Kwanini tusimuache Magufuli afanye kazi?

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SINA tatizo la msingi na wananchi wa kawaida kuhoji na kulalamika juu ya uamuzi wa aina mbalimbali anaochukua Rais John Magufuli akiwa katika harakati za kutekeleza ahadi zake kama mgombea wa urais. Sina tatizo kabisa na watu ambao hawajawahi kuwa sehemu ya serikali au walio nje ya serikali (ambao hawakuwahi kushika nyadhifa kubwa) wakilalamika na kuhoji mambo mbalimbali na hata kupinga uamuzi wowote.

Hata hivyo, nina tatizo la msingi kabisa ninaposikia viongozi au watendaji ambao siku chache nyuma waliwahi kushika nafasi kubwa za uongozi wakianza kupinga mwelekeo na utendaji wa Serikali ya Magufuli. Tanzania ina Rais mmoja tu ambaye ndiye anadhamana ya kuliongoza taifa kwa miaka mitano ijayo. Yeye ana jukumu la kusimamia serikali yake anavyopenda.

Sasa inapotokea watu – ambao labda waliitaka nafasi hiyo hiyo ya Magufuli – wanaanza kumkosoa na kuhoji uwezo wake wa kiuongozi ni lazima watu hawa wakataliwe na kukemewa. Wakataliwe kwa sababu wao hawakuchaguliwa na mipango yao ya kuitaka nafasi ile ya Magufuli ilishindikana. Hili ni matokeo ya demokrasia tu.

Kama Magufuli ataanza kuwasikiliza hawa na kujali wanayoyasema na hivyo kutekeleza wanayoyataka ina maana nchi itakuwa na uongozi usio na mwelekeo. Chukulia kwa mfano mtu ambaye amekosoa ubomoaji wa waliojenga kiholela, au anayehoji watu kuchukuliwa hatua kali, au wakwepa kodi kubanwa; hivi huyu mtu anataka kutuambia kuwa yeye angekuwa Rais hawa wakwepa kodi angefanya nao nini? Angeshikana nao mikono na kuimba “kioo kioo alikivunja nani?” Hivi ambaye anapinga hizi bomoabomoa ina maana yeye angewaacha watu waendelee kujenga kiholela kwa sababu kuwabomolea nyumba zao watu watalia na kupata mishtuko? Hivi si ndiko nchi ilikuwepo huko kwa miaka karibu ishirini hii?

Hivi, leo hii wakuu wa TRA wameng’olewa, wakuu wa Uhamiaji matatani, Takukuru bosi katimuliwa halafu watu wanahoji “ooh anafanya hivyo kwa sababu hawa wametuliwa na mwingine” hivi ina maana wao wangeshika nafasi ya Magufuli leo hii watu wa TRA, Uhamiaji, Takukuru wangeendelea kupeta? Au wenzetu wangefanya nao nini? Au wafanyabiashara wajanja wajanja (waliokwepesha makontena yao) wenzetu wangefanya nao nini? Ina maana wasingeenda kuangalia kinachotokea Bandari? Wasingemfukuza mtu hata mmoja? Wasingemhamisha anayetakiwa kuhama? Na kwa hakika wasingeagiza watendaji wabovu wasifikishwe mahakamani?

Kama kweli wana tatizo na Magufuli ndugu zetu hawa waseme wao wangefanya nini na kama wanataka kuwatetea hawa wakwepa kodi watoke hadharani na waseme wanawatetea kuliko kujificha kwenye pazia la kujifanya wanatoa maoni ya ushauri? Ushauri gani wa kumshauri kiongozi mkuu wa nchi asifanye kazi aliyosema atafanya? Hivi Magufuli aliposema anataka kwenda kutumbua majipu walifikiria anasema kama utani au ngonjera ili wengine waje na beti zao nao wajibu?

Mbona – kama nilivyosema huko nyuma – Magufuli bado hajaanza kazi mwenyewe hasa hasa? Hivi walimtaka Magufuli aingie na kuendelea kana kwamba mambo yako sawa tu? Au wenzetu walikuwa hawafuatilii muda ule wa kampeni yale ambayo Magufuli aliyasema? Au walidhani alikuwa ni mwanasiasa kama wengine ambao wanasema wasiyomaanisha na wanamaanisha wasiyoyasema? Magufuli alisema alichosema na sasa anakifanyia kazi na hawa “magenius’ wetu wanataka ageuke alivyosema?

Binafsi naamini kabisa kuwa hata wapinzani wanapokosoa wanakosoa kwa haki yao lakini hawawezi kukosoa na kumtaka Magufuli asifanye kazi. Sijamsikia mpinzani wa kweli ambaye anapinga Magufuli kushughulikia viongozi wabovu, wakwepa kodi, watumia madaraka vibaya na akabakia mpinzani. Mpinzani ambaye anataka Magufuli awaonee huruma, awaogope baadhi yawatu (wawe wafanyabiashara au vinginevyo) huyo si mpinzani. Na kiongozi yeyote ambaye anatoa ushauri ambao unaonekana una lengo la kupunguza kasi na makali ya kazi ya Magufuli sidhani kama analitakia taifa ahueni au anawatakia (anajitakia) yeye ahueni mahali fulani.

