Kwanini M23 wanazidi kuwa na nguvu kuna nini nyuma yake

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
25,133
48,274
Waasi wa M23 wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao wanaungwa mkono na Rwanda wanaripotiwa kuuteka uwanja wa ndege wa kimkakati wa Kavumba karibu na Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.
Uwanja huo wa ndege upo takribani kilomita 20 kutoka mji wa Bukavu ambapo wakaazi wameileza BBC kuwa kuna hali ya taharuki.
Msemaji wa muungano wa waasi amesema kwenye chapisho kupitia X, waasi wanadhibiti uwanja wa ndege na maeneo jirani.
Hatua hiyo ya waasi inakuja licha ya wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano na kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya amani.
Maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao katika wiki za hivi karibuni kutokana na hatua hiyo ya waasi.
Akizungumza na BBC Makamu Gavana wa Kivu Kusini Jean Elakano hata hivyo ameiambia BBC kuwa mapigano makali yanaendelea lakini hakuthibitisha wala kukanusha ripoti kwamba waasi hao wameuteka uwanja wa ndege wa Kavumba karibu na mji wa Bukavu.
''Mapambano makali yanaendelea, tunavamiwa kutoka kila upande ardhini na ziwani. M23 pamoja na jeshi la Rwanda wanatushambulia. Tunaomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati.
Rwanda imekuwa ikikabiliwa na shhinikizo la kuwaondoa wanajeshi wake mashariki mwa Congo na kusitisha harakati za kuisaidia M23.
Hata hivyo Rais Paul Kagame wa Rwanda anasema kipaumbele chake ni usalama. Kagame anadai kuwa nchi yake inakabiliwa na tishio la mashambulizi kutoka kwa waasi wa Kihutu nchini Congo.
From BBC

Hawa kuna watu wanapa nguvu hawawezi kuwa na ujasiri uhu si kawaida hii
 
SADEC wanasemaje kwani?
 
Back
Top Bottom