Kwanini Watangazaji wa Redioni wanatumia nguvu kubwa mno kutushawishi tucheze Bahati Nasibu zao?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,948
119,221
Mtangazaji wa Bahati Nasibu ya EFM ( Mshindo Milionea ) utamsikia.....

Fanya upesi ucheze Mshindo Milionea kwa kuweka tu Shilingi Elfu Moja yako ushinde Shilingi Milioni Moja ili Kesho Baba mwenye Nyumba wako akakufukuza kwa Kukudai Kodi yake na Ukaibika Mtaani.

Mtangazaji wa Bahati ya Clouds FM ( Mchongo Pesa ) utamsikia....

Tafuta popote pale Shilingi Elfu Moja ili ucheze Mchongo Pesa uweke Heshima Mjini kwa Kujipatia Shilingi Milioni Moja yako.

Mtangazaji wa Bahati Nasibu ya Radio One ( Bukutua ) utamsikia....

Kufa Masikini Tanzania unajitakia Mwenyewe hebu haraka cheza Bukutua na ujipatie Shilingi Milioni Moja na Maisha yako yabadilike ghafla Mtaani wakukome.

Mtangazaji wa Bahati Nasibu ya TBC Taifa ( Cheza Pesa ) utamsikia......

Huna Pesa ya Kumtolea Mahari Mchumba wako upesi sana Cheza Pesa ili upate Hela yako Shilingi Milioni Moja na ukalipie Mahari ili uweze Kummiliki kihalali huyo Mtoto mzuri wa Watu uliyenae kabla Wajanja hawajamnyakua.
 
IMG_3808.jpg
 
Wataanzani tuko milioni 60...assume watanzania 1000,000 wakupe tsh 1000..jumla ni billioni kwa siku 1...toa running cost labda millioni 200.. imebaki million 800..wape washindi milioni 100...inabaki 700..toa hapo 18% ya million 700 kama kodi..alafu kinachobakia ndio chao.....
 
Media nyingi bado hazijasimama so ile ni moja ya strategy ya kuongeza mapato

Me naona ni sahihi wanavyofanya coz hulazimishwi ni ww tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom