Kwanini taifa halijifunzi tu kwa mauaji ya kisiasa?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
17,005
20,421
Kwanini taifa halijifunzi tu kwa kila maandiko na ushauri tunaoutoa wadau? Miaka 7 nyuma niliandika kisa muhimu kutoka Buenos Aires nchini Argentina, Niliandika nikionya serikali ya Hayati Magufuli kufuatia jaribio la Mauaji ya Mh Tundu Lissu ambalo hadi leo hakuna uchunguzi wa aina yoyote uliofanywa kujua waliohusika.

Sehemu ya andiko lile nilieleza kirefu kwamba, Tarehe 18 Januari 2015 Idara ya usalama ya Agentina ilituhumiwa kuhusika na mauaji ya mpelelezi binafsi bwana Alberto Nisman aliyekuwa akitaka kuanika madudu ya serikali hiyo ikiwemo ufisadi uliopelekea kulinda ugaidi wa Iran uliofanyika Agentina. Wairani walikuwa wamewahonga usalama wa taifa wa Agentina kwa vipande vya fedha ili wasiiumbue Iran katika ugaidi huo uliotekelezwa katika kituo cha Israel kitwacho AMIA Jewish Community Centre" kilichomo mjini Buenos Aires Agentina.

Alberto Nisman akafanya uchunguzi, akagundua ukweli huo bila kuacha chenga ambapo sehemu ya ripoti hiyo ilimuhusisha rais wa zamani Cristina Fernández de Kirchner na ugaidi huo wa mwaka 1994, na kukazia kuwa rais aliitumia idara hiyo kuendesha mauaji ya raia wakosoaji, wapinzani, wanaharakati na wanahabari nchini humo. Ilipofika Mwaka 2015 aliyekuwa Rais wa Agentina kwa wakati huo, Bwana Mauricio Macri yeye akataka kuifutilia mbali kurugenzi ya ndani ya usalama ya Agentina kufuatia kashfa hiyo ambayo ilikaribia kuhatarisha mamlaka yake ya urais na nchi kwa ujumla. Jamaa wa Usalama kuona hivyo, wakamuua mpelelezi bwana Alberto Nisman siku moja kabla hajawasilisha ushahidi wake bungeni ili aanike ukweli.

Bunge la Agentina baada ya kuona hali hiyo, likamualika Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Agentina ili awaeleze utendaji wa taasisi hiyo. Ilikuwa afanye kazi hiyo siku ya Jumatatu April ya 2015. Katika hali ya ajabu sana, Mkurugenzi huyo wa Idara ya Usalama ya Argentina akatekwa, haikujulikani alipo hadi ilipokuja kugundulika mwili wake ikidhaniwa alikufa kwa msongo. Sheria ya Usalama wa Taifa Argentina ilikuwa inafanana sana na sheria mpya ya Usalama wa Taifa Tanzania iliyopitishwa August 2023, sheria ya Argentina iliweka Kinga na katazo kuu kwa shughuli za idara kuhojiwa popote, wala maafisa wake kushitakiwa kwa ukiukaji wowote watakaoutenda, Yaani chombo hicho kilikuwa kiko juu ya sheria zote za Argentina.

Sasa baada bunge kuona hivyo, likaamua kuvunja Shirika la Ujasusi la Agentina kwa sababu shirikali hilo lilikuwa limegeuka kuwa chombo cha uhalifu na genge lililokuwa linahatarisha kumpidua Rais, pia lilikuwa linaendesha vitendo vya kidharimu kwa wapinzani na wanaharakati kwakutumika na wanasiasa na usaliti kwa taifa. Bunge hilo lilivunja shirika hilo la Ujasusi na kisha kuliunda upya likiwa na sheria mpya, watu wapya wenye weledi kabisa na mfumo mpya wa uendeshaji

Hali ya Agentina kipindi hicho haikuwa na tofauti sana na ya Tanzania sasa. Usalama wa Raia umekuwa jambo tete sana kama ilivyokuwa Agentina ya zamani ambako maafisa usalama waliwawekea vinasa sauti wanasiasa, kuwahujumu, kuwateka, kuwapiga na kuua wanaharakati, wanasiasa, na wanahabari. Uhuru wa kutoa maoni Argentina ulizimwa kabisa.

Binafsi nilionya baadhi ya vifungu vya marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa 2023, niliviona vifungu hivyo ni hatari kwa mstakabali wa taifa la kidemokrasia lenye uhuru wa vyama vingi, Sheria ile ni hataei kwa mamlaka ya Urais, Sheria ile haiwezi kufanya kazi kwa mataifa yetu ya kiafrika hasa kwenye nchi masikini hizi ambazo madaraka ya kisiasa yanalindwa kwa jasho na damu.

Fundisho kubwa kwa Tanzania ni wakati sasa wa kufanya marekebisho upya ya sheria ya Usalama wa Taifa licha ya kupitishwa mwaka jana tu, Yafanyike marekebisho makubwa ya mfumo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini hasa idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha uhai wa kila Mtanzania na kila mtu unalindwa na kuthaminiwa sawa na matakwa ya katiba ya Tanzania na katiba ya Ulimwengu.

Na Yericko Nyerere
IMG_3933.jpeg

IMG_3934.jpeg
 
Hili bunge letu la Spika Tulia haliwezi kuwa na uthubutu wa kufuta sheria mbovu za TISS.

Bahati mbaya zaidi, hata haya mauaji na utekaji unaoendelea sasa nchini kama ikitokea serikali ikabanwa bungeni, basi usishangae wabunge wa CCM wakawa upande wa serikali yao.

Hapa kilichobaki ni kwetu watanganyika tuamue sasa, huu utekaji ufike mwisho, mambo wanayotufanyia tunageuzwa kama wakimbizi ndani ya nchi yetu huku tukiwaangalia tu, huu ni ujinga mkubwa sana.

Bado najiuliza, kwanini haya mambo ya kijinga hayapo Zanzibar ikiwa kote kunaongozwa na serikali za CCM?

Jibu, tatizo letu watanganyika ni huyu kiongozi wetu, anachezea uhai wetu kwa makusudi.
 
Fundisho kubwa kwa Tanzania ni wakati sasa wa kufanya marekebisho upya ya sheria ya Usalama wa Taifa licha ya kupitishwa mwaka jana tu, Yafanyike marekebisho makubwa ya mfumo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini hasa idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha uhai wa kila Mtanzania na kila mtu unalindwa na kuthaminiwa sawa na matakwa ya katiba ya Tanzania na katiba ya Ulimwengu.

Na Yericko Nyerere
Naunga mkono hoja!.
P
 
Kisiwa cha amani chageuka kisiwa cha taharuki na ghasia za mauaji kama enzi za utawala wa Makaburu kule SA.
 
Ni kosa kubwa sana. Yaani ukiishi kwa upanga basi jiandae kisaikolojia koundoka kwa upanga.

The moment ukianza kuua wenzako, unakuwa umewasha green light kuwa nao wakipata nafasi basi wakuuwe.
 
Back
Top Bottom