Kwanini wabunge wa CCM Hubakia Bungeni?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,353
38,588
Hii si mara ya kwanza kwa wabunge wa CCM kubakia bungeni wakati wabunge wa vyama vingine wanapotoka nje ya ukumbi vinapofanyika vikao vya bunge kupinga jambo fulani. Kubaki kwao na kuendelea na vikao vya bunge huwa kuna ujumbe fulani tunatakiwa tuupate sisi wananchi tuliowachagua.

Kwa mfano wakati UKAWA walipotoka bungeni kupinga kubadilishwa kwa mfumo wa serikali uliokuwa kwenye Rasmu ya Katiba iliyowasilishwa Bungeni na Tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya wabunge wa CCM walibakia bungeni na kuendelea na vikao vyao.

Lakini likatokea tatizo la kufikia akidi ya kura toka Zanzibar, hapo tukaona kila aina ya sarakasi ili kukidhi haja ya waliobakia kikaoni. Na mojawapo ya sarakasi hizo ni lile la kusema kuwa wajumbe waliokuwa Hajji nao pia walipiga kura!! Swali la kujiuliza kama wao walijua kuwa ni lazima hoja zao zipitishwe ije mvua lije jua ni kwa nini walipoteza muda na fedha za wananchi kujifanya wanafanya majadiliano ilhali walikuwa wamebaki wenyewe?

Hivi sasa iko hoja ya Wabunge wa upinzani kukataa kuongozwa na Tulia Akson kama Naibu spika wa bunge hilo. Kila siku tunaona wabunge wa upinzani wakitoka na wa CCM wakibakia bungeni. Lakini wanabaki wakifanya nini?

Kitu gani cha maana wanachofanya wabunge wa CCM hadi kuhalalisha kubaki kwao bungeni?
 
Sasa unaataka watoke ili wakuliridhishe wewe? cha kujiuliza kwanza kabla ya kuuliza nafikiri ungeuliza kazi ya wabunge inayowapeleka dodoma ni nini? harafu ukipata jibu uendelee na maswali mengine matatu kabla ya kufikia hili swali ulilouliza.
 
CCM walipelekwa ili kuipigia makofi serikali
 
Sasa unaataka watoke ili wakuliridhishe wewe? cha kujiuliza kwanza kabla ya kuuliza nafikiri ungeuliza kazi ya wabunge inayowapeleka dodoma ni nini? harafu ukipata jibu uendelee na maswali mengine matatu kabla ya kufikia hili swali ulilouliza.
Kuna tija yoyote inapatikana kwa watanzania kwa wao kubakia bungeni?
 
Je kunatija yoyote kwa watanzania kwa kuziba midomo?
Hapa hoja ni wabunge wa CCM. Hao mashujaa wanaokataa kuburuzwa anzisha bandiko lao kama unataka tujadiliane kuhusu wao. jee kuna tija yoyote kwa wabunge wa CCM kuendelea na vikao vya bunge, au wanasukumwa na Posho wanazolipwa?
 
Hongera maana hata yule anayetaka Tujenge sanamu ya Diomond naye anatetea wananchi wake

Tatizo lakuwa brainwashed ndo hilo, kila mtu anajenga hoja ile ile ya sanamu la Diomond. Hivi huko wote mnafikiri kwa kichwa kimoja? kwanini msiweze jenga hoja kwa vichwa tofauti tofauti. Wote kwa wakati mmoja wengi wenu mna password za vijimaneno vile vile ? Na hata hivyo tutaendelea kuwakumbusha mawazo yenu sio yako sahihi na ya wengine pia hayako vilevile sahihi knachotakiwa ni hoja na sio u radicals.
 
Hapa hoja ni wabunge wa CCM. Hao mashujaa wanaokataa kuburuzwa anzisha bandiko lao kama unataka tujadiliane kuhusu wao. jee kuna tija yoyote kwa wabunge wa CCM kuendelea na vikao vya bunge, au wanasukumwa na Posho wanazolipwa?

ha ha ha
dude anayetaka maono yake tu kuwa sahihi. Kazi ya wabunge nini? je wabunge wa ccm sio wabunge?
 
Kuna tija yoyote inapatikana kwa watanzania kwa wao kubakia bungeni?

Wale wa CCM waliomo ndani ya bunge wanasikiliza na kusoma bajeti kuona kama imegusa maeneo ya majimbo yao na kuipigia kura ya ndiooooooooooooooooo wakiona mambo safi.Hao wazururaji wa UKAWA wanaoenda kutalii bungeni na kutoka na kujilia posho za malazi na usafiri za bure wakiwa DOdoma ndio hawana tija kwa majimbo yao.

Wangekuwa wakweli kwa nafsi zao kuwa hawaoni chochote cha kufanya Dodoma ilitakiwa wajirudie zao tu majimboni ili Walipa kodi wasiendelee kuumia kwa kuwalipia malazi na usafiri wakati hawana kazi ya kufanya kule.Hawasomi hayo makaburasha ya bajeti ,wala hawawakilishi na kuongelea lolote kuhusu majimbo yao!!

Wewe mtu wa UKAWA jiulize mbunge kama Msigwa Iringa kuna matatizo kibao,umaskini wa kupindukia hajaongelea hata jambo moja la matatizo ya watu wa Iringa mjini bungeni.

