Kwanini Prince Dube anachezeshwa dakika 90 kila mchezo?

holoholo

JF-Expert Member
May 10, 2023
1,542
2,449
Prince Dube ni straiker bora sikatai, ubora wake huo ndio uliwavutia mabosi wa YOUNG AFRICANS SC kumleta Jangwani, kongole kwa Eng. Hersi Saidi na mfadhiri GSM.

Wanayanga walikuwa tuna matumaini makubwa na straiker huyu kuwa ndiye atakuwa mshambuliaji kinara na kiongozi klabuni hapo

lakini mambo ni tofauti, Prince amekuwa goigoi, dhaifu na mtu wa hovyo sana hasa anapokuwa na mpira kwenye box la wapinzani, ni eidha ajikwatue aanguke, apige nje au apige shuti mtoto na kiukweli imekuwa ikighalimu timu kwa muda sasa.

amepewa muda vya kutosha lakini habadiliki, washambuliaji hatari hasa Jean Othos Baleke mpaka anaondoka hakuwa na nafasi mbele ya Prince goigoi, Mzize anacheza vizuri sana na anafunga ila anatolewa mapema sana kuliko Dube.

Je kuna siri gani kwa Prince Dube kuchezeshwa dk 90 kila mechi wakati mchango wake ni mdogo katika timu?
 
Kwa sababu Kuna yule NABII alimtabiria kua utaanza kufunga sana Kila mechi, baadae utakua haufungi kabisaa ,ili mungu akupime Imani yako, kwahiyo hata kama hautafunga magoli usirudie nyuma, ni kipindi Cha kupima, baadae Utanza kufunga ,utafunga mpaka watu washangae


Kwahiyo, NABII huyu kwakua anamahusiano na Viongozi yanga, analazimisha Dune apangwe, ili baadae Ionekane NABII Alitabiri .
 
Prince Dube ni straiker bora sikatai,ubora wake huo ndio uliwavutia mabosi wa YOUNG AFRICANS SC kumleta Jangwani,kongole kwa Eng. Hersi Saidi na mfadhiri GSM.

Wanayanga walikuwa tuna matumaini makubwa na straiker huyu kuwa ndiye atakuwa mshambuliaji kinara na kiongozi klabuni hapo

lakini mambo ni tofauti, Prince amekuwa goigoi,dhaifu na mtu wa hovyo sana hasa anapokuwa na mpira kwenye box la wapinzani, ni eidha,ajikwatue aanguke,apige nje au apige shuti mtoto na kiukweli imekuwa ikighalimu timu kwa muda sasa.
amepewa muda vya kutosha,lakini habadiliki,washambuliaji hatari hasa Jean Othos Baleke,mpaka anaondoka hakuwa na nafasi mbele ya Prince goigoi, Mzize anacheza vizuri sana na anafunga ila anatolewa mapema sana kuliko Dube,

Je kuna siri gani kwa Prince Dube kuchezeshwa dk 90 kila mechi wakati mchango wake ni mdogo katika timu?
Mpira unatumia mwili wa binadamu wachezaji muhimu inatakiwa wapumuzishwe kwa michezo unao/inayo kuja, "fatigue" uchovu
 
Dube ni mzuri ila sio straika wa kumtegemea hili nililisema mapema na yeye ndo wa kulaumiwa Yanga kushindwa kuvuka makundi...

Dube ni mchezaji muoga sana, unakuta kapigiwa pasi nzuri sana lakini anakimbia na kupiga bila kutumia akili yaani Bora apige tu huku akitetemeka hua ananikera sana mara kumi Guede kuliko Dube yaani Yanga tungekua na straika mwenye kiwango tu cha Elvis Rupia tungempiga mwarabu siku Ile..

Dube labda abadilike vinginevyo hata msimu ujayo Yanga haitakua Bora kimataifa otherwise tutumie mfumo kama wa Gamondi kutegemea zaidi viungo ndo wafunge magoli zaidi, lakini huyu Dube ni kusubiri meli stand.

