Munamuge
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 798
- 759
Wakuu, habari za jioni.
Kwanza kabisa napenda kutamka wazi kwamba mimi ni Mtanzania ninaetamani tuwe na Muundo pendekezwa wa serikali tatu.
Nikirudi kwenye mada yangu, nimeshangazwa sana na kitendo cha serikali kuamua kutugawa katika matabaka kwa kutaka tutambulike Utanzania wetu ni wa Bara ama Visiwani, hali niliyoiona katika tovuti ya Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma (PSRS).
Kipengele hiki ninaamini ni kipya kwa sababu sikuwahi kukutana nacho kabla (miaka ya 2018 na 2019 nilipokua nikitembelea tovuti hiyo).
Ninashangazwa kwasababu serikali inayoongozwa na CCM imekua mstari wa mbele kupinga kuanzishwa kwa serikali tatu na kusimamia hoja yao ya serikali ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inawezaje kuutambua uraia wa Tanzania bara pasipokuwepo na nchi ya Tanzania bara wala serikali yake.
Ninafahamu Wazanzibari wana vitambulisho vinavyowaonesha Uzanzibari wao (Mtanzania wa Tanzania visiwani), sasa najiuliza kwa sisi wa Tanzania bara tutatambulishwa na nini?
Nimeweka hapa chini picha ya taarifa niliyoombwa kujaza kwenye tovuti hiyo kuhusu uraia.