje ya box??

maccavel

Member
Jan 17, 2025
5
5
Habari members of great thinkers,

Leo nikiwa katika matulizo yangu ya kujiandaa na mtihani,ndipo sauti inanijia kichwani ikinena kwanini sisi?

Unajua sisi vijana tulio wengi tunawaza kila siku kuhusu mapenzi,kiasi kwamba nyuzi mbalimbali humu jamiiforum zimejaa ngono tu,yan jamiiforum ya leo sio Ile ya ma great thinkers akina Pascal Mayalla, Nowadays mtu akikuona upo jamiiforum anaona ni sawa tu yule wa TikTok, Facebook Yani jamiiforum inakwenda kuanguka kabisa ule umahiri wake,tubadilike vijana sio kila wakati tunawaza ngono,

Sasa katika kundi hili la vijana,Kuna wengine mawazo na mitazamo positive humu jamiiforum ambayo ni muhimu kwa taifa

Sasa niende kwenye Ile sauti iliyonijia,hivi ni kwanini waigizaji pamoja na wadau wa filamu wakaanza kuigiza filamu ambazo zitakuwa ni worldwide,kwasababu kila siku movie ni zilezile mara joka la kijiji,mara mama wa kambo, that's why hatupigi hatua,je ni kweli mmeshindwa hata kuja na wazo la kuigiza movie maji maji war,Serikali ya mama enu iwatafutie makampuni ya kijerumani hizo movie ziigizwe,

Mnashindwa kuja na full movie kuhusiana na mapinduzi tukufu ya Zanzibar,mkaigiza kinjiketile Ngwale alivyokuwa,au namna Mkwawa alivyokuwa pasua kichwa dhidi ya wajerumani,mkaigiza maisha ya Babu yangu Mazengo wa pale Mvumi, movie ikawa in Swahili na English ili iende mbali kimataifa

Kwanini tusijifunze hata kwa wenzetu china na movie zao za kihistoria mbona ni nzuri na tunazifuatilia kweli kweli,au kule ulaya Escape from Sabibor,watu tunafatilia sana movie kama hizi alafu hata hatujifunzi kitu

Mje na movie ikaitwa Maji maji war, movie ikahusisha characters wa kijerumani na Watanzania mkitumia mishale na mikuki,hamuoni mtakuza soko la filamu Tanzania, Serikali imewapeleka Korea lakini hatuoni mabadiliko mwambieni mama enu akuleteeni mashirika ya kijerumani mfanye nayo kazi,

Contest zipo nyingi sana mfano independence movement in Tanganyika the way Tanu ilivyo spread,au about our Geography,tuna dinnosaria yupo ujerumani tunashindwa kuja na mpango mkakati namna tutakavyo mfanyia characterization, about our culture , about our technologies.sasa kila siku mama kimbo kimbo,zahanati ya kijiji,mara ukimwi unaua, tubadilike

Bodi ya filamu nao wametulia tu kiasi kwamba hawana hata mbinu za kukuza soko la filamu kimataifa

Vijana tuna mawazo mengi ni vile hatupewi nafasi, sio tu filamu hata uchumi,mazingira,michezo,elimu,Kuna namna tunaweza leta mabadiliko Kwa kiasi chake,

Haya ni mawazo tu yalinijia kwahiyo mnakaribishwa kunikosoa na najua sio kila kitu kinachokuwa kichwani Kwa mtu ni sahihi,huenda mawazo yangu yakawa ni nothing kabsa lakini ni mawazo tu,

Watu wa filamu nimewapa content,si ajabu tukaja kugawana umaskini baada ya filamu kama hizi kutokea even ten years ahead,tupeana asilimia even Moja Moja

Mwisho kabisa niwatakie asubuhi tulivu.nakoma kuandika nikiwa nasubiri kufanya mtihani wangu hapo baadae✍️✍️✍️
 
Hatuna ubunifu sisi na mapenz mapenz na sisi napenda kuigiza ila hakuna story nzur za kueleweka ni mapenz na vitu vya ajabu ajabu

Africa tunasafar ndefu kwenye maswala ya films
 
Tasnia ya filamu in wadau wengi Sana pengine tumeimarika idara ya waigizaji, lakini bado idara zingine pia Gharama ni kubwa sana kutengeneza filamu za namna umezitaja labda ziwe chini ya kiwango saana ambazo zitachefua....
 
Tasnia ya filamu in wadau wengi Sana pengine tumeimarika idara ya waigizaji, lakini bado idara zingine pia Gharama ni kubwa sana kutengeneza filamu za namna umezitaja labda ziwe chini ya kiwango saana ambazo zitachefua....
Hatuna hela lakini za kununulia magoli ya akina chasambi tunazo sio
 
Hatuna ubunifu sisi na mapenz mapenz na sisi napenda kuigiza ila hakuna story nzur za kueleweka ni mapenz na vitu vya ajabu ajabu

Africa tunasafar ndefu kwenye maswala ya

Hatuna ubunifu sisi na mapenz mapenz na sisi napenda kuigiza ila hakuna story nzur za kueleweka ni mapenz na vitu vya ajabu ajabu

Africa tunasafar ndefu kwenye maswala ya films
Mkuu Kuna taarifa Jana ilinivunja mbavu, wakati bukinafaso wakizindua magari yao ya umeme,sisi tunazindua anwani za makazi
 
Back
Top Bottom