Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,085
- 4,888
Mwaka 2004 Manispaa ya Sumbawanga ilichukua mashamba ya wananchi huko kizwite na kufanya uthamini na kuwalipa fidia wahusika.
Baadae ikapima viwanja na kuviuza kisha kuvimilikisha kwa walionunua na kuwapatia hati milki za miaka 66. Ghafla kumeibuka wimbi la watu wanavamia hivyo viwanja na kudai wazee wao walifariki kabla ya kulipwa fidia hivyo wanadai fidia.
Maafisa ardhi badala ya kujiridhisha kuwa wanaodai fidia ndio kweli wenye mashamba na pia kama kweli wazazi wao ndio walikuwa wenye hao mashamba na hawakulipwa fidia mwaka 2004 kwa kuangalia majedwali ya fidia ambayo yapo ofisini kwa mkuu wa wilaya wao wameamua kuwalazimisha wamiliki wawalipe fidia hao wanaodai.
Kama manispaa ndio iliyochukua hayo mashamba suala la fidia ni la manispaa na sio la wamiliki manispaa kama kweli hao wanaodai walisahaulika basi manispaa ni wajibu wao kuwalipa fidia isiwatwishe mzigo wamiliki.