Kwanini serikali hii inazidi kututia katika lindi la umasikini badala ya kutusaidia!?

Bornventure

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
529
523



http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/312e13567a8e79e7565b0948959c70a0.jpg[/IMG

Nimeambatisha copy ya form ukiangalia heading yake inajieleza wazi.

Mimi ni mmojawapo wa wahanga wa kuchukuliwa kwa ardhi yangu kutokana na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Matema (Kyela , ziwa Nyasa) to Kyela njia panda ya Ipinda.

Tumefanyiwa tathmini nyiingi sana na tukajazishwa form za mkataba wa fidia ya mali zetu ikiwemo miti ya kokoa ambayo ndiyo nguzo ya uchumi huku kwetu, nyumba na ardhi.

Baadaye viongozi wa mkoa, wakaja na kutusihi turuhusu ujenzi uanze bila fidia ili tusicheleweshe mradi halafu malipo yatafuata . Tukakubali.

Cha kushangaza majuzi amekuja Mkuu wa Wilaya na kututangazia kwamba hakuna malipo. Mara Sijui wengine walifata barabara na wengine iliwafuata.

Kwa Kweli nimekosa imani saana na serikali hii. Tafadhali msaada jamani tusaidieni wana Kyela kutupazia sauti tunataka kudhulumwa. Tumerudishwa nyuma sana kimaendeleo halafu tudhulumiwe!!?

Nina mengi Ila kifupi ni haya.
 
Umasikini Unajitengenezea mwenyewe
Najitiaje umasikini hapo ndugu? Nilikua na kakao, migomba, michikichi, miparachichi na miembe mingi sana. Imekatwa yote. Eneo langu limechukuliwa mita 29 upana na mita 111 urefu. Siwezi tena kufanya kilimo, mie Sio mwajiriwa unasemaje najitia umasikini?? Nyumba pia inatakiwa ibomolewe
 
Kosa lilikuwa kuruhusu ujenzi kabla hamjalipwa......... mngeungana pamoja mngelipwa
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…