Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,736
- 23,125
Picha na Daily News.
Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae ni mjumbe maalum wa raisi Samia, siku ya tarehe 17 April alifanya ziara ya kikazi nchini Burkina Faso.
Akiwa mjini Ougadougou mjumbe huyo aliwasilisha salamu kutoka kwa raisi wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambao ulisisitiza ushirikiano baina ya mataifa ya Afrika. Katika salamu hizo pia raisi Samia alisisitiza juu ya mashirikiano ya kijamii na kiuchumi katika kipindi hiki kigumu ambapo nchi tajiri duniani zazidi kupunguza misaada kwa bara la Afrika.
Ziara hii ya mjumbe huyo maalum wa raisi Samia bwana Jakaya Kikwete akiongozana na profesa Janabi imenifanya nitafakari sana juu ya malengo ya ziara hiyo na manufaa yake kwa Tanzania na ushirikiano wake ni Burkina Faso.
Soma Pia: Jakaya Mrisho Kikwete alivyokutana na Rais wa Burkina Faso, Captain Ibrahim Traoré
1. Je, uongozi wa raisi Samia umenza kujiandaa kutafuta nchi kadhaa barani Afrika ziwe marafiki ili kuanzisha mahusiano ya kibiashara. Lakini hapohapo sidhani kama waziri wa biashara na viwanda alikuwepo katika ujumbe ulokwenda Ougadougou.
2. Je, kwatafutwa fursa za uwekezaji kwa makampuni ya kitanzania kuwekeza katika sekta ya madini nchini humo huku Jakaya Kikwete akiwa ni mtu kati?
3. Je, ni katika kuishawishi Burkina Faso ijiunge na Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya nchi hiyo kujiondoa katika jumuiya ya ECOWAS ambayo ni ya nchi za Afrika Magharibi?
4. Je, ni kuiga mtindo wa utawala wa Ibrahim Traore ambae ni kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo ambae ameingia madarakani baada ya kumpindua aliekuwa kiongozi mwingine Paul -Henri Sandaogo Damiba?
5. Je, ni kutaka kuwekeza katika sekta ya afya hususan matibabu ya moyo na ujenzi wa hospitali mjini Ougadougou?
Na mwisho je, ziara hii ya katika kutafuta uwekezaji au mwekezaji ametaka kuongezwe uzito wa salamu za kutoka kwa raisi Samia Suluhu Hassan?