Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 561
- 1,834
Ulishawahi kutoka na mwanamke wa mjini sister du fulani out? Akiletewa menu anaagiza nusu kuku na chips alafu anakula kiupaja kimoja na vichips kadhaa anajifuta na tishu kwa mikogo vingereza vingi alafu anakwambia ameshiba! 🤔
Wanaume tumeumbwa mateso hadi kwenye ndoa yanatukuta haya. Leo naongelea wanawake walioolewa au wanaoshi na wanaume kama familia, kwanini wengi wao wana tabia hii? KUTUPA CHAKULA!!! 😭
Nikijitolea mfano mimi binafsi nimetoka familia masikini, Mungu kanijaalia nna kipato cha kubadilisha mboga kwa sasa. Kwakuwa chanzo kikuu cha mapato ni mshahara basi huamua kununua vyakula vya jumla kila mwisho wa mwezi mf. mchele,unga, mboga kama maharage, dagaa, samaki, nyama ya ng'ombe, kuku n.k yani kiufupi mwisho wa mwezi friji inakuwa top kwa mazagazaga na huwa tunapanga kabisa na mke wangu anunue vitu kiasi gani lakini matumizi ya vitu hivi yanakuwa ya hovyo sana hadi kupelekea kitu fulani kuisha mapema kabla ya muda mliojiwekea. Na hata ukimuuliza kuhusu pesa ya matumizi uliyompa tofauti na ya manunuzi ya vitu hivyo utaambulia patupu.
Kuna jambo wanawake hawawezi kubajeti kabisa hasa kipimo cha chakula. Unakuta mchana wanapika ugali mkubwa hadi jioni unatoka kazini unakuta hotpot limejaa ugali na mboga kibao zimebaki wote wameshakula na mimi huwa sili nyumbani mchana siku za kazi. Usiku pia wanapika wali kibao unabaki, asubuhi hauliwi wote sababu kuna mkate au mwanamke kajisikia kupika tambi au chapati, mchana unakuta sufuria limelowekwa na mpunga kibao mwisho wa siku wanapewa kuku wale....
Nimeongea kwa ujumla wanawake maana hiki ni kilio cha wanaume wengi tunaofatilia mambo ya jikoni. Siwafichi mimi huwa nafatilia mambo ya jikoni.
Nna rafiki zangu wengi, ndugu zangu na jamaa wanaoishi maisha ya shida sana, mfano jana nilipigiwa simu na rafiki yangu ananiambia hadi muda huo (saa 2 usiku) hajajua watoto watakula nini akaniomba nimsaidie kumtumia buku mbili tu japo anunue mkate. Si kwamba napesa nyingi lakini najua uhalisia wa anachoniambia sababu haya maisha nimeyaishi nilipambana nikamtumia hela ya kula siku hiyo.
Nikirudi kwa mke wangu mimi hajali kabisa unaweza kushangaa baada ya siku 15 tu anakwambia mchele karibia unaisha, namuuliza mmetumia mchele kilo 30 kwa siku 15?! Jibu lake rahisi anajibu 'unadhani mimi naumwaga, si watoto wako wanakula!' Mwanamke mwenyewe katoka familia hizi hizi kama zetu sijui kwanini hana uchungu!
Lakini si wote kuna wanawake wanajua kubajet aiseee... Kama shemeji yangu mama Alice nakumbuka wakati huo tunaishi nae nyumba moja na mume wake(rafiki yangu). Huyu mwanamke hatumii kwasababu vipo tu, nisiseme mengi.
Kama kusema nilishasema sana sasa hivi naumia tu maana ukizidi kuongea hawachelewi, utasikia "We mwanaume una gubu kweli, mambo ya jikoni yana kuhusu nini?"
Ah! Basi bana, namwachia Mungu 😢