Kwanini wanatenguliwa Wakurugenzi wa Halmashauri pekee na Si wa taasisi?

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
903
1,474
Serikali ya CCM Kila siku inatumbua wakurugenzi wa Halmashauri, ambapo naona ni uonevu kwa kiasi Fulani.

Serikali aigusi wakurugenzi wa taasisi za serikali, ambao ni wakurugenzi wa vitengo mbalimbali, ambao wengi hawana utendaji mzuri hata kidogo, na Wana mishahara mikubwa, mara nne ya mishahara ya wakurugenzi wa Halmashauri, na wakurugenzi Hawa wa vietengo mbalimbali wa taasisi wamekuwa wakikaa muda mrefu sana katika vitengo vyao na kusababisha utendaji mbovu wa mazoea.

Wanawaonea wakurugenzi wa Halmashauri, naomba muangalie utendaji wa wakurugenzi wa taasisi, wengi wamebweteka.

Tunaomba Hili suala liangaliwe, wakurugenzi wa halmashauri wanaonewa, serikali ikaangalie wakurugenzi wa vitengo wa taasisi, ambao ni Wana utendaji wa hivyo, na wanafikiria pesa tu muda wote

Pia soma: Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Kassim Seif Ndumbo
 
Back
Top Bottom