Habarini,
Hivi ni kwa nini single mother walio wengi wana mafanikio kuliko wanawake waliopo kwenye ndoa? Maana naona wengi wao kiuchumi wapo vizuri kuna wengine nimewashuhudia walitelekezwa na watoto wakaanza na vibiashara vidogovdogo tu ila walipoanza tu mambo yamewanyookea moja kwa moja.
Mwanzo unakuta amepauka haeleweki ila ukija kumuona baada ya miaka miwili unakuta yupo vizuri kiuchumi mtoto anasomesha shule nzuri anavaa vizuri tofauti na walio kwenye ndoa ambao wengi wao unakuta mambo yao ni tofauti.