Dube ataonekana Bora kwenye game za mchangani japo hata huko akikutana na mabeki katili hatapiga hata on target Moja...
Ngoja niishie hapa kama anashinda kumfunga kipa wa Kengold kwenye 1v1 unategemea atamfunga kipa wa mamelodi??
 
ngara23 wakati mwingine uheshimu watu usio wajua. haya, turudi kwenye main topic,wewe unafkilia ni kwa nn prince dube anapangwa kila mchezo tena kwa dk zote 90?
Hayo ni maamzi ya bench la ufundi
Wao ndo wamesoma hiyo kazi
Lazima ujifunze kuheshimu taaluma za watu
Wao ndo wanakaa na wachezaji wote mazoezini
Wanaona potential ya kila mtu
Umesema wewe ni kiongozi Bado unaingilia majukumu ya wataalam uliowaamini
 
Hayo ni maamzi ya bench la ufundi
Wao ndo wamesoma hiyo kazi
Lazima ujifunze kuheshimu taaluma za watu
Wao ndo wanakaa na wachezaji wote mazoezini
Wanaona potential ya kila mtu
Umesema wewe ni kiongozi Bado unaingilia majukumu ya wataalam uliowaamini
kibwana shomari ni nani aliyepaza sauti mpaka kurudishwa kikosini?
 
kibwana shomari ni nani aliyepaza sauti mpaka kurudishwa kikosini?
Kibwana Shomari kaja kucheza baada ya kuja kocha mpya baada ya Gamondi kufukuzwa ila Gamondi aliona bora amuweke Nkane na sio Kibwana. Pamoja na kelele za mashabiki ila Gamondi kabakia na msimamo wake ule ule kwa Kibwana.
 
ngara23 wakati mwingine uheshimu watu usio wajua. haya, turudi kwenye main topic,wewe unafkilia ni kwa nn prince dube anapangwa kila mchezo tena kwa dk zote 90?
Ndio Utuambie Wewe,Ewe Mwandamizi Wa Timu Au Kwa Maoni Yako Ulihitaji Akipangwa Acheze Dakika Ngapi?Na Kwani Mchezaji Wa Mpira Wa Miguu Anatakiwa Kucheza Dakika Ngapi??Ili Astahili Kuwa/Kuitwa Mchezaji Wa Mpira Wa Miguu??
 
kibwana shomari ni nani aliyepaza sauti mpaka kurudishwa kikosini?
Heshimu taaluma za watu
Coaching ni professional sio harakati za kupaza Sauti kama unadai uhuru
Kama unajiamini unaweza peleka CV zako Yanga upewe timu, uwe unaipanga unayemtaka
 
Tukiacha ushabiki! Mtoa mada una hoja ya msingi sana. Hata mimi nimekuwa nikijiuliza, hivi kweli Prince Dube ana sifa ya kucheza dakika 90 zote za mchezo kwenye mechi za Yanga?
Kweli Prince Dube ana sifa ya kuwa mshambuliaji kiongozi, wa kumsugulisha mpaka Kenned Musonda benchi? Kila ninapojiuliza haya maswali, majibu mara zote huwa yanakuja Hapana!!

Kwa sababu gani? Jibu ni kwamba Prince Dube hana utulivu! Hana stamina! Hana uwezo wa kutumia nafasi anazopata! Hana uwezo wa kuwapangua walinzi kama alivyokuwa akifanya Fiston Mayele, na pia dogo Clement Mzize, ambaye kwa sasa eti anachezeshwa pembeni baada ya Dube kusajiliwa!!

Nina wasiwasi huenda Prince Dube anachezeshwa kutokana maelekezo kutoka juu. Ila siyo kwa sababu tu ya uwezo wake. Nina wasiwasi kama atakuja kubadilika siku za usoni. Ila kama atabadilika kwa kuwa mshambuliaji aliyekamilika (mwenye stamina, utulivu, pace, nk), basi litakuwa ni jambo la heri kwake na pia klabu.

Ila mpaka sasa tukubali tu mchezaji wetu ni tia maji tia maji.
 
Back
Top Bottom