Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 45,440
- 64,251
Watu wengi huwa wanawalaumu Wayahudi na kuwazushia conspiracies nyingi sana kwamba wamesababisha matatizo makubwa kwa dunia, mimi nafikiri hii ni tabia ya ukasuku wa watu kukariri tu mambo yanayosemwa bila kuyatafakari.
Kama kuna taifa ambalo limechangia madhila makubwa duniani ni Ujerumani (japo wametubia baadhi). Tafakari baadhi ya mambo waliyohusika nayo ambayo yalileta mabalaa makubwa kwa dunia yetu.
1. Walikuwa kichochezi kikubwa kuanza kwa vita vya kwanza vya dunia(WW I) kwa maslahi yao binafsi.
2. Walikuwa waanzilishi wa moja kwa moja wa vita vya pili vya dunia(WW II)
3. Walihusika na genocide kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani, wakiwaua mamilioni ya Wayahudi.
4. Walihusika kugawanywa rasmi kwa bara la Africa kuwa makoloni ya Ulaya kupitia mkutano wa Berlin 1884/85.
5. Kupitia raia wake wawili Karl Marx and Freidrich Engels ambao wanachukuliwa kama waanzilishi wa falsafa ya ujamaa kitaifa wamehusika kuibuka kwa watawala wenye idea ya ujamaa ambayo imeharibu sana nchi nyingi duniani mpaka leo hii.