Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,102
- 6,241
Habari zenu
Hivi ulishawahi kukaa chini na kujiuliza kwanini amri ya kwanza ya Mungu kwenye Torati imekemea suala la Ushirikina kabla ya kukemea uuaji, uongo, ushoga, uzinzi, wizi n.k?
Kwanini iwe ni suala la Ushirikina? Kwanini vilevile kitabu cha Quran kikaja tena kupigilia msumari ww Moto kwa kusema Mungu anasamehe dhambi zote ila Ushirikina?
Rejea nami katika kitabu cha kutoka Sura ya 20:
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu
Ama ukirejea katika kitabu kitakatifu unakutana na amri hiyo hiyo katika Sura ya 17:23
"Na Mola wako mlezi ameamrisha msimuabudu yeyote ila YEYE tu"
Kama hiyo haitoshi ikaelezwa tena kuwa
Quran 31:13
"Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa."
Kwanini Ushirikina iwe ndio dhambi kubwa?
Ngoja nitolee mfano wa kilimwengu ili twende sambamba
Kuna uzi humu Jamii Forum unaooleleza kuhusu mwanamke aliyependwa sana na Mumewe, akapewa kila kitu kuanzia chakula,gari, zawadi mbalimbali na pia watoto!! Kifupi mumewe alimpenda mnoo na wakaishi vizuri tu ila yule mwanamke akamsaliti mumewe kwa kutembea na mfanyakazi mwenzie wa ofisini, za mwizi ni arobaini,mumewe akajua...tokea hapo mumewe akaupoteza upendo wote aliokuwa nao.Wachangiaji wa mada wakasema kuwa huyo mwanamke ametenda kitendo kiovu na kibaya mno kwa mume aliyempenda sana na kumtendea kila aina ya wema ila yeye aliamua kumlipa malipo ya usaliti, wengine wakaenda mbali wakasema ni ngumu kwa huyo mwanaume kupona majeraha yake.Na kibaya zaidi yule mwanamke akasema kuwa upendo uliokuwepo slzamani wote uliisha.
Kwanini?
Jibu ni kuwa Mwanamke aliamua kumshirikisha mumewe ( ambaye ni mmiliki halali kwake) na mwanaume mwingine. Wanaadamu tuna wivu mkali sana na Mungu aliyetuumba ana wivu mkubwa zaidi yetu wanaadamu kiasi hataki kusikia kuwa mwanadamu amemshirikisha na kitu chochote kile.Yeye ndiye mmiliki halali wa viumbe vyote hapa duniani na mbinguni hivyo anaghadhibika na kuchukia mno pindi mwanadamu anapoabufu miungu mingine na kumuacha YEYE
Kutokana na hili Mungu akauandaa Moto mkali wa Jahannam kwa ajili ya wote ambao watakufa wakiwa hawajaitubia hii dhambi ya ushirikina.
Mungu ndiye mtoa Riziki kwa viumbe vyote ila mwanadamu anaona aende akaabudie mashetani kupitia waganga ili apate rizki anbayo inatoka kwa Mungu. Kitendo kama hiki ni mifano katika mifano mingi ya ushirikina, yaani kuamini kwamba kuna mungu/miungu mingine inayoweza kukupa riziki pamoja na MUNGU muumba ndio mfano wa ushirikina.
Ukiichukua haki ya MUNGU na kumpa kiumbe au kitu chochote kile hapo utakuww umetenda dhambi ya ushirikina. Fikiria kuwa ikiwa mwanadamu tu anachukia sana pindi akijua kuwa mkewe amemsaliti kwa mwanaume mwingine ,vp MUNGU akiona kuwa unaabudu mizimu ,majini na vinyamkera vingine pamoja NAYE? Hasira zake juu yako zikoje, wakati yeye ndiye aliyekuumba toka tumboni mwa mama yako, akajaalia ukazaliwa salama,akakujaalia macho,masikio n.k ambavyo huvilipii chochote na akakupa hewa na chakula bure, akakupa na uzao ila mwisho wa siku ukaona umlipe kwa Kumshirikisha YEYE na miungu mingine.Ukaona vyema ukasujudu kwenye miti mikubwa huko porini kuiomba mizimu ikujaalie ufanikiwe biashara zako, ukaona bora ukasujudie kaburi la babu yako umuombe akutatulie matatizo yako, ukaona bora ukachonge sanamu uwe unalisujudia na kuliomba usiku na mchana likufanyie wepesi mambo yako ,ukaona ni bora sifa ya uungu ukampe mwanadamu mwenzako aliyezaliwa na mwanamke kama wewe ili akupe uzima wa milele na ukamsahau MOLA WAKO MLEZI!!
Mfano wa mwisho wa Ushirikina ni huu.
Ni mfano wa tajiri mwenye biashara aliyeajiri wafanyakazi wengi kisha akawa anawalipa na kuwahudumia kila kitu ila jioni wale wafanyakazi wakishamaliza kuuza bidhaa za boss wao,mauzo yote wanakwenda kumpa mtu mwingine ambaye hata hausiani na ile kampuni tena wakidai yule mtu ndiye boss wao.
Hivi unadhani huyu tajiri ataghadhibika na kuchukia kiasi gani kww tendo hilo?
Ukishajua haya ndio utajua kwanini amri ya kwanza MUNGU amekemea kuhusu KUSHIRIKISHWA NA YEYOTE AU KITU VHOCHOTE KATIKA MAMLAKA YAKE.