Wale wa CCM wakicheki bajeti wakiona mambo safi majimbo yao yako covered kazi inayobaki kwao wakiulizwa bajeti ipite au isipite ni kupiga kelele kwa nguvu ndiooooooo ipite.Hata wanakuwa hawana hata haja ya kuchangia sababu wakisoma wakiona iko safi wachangie nini ni kusubiri tu kuipitisha.

Lakini UKAWA kwa kweli ni tatizo.Unakuta badala ya kusoma bajeti wanasoma magazeti kuangalia yameandika nini kuhusu Lugumi,Badala ya kuchangia matatizo ya majimboni kwao unakuta wanasimama wanataka BUNGE LIONYESHWE LIVE!! ni wapotezaji muda hawajikiti kwenye hoja bora kabisa wamesusa.
 
Watoke ili wafukuzwe? Ujui kua wameshikiliwa akili zao?
Kwahiyo wanaotoka nao wakigoma wanafukuzwa, kwa maana haiwezekani wote wawe na msimamo mmoja? sasa ni nini tofauti kati ya wote wanaotoka na wote wanaobaki.
Hapo kama uko uhuru lazima useme wote wanaotoka wmelazimishwa na wote wanaobaki nao wamelazimishwa. Hapo atleast ungekuwa na hoja
 
ha ha ha
dude anayetaka maono yake tu kuwa sahihi. Kazi ya wabunge nini? je wabunge wa ccm sio wabunge?
Wabunge wa CCM wanatimiza hayo majukumu ya kibunge? Hebu fikiria yule mbunge aliyetaka maelezo kwa nini Askari hawawapigii saluti, unadhani saluti kwa wabunge ndiyo matatizo yanayowakabili watanzania?
 
Wewe mtu wa UKAWA jiulize mbunge kama Msigwa Iringa kuna matatizo kibao,umaskini wa kupindukia hajaongelea hata jambo moja la matatizo ya watu wa Iringa mjini bungeni.
Iringa kama Mkoa au Jimbo la Iringa mjini analotoka Msigwa? Unadhani umaskini wa kutupwa unaondolewa kwa kuongelewa au kwa kufanyiwa mikakati yakinifu?
 
Wabunge wa CCM wanatimiza hayo majukumu ya kibunge? Hebu fikiria yule mbunge aliyetaka maelezo kwa nini Askari hawawapigii saluti, unadhani saluti kwa wabunge ndiyo matatizo yanayowakabili watanzania?

Kwanini mna hoja ya vijimaneno vile vile wote? eti kupiga saluti yani password ya vijimaneno ni vile vile. Hapo ndo nalazimika kusema kuna mtu ana wa brainwash.
Kwa taarifa yako huyo ni mbunge na demokrasia ndo inataka hivyo, watu wakiamua kuchagua hata mbuzi kuwawakilisha hiyo ndo demokrasia. Wewe kama unapigania kweli demokrasia yakupasa kuheshimu mawazo ya huyo mbunge , ukubali kutokubaliana naye na sio kuhoji uhalali wake wa kibunge.

Ukianza kuhoji mawazo yake na uhalali wake ndo u radical huo na inakuwa si demokrasia kama unayolilia.
Wala hupaswi kuhoji uhalali wa kibunge wa bunge waliobaki bungeni maana demokrasia ni kuheshimu mawazo hata ya mjinga kama tu huyo mjinga kachaguliwa kidemokrasia.

Demokrasia sio ya kwamba kipi ni best na chatakiwa kufanyika BIG No. Demokrasia ni kuheshimu mawazo ya wananchi walio wengi hata kama hayo mawazo ni ya kipuuzi.
 
Wabunge wa CCM wanatimiza hayo majukumu ya kibunge? Hebu fikiria yule mbunge aliyetaka maelezo kwa nini Askari hawawapigii saluti, unadhani saluti kwa wabunge ndiyo matatizo yanayowakabili watanzania?

unaongelea tatizo la mbunge mmoja kati ya wabunge karibu mia tatu wa CCM!!

CCM haina kitu kinachoitwa COLLECTIVE STUPIDITY kama ambavyo yaweza onekana kwingine ambako jambo likiwa la kijinga linashabikiwa na wote.Unajua ni aibu mambo yanayofanywa na UKAWA.
 
CCM haina kiytu kinachoitwa COLLECTIVE STUPIDITY.
Ingawa Kiingereza kinanipiga chenga, lakini inakuwaje kuna yule mbunge anayetaka tujenge Sanamu la Diamond na yule mwingine tujenge uwanja kama kumbu kumbu mahali Magufuli alipoanzia kupiga Push Ups wakati wa Kampeni wote wanatoka CCM. Hivi unamuelezeaje Lusinde? hiyo "Kollective Stupidity" unaipimaje?
 
Iringa kama Mkoa au Jimbo la Iringa mjini analotoka Msigwa? Unadhani umaskini wa kutupwa unaondolewa kwa kuongelewa au kwa kufanyiwa mikakati yakinifu?

Hiyo mikakati yakinifu ya kuondoa huo umaskini Iringa mjini ndiyo alitakiwa asimame achangie kwenye hiyo bajeti ili iwekwe na iwekewe hela tayari kwa utekelezaji !! Lakini huyo yuko anazurura Dodoma.
 
Hiyo mikakati yakinifu ya kuondoa huo umaskini Iringa mjini ndiyo alitakiwa asimame achangie kwenye hiyo bajeti ili iwekwe na iwekewe hela tayari kwa utekelezaji !! Lakini huyo yuko anazurura Dodoma.
Unajua kwamba bunge haliwezi kubadili bajeti inayoletwa na Serikali bungeni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…