Binafsi kama nilivyosema huko nyuma, naunga mkono harakati za mabadiliko na ninaziunga kwa asilimia mia moja na moja. Magufuli asirudi nyuma, asisite, asitishike na asiwaangalie machoni wale ambao wanakutana na mkono wa sheria. Magufuli asirudi nyuma kwa sababu Tanzania imekuwa na muda wa kutosha wa viongozi vigeugeu, uchwara na wenye kuendekeza “uenzetu huu” kiasi kwamba wameacha alama mbovu ambazo tunatamani zifutwe kabisa.

Mapambano ya kweli dhidi ya ufisadi ndio yameanza na kwa hakika yatagusa hata wasioguswa, yatashika wasiowahi kushikwa na yatarudisha heshima ya Mtanzania popote pale alipo. Mabadiliko haya ni lazima yapate upinzani kwani ndivyo ilivyo asili ya mabadiliko yoyote yale ambayo yanalengo la kubadilisha kwa haraka na kwa kiasi kikubwa maisha ya watu. Ni lazima kuwepo kwa upingamizi (resistance) dhidi ya mabadiliko. Lakini mabadiliko ni lazima!

Wenye mawazo ya kutaka kuongoza nchi tofauti na Magufuli; na wale ambao wanataka kuona nchi iendeshwe tofauti na hivi wana muda wa kujipanga; miaka mitano si mingi. Waje na mapendekezo yao 2020 na wapiga kura wakiwakubalia watawachagua; sasa hivi hizi ni zama za Magufuli. Anaiweza shughuli.

Raia Mwema
 
Lazima serikali iwe na nguvu kwa kifedha, ulinzi, usalama na uadlifu kwa kila sekta. Naunga mkono hoja tena akaze buti heshima iwepo na hata kimataifa tuwe na uwezo mkubwa wa kujikimu wenyewe.

Naamini kwa mwendo huu itafikia kuwa na uwezo wa kujitegemea wenyewe bila kukopa au kuomba kwa matajiri.

Tubadlike maana hii ni ndio nchi yetu kwa maslahi yetu wote
 


Kuna mambo kadhaa Magufuri anafanya yasiyo fuata haki za binadamu.. Watu hawataacha kumkosoa
 
yeye ndo raisi ataamua kama anataka kuongoza nchi ki nguvu au kufanya wanavotaka wananchi ila mwisho wa siku kila mtu atakua na maoni yake...na kama raisi anashindwa kufanya kazi kisa kuna watu wana maoni tofauti na yake basi huyo sio raisi mzuri.
 
Hii sio nyumba ya baba na mama na watoto.....nchi ni yetu sote watanzania.....asitufanye kuwa wakimbikizi nchini mwetu!
kwa kifupi aache ubabe afuate katiba iliompa madaraka vinginevyo The Hague inamsubiri!
 

hakuna jipya hapo ni usanii!!!!! tupu na takwimu za kutengeneza,,,,,mwisho wa siku wewe unaehesabiwa msukule na chama cha majipu(ccm) utatueleza nini effect umepata ktk kuishi kwako??????kuna agenda ya kubinya na kupora mshindi zabar na agenda za kupitisha miswaada ya kiccm kupora raslimali za nchi ndio maana magazeti na television vinazimwa kwa nguvu ya dola na utapewa habari iliyokuwa edited(imechujwa)=feki
 
Siku zote kila mmoja anapotoa maamuzi kutaka kuinua Uchumi hata kama ni wa familia lazima kuna watakao umia kwa kuwa wanayotaka yafanyike wao hawataki au ni wavivu. Watakaofurahia mabadiliko Wataunga mkono. Kwa hiyo ni lazima yanayojiri kwa sasa yaonekane kwa kuwa kila mmoja anaupeo tofauti wa kufikiri.
 
Magufuli atafanya kazi, hao watakaojaribu kumkwamisha wanajisumbua. Ametumia akili sana kuanza na TAKUKURU pamoja na DPP, katengeneza msingi wa kazi kubwa anayotegemea kuifanya. Hao ambao wamezoea kupata umaarufu wa bei rahisi, wakitegea mambo yatokee halafu waitishe press conference waweze kutazamwa saa mbili usiku wakati wa taarifa ya habari ya siku nzima, watakuja kuonekana hakuna cha maana wanachokifanya mpaka wakapewa airtime. Magufuli kaanza vizuri.
 
mtoa mada umecopy na kupaste hilo ndo ttz lako nchi aindeshwi km familia isipoukuwa kwa misingi maalum tuliojiwekea kikatiba sio ukiona mtu humpend unamfukuza mara mwingine unampakaz nyingine au we umejaaa mapenz mpaka uoni wala usikii kuwa wale unaowaita mafisad bado wanakula nchi huku tukiaminshwa mchawi mpe mwanao na kwa kuongezea sera mbovu za nchi zikipeperushwa na viongozi uchwara kwa madai na wachapa kazi jmn tuwe wakweli hatukumchagua rais awe tishio kwetu sasa my take borq ifutwe katiba tunayojiaminsha ni nchi yenye utawala bora huku hakuna kitu km hicho napenda rais atumie hekima km elimu tyr nayo la sivyo nchi itakuwa ya ulalamishi daima kwan **** makundi yanawatafna wengine
 
