Kwanini social media accounts za kampuni/biashara yako aziwafikii watu kama ulivyotarajia?

Big dady 11

Member
May 21, 2023
54
59
Skuizi imekuwa kama fashion tu kuona wafanya biashara wadogo kwa wakubwa, makampuni Hadi taasisi mbalimbali kuwa na account za mitandao ya kijamii(Facebook, Instagram na YouTube)..

Na wengi wao wakiwa motivated kuwa na iyo mitandao ya kijamii kwa ajili ya biashara zao kwa kuiga au kwa kuskia tu kwenye semina za motivation za online marketing 🤷..

Ukwel ni kwamba kwa asilimia 90 za hizi motivation semina za online marketing huwa haziwezi kufanya kazi Tanzania..
Je ni kwasabab gan??


Sababu zipo nyingi sana ila Kuna hii ya unakuta huyo anaekupa elimu ya online marketing elimu yake kaipatia YouTube, topic zake anazitoa hukohuko YouTube anachofanya yeye ni kutranslate kutoka kingereza kuja kiswahili..

Na kuja kuwalisha wafanya biashara na waendesha kampuni matango pori kwny semina zao zenye title kubwaaaaa FANYA BIASHARA KIDIJITALI 😁.

video za YouTube mzungu huelezea online marketing na branding kutokana na matumizi yao wao kwenye hiyo mitandao ni tofauti na hapa bongo..

Mfano bongo insta ni mtandao wa mastaa .. X ni mtandao wa wanasiasa na wasomi.. Facebook ni mtandao wa watu wa hali ya chini ..mabeki 3, mama na watoto kwa hapa Tanzania ndivyo tunavyo tafsiri hii mitandao na huu mtazamo unauhalisia wake..

Sasa ukisema u apply mbinu za online marketing za marekani uje uzifanye bongo utafeli.. ukisema u apply mbinu za online marketing za Facebook kwa nchi za ulaya uzlete bongo utafeli x100😁..

Mfano una show room ya magar unauza magari unafungua page au group la kuuza magari Facebook 🤔.. unapost magari milion 50,30, 20.. utegemee kupata wateja Facebook na unalipia kabisa page yako sponsored ili iwafikie watu weng 🤔. Facebook ya bongo hakuna biashara ya mamilioni utamuuzia Nan ???

Na Mara nyingi unakuta wafanya biashara hununua hizi page za Facebook na account za insta zenye followers wengi..

Unakuta unanunua page ya Facebook ya followers 200k lakn 80% ya hao followers ni kinamama wa nyumbani na wadada .. ukifuatilia iyo page ilipataje followers 200k unakuta ilikuwa page ya simulizi za mapenz 😁😁..
Alafu ww unaibadili unakuja kufanya page ya biashara unauza magari 🤣🤣.
Au unakuta unanunua account ya Instagram unauza vifaa vya ujenzi na decorations za nyumba.. unakuta hapo kabla iyo account ilikuwa ni ya Amina utamu 🤣 ni post za makalio uno ndembe ndembe.. unakuwa asilimia 90 ya followers ni vijana wa hovyo na vitoto vya 2000..
Alaf ww unakuja kununua iyo account na unauza vifaa vya ujenzi..

Hapo hapo unachukua tu mdogo ako unampa Kaz kuwa unapga pcha bidhaa na kupost Instagram au Facebook..
unakuta Hana ujuzi wowote wa kushoot Wala kuendesha mitandao ya kijamii.
Ni kwel siku hizi Kila mtu anaweza kuwa camera man ila sio kila mtu anaweza kuwa creative.

Online marketing inahitaji creativity ya hali ya juu..
Unahitaji ujue unauza nini na mteja wako ni nani na Kwenye mitandao ni mtandao gani utakuwa na wateja wengi wenye uhitaji wa bidhaa yako..

Ukisha jua Hilo unahitaji upate camera man mzur (videographer au photographer) na graphics designer
Ili uwe unapata video na picha nzur pamoja na posters za matangazo ya kuvutia wateja wako..

Pia kwakumalizia..
Hapa watu wengi huchanganya sana na kutokuweza kutofautisha kati ya camera man na graphics designer..
Hawa ni watu wawili tofauti na ni taaluma mbili tofauti..

Sio kila camera man anaweza kuwa graphics designer na sio kila graphics designer anaweza kuwa camera man..
Ila pia wapo wanaoweza vyote viwili.

Wakuu toeni maoni yenu na nyie mmeona Nini kwenye hili la account na page za biashara.
 
Kuna mfanyabiashara ana page insta anasema anafundisha kutengeneza ice cream, smoothie, juice nk....nikasema ngoja nilipie nione yaliyomo nijifunze vitu vizuri.

Nmelipa nikawekwa katika group kifuatacho kapakua zake vids za you tube wala hazina maelezo ni vimziki tu kwa background unaona mtu anakata maembe anamix nkabaki 🤦🤦🤦 sa si ningeingia you tube mwenyewe.
 
Kuna mfanyabiashara ana page insta anasema anafundisha kutengeneza ice cream, smoothie, juice nk....nikasema ngoja nilipie nione yaliyomo nijifunze vitu vizuri.

Nmelipa nikawekwa katika group kifuatacho kapakua zake vids za you tube wala hazina maelezo ni vimziki tu kwa background unaona mtu anakata maembe anamix nkabaki 🤦🤦🤦 sa si ningeingia you tube mwenyewe.
🤣🤣 Ndo wanavyofanya. Yan awanamda wa kuumiza kichwa kuandaa contents zao ztakazoendana na ihalisia wa mtanzania
 
Back
Top Bottom