Kwanini tunang'ang'ania matumizi yasiyo sahihi ya neno "Pelekea"?

Oct 4, 2023
6
14
Pelekea na Sababisha

Pelekea ni mnyambuliko wa neno peleka ambalo maana yake ni kumchukua mtu au kitu na kukifikisha mahali panapotakiwa. Kwa kuzigatia maana ya peleka na mnyambuliko huo wa kutendea wa peleka, maana ya pelekea ni kufanya tendo la kupeleka kwa ajili ya mtu fulani au kwa niaba ya mtu fulani. Mifano ya matumizi ya neno Pelekea ni, ‘Juma alimpelekea Asha kitabu chake’ au ‘Nilimpelekea mwandishi makala yake katika Jukwaa la Jamii Forumn’. Pelekea haina maana ya sababisha. Wanaotumia Pelekea kama kisawe cha sababisha wanafanya tafsiri sisisi ya Kiingereza ‘leads to’. Huu ni upotoshaji wa matumizi sanifu na fasaha ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Neno sahihi linalofaa kutumika katika mazingira kama hayo no Sababisha na siyo pelekea.

Sababisha ni kitenzi chenye maana ya fanya jambo fulani liwe au litokee. Maneno mengine yenye maana inayokaribiana na sababisha ni anzisha, ibua, fufua, leta na asisi. Mifano ya matumizi ya neno hili inaweza kuwa, ‘Mvua iliyonyesha jana ilisababisha nyumba na barabara nyingi kujaa maji’ au ‘Ugonjwa wa malaria husababisha vifo vingi katika jamii yetu’. Hivyo, watumiaji wa lugha ya Kiswahili wanapaswa kuzingatia maana hizi na kuelewa kwamba maneno haya, pelekea na sababisha maana zake si sawa na hivyo hayapaswi kutumiwa kwa kubadilishana nafasi kama ambavyo baadhi yetu wanafanya.

Zacharia Emanuel ( Swahili Linguist and translator)
WhatsApp +255755350165.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2023-10-09 at 09.50.04.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-09 at 09.50.04.jpeg
    63.9 KB · Views: 6
Pelekea haina maana ya sababisha. Wanaotumia Pelekea kama kisawe cha sababisha wanafanya tafsiri sisisi ya Kiingereza ‘leads to’. Huu ni upotoshaji wa matumizi sanifu na fasaha ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Neno sahihi linalofaa kutumika katika mazingira kama hayo no Sababisha na siyo pelekea.

Taarifa hii iwafikie wanahabari, maana kwa kiasi kikubwa wamekuwa wapotoshaji wa matumizi sahihi ya maneno ya Kiswahili...
 
Pelekea ni mnyambuliko wa neno peleka ambalo maana yake ni kumchukua mtu au kitu na kukifikisha mahali panapotakiwa. Kwa kuzigatia maana ya peleka na mnyambuliko huo wa kutendea wa peleka, maana ya pelekea ni kufanya tendo la kupeleka kwa ajili ya mtu fulani au kwa niaba ya mtu fulani. Mifano ya matumizi ya neno Pelekea ni, ‘Juma alimpelekea Asha kitabu chake’ au ‘Nilimpelekea mwandishi makala yake katika Jukwaa la Jamii Forumn’. Pelekea haina maana ya sababisha. Wanaotumia Pelekea kama kisawe cha sababisha wanafanya tafsiri sisisi ya Kiingereza ‘leads to’. Huu ni upotoshaji wa matumizi sanifu na fasaha ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Neno sahihi linalofaa kutumika katika mazingira kama hayo no Sababisha na siyo pelekea.

Sababisha ni kitenzi chenye maana ya fanya jambo fulani liwe au litokee. Maneno mengine yenye maana inayokaribiana na sababisha ni anzisha, ibua, fufua, leta na asisi. Mifano ya matumizi ya neno hili inaweza kuwa, ‘Mvua iliyonyesha jana ilisababisha nyumba na barabara nyingi kujaa maji’ au ‘Ugonjwa wa malaria husababisha vifo vingi katika jamii yetu’. Hivyo, watumiaji wa lugha ya Kiswahili wanapaswa kuzingatia maana hizi na kuelewa kwamba maneno haya, pelekea na sababisha maana zake si sawa na hivyo hayapaswi kutumiwa kwa kubadilishana nafasi kama ambavyo baadhi yetu wanafanya.

Zacharia Emanuel ( Swahili Linguist and translator)
WhatsApp +255755350165.
Ok ni vizur mkiwa mnatuoa shule namna hio tuna jifunza humo humo na kuelewa
 
Back
Top Bottom