Mabadiliko ya kweli yataanzia katika fikra za watanzania.

kubadilika fikra ni kwa watanzania kujua kile wanachokitaka katika akili zao na sio kudai mabadiliko alafu hawajui wanachokitaka na yule anayekuja anafanya anavyotaka eti wamuache.

raisi ana vision nzuri lakini kinachotendeka kinaweza kisitimize azma ya watanzania. kwa mantiki hiyo mimi napingana na wewe kwa kusema "tumuache raisi afanye anavyotaka" kana kwamba anachokifanya ni business ya familia yake.

kitaaluma mtu yeyote anayeona kitu kinatendeka na yeye akawa anaamini kinachofanyika ni makosa na yeye ana njia sahihi na akaa kimya kusubiri mpaka mambo yamekwisha haribika alafu ndio anasema mimi nilijua hafai na hawezi kupewa nafasi.

mimi naamini katika walioko madarakani kufanya kila linalowezekana ili taifa lisonge mbele. kuwakosoa ni kuwapa nafasi nzuri zaidi ya kutumia busara zao na kuamua njia ipi sahihi na yule anayekosoa anajiweka katika nafasi ya jamii kuangalia hata kama hana nafasi ya kutekeleza lakini je anaweza kuleta hoja za kusaidia jamii?

kama mtu akileta hoja ya kutetea wezi kuna tatizo gani kwako wewe maana jamii ndiyo itamhukumu kwa kuangalia siku akijitokeza kugombea. kama jamii ni ya wezi basi watajua wana mtetezi na kama jamii ni ya watu wa haki basi watajua huyu hatufai.

kila analolifanya raisi nadhani jamii ingefungua mjadala na kujadili ili kuwajua hata wale wasiotekeleza wanawaza nini na kama wana mitizamo mibovu ni jamii yenyewe itaamua na hiyo itakuwa njia sahihi ya kuwalinganisha watu uchaguzi mwingine ukifika.

sasa ndugu yangu nakushagaa kuchanganya kila anachokifanya raisi kuwa katika kapu moja kuwa anayepinga moja kapinga yote na anayesapoti moja kasapoti yote.

labda nikuulize fikiria wewe umejenga nyumba yako ina vyumba kumi vya kulala. familia yako ikahamia katika nyumba hiyo bila kupewa mwongozo wa kila mtoto chumba chake ni kipi na kila mmoja akalazimika kuchagua chumba chochote na kuingia. Mara ukarudi nyumba ukakuta vipi vyumba ulipanda viwe stoo lakini kuna watoto wanalala, ukakuta kuna vyumba ulipanga viwe makitaba lakini kuna watoto wanalala.

je utajitambua kuwa watoto kuingia katika vyumba ambavyo ulivipangia shughuli nyingine ni kutokana na wewe baba kutokuwaelekeza ukakaa kimya au utawaona watoto hawa wana makosa makubwa?

je utafanya nini? utaanza kuwaeleza kila mtoto chumba chake ni kipi na kuwataka wahame au utaanza kukagua na kumuadhibu kila unayemkuta katika chumba kisicho chake?

swala la bomoabomoa usiliangalie kwa kusema hawa wamejenga maeneo wasiyostahili kujenga bila kujiuliza walitakiwa kujenga wapi na nani alitakiwa kuwaonyesha mahali sahihi pa kujenga na je huyo alifanya hivyo na kama hakufanya wakajenga ovyo je kosa ni la nani?

je huyu anayebomoa leo anawaonyesha watu hawa wanaojenga leo mahali sahihi pa kujenga au bado hatimizi wajibu wake. mvua zikinyesha watu wa mabondeni wakumbwa na mafuriko anasema ni marufuku kujenga mabondeni na milimani mawe yakiporomoka yakaua watu anasema ni marufuku kujenga milimani.

kwa nini huyu asichukue jukumu lake la msingi la kuanza kubainisha ni wapi watu wakae, ni wapi biashara Fulani zikae, ni wapi kila kitu kikae na hilo ndilo suluhisho la kudumu na sio kuwabebesha mzigo wahanga wa serikali zetu kutokutimiza wajibu wao.


 
Kuna mtu anaweza kuridhisha mamilioni ya watu kwa wakati mmoja? Lazima ikubalike kwamba Rais atasifiwa na atakosolewa sana na wanaomjua na wasiomjua. Uongozi ndivyo ulivyo. Ukiwa kiongozi rafiki wa watu ujue kazi imekushinda. Tunachotaka wengi ni utawala wa haki.

Kukaa kimya wakati mtu anavurunda ni jadi yetu na anayejaribu kusema huitwa mpinzani. Tabia yetu hii ndio iliyotufikisha hapa tulipo. We are paying for the sins of others.
 
Yeye afanye tu kazi zake, la msingi ajue kuwa sisi ndio waajiri wake, awe na muda wa kutusikiliza na kujua tunataka nini na aheshimu maamuzi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…