Kwanini kuumizana na kumbakiana kesi za uhaini? Tuwe na kampeni mbili; No Reforms, No Election iongozwe na CHADEMA na No Reforms, Yes Election - CCM

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,104
4,518
Hivi kuna sababu gani kwa polisi wetu kutumika vibaya na CCM kwa kuteka, kukamata, kuumiza na kumbakia kesi ya uhaini Mh Tundu Lissu Mwenyekiti wa CHADEMA wakati tunaweza kushindana kwa hoja na hoja zinazoshinda ndizo zitoe mwelekeo wa taifa na nchi hii...

TUAMUE TU NA TUFANYE HIVI:

Tuwe na kambi mbili za kampeni zilizobeba hoja. Na kambi hizi zipeleke hoja zao kwa wananchi na kambi itakayoshinda kwa hoja, wananchi watakakuwa wameshinda na huo ndio utakuwa uelekeo wa nchi na taifa hili...?

1. Kambi ya "NO REFORMS, NO ELECTION" inayoongozwa na CHADEMA ibebe hoja zake, izipeleke kwa wananchi na kisha wananchi tupime uhalisia wa hoja zao kisha tufanye maamuzi..

2. Kambi ya "NO REFORMS, YES ELECTION" iongozwe na CCM na ibebe hoja zake, izipeleke kwa wananchi, tuzipime ukweli na uhalisia wake na sisi wananchi tuamue...

##Kwanini tupigane? Kwanini tuuane na kuumizana? Kwanini CCM na serikali yake wanajipa uhalali kwa kulazimisha kukubalika kwa hoja zao kwa kutumia polisi, TISS na Jeshi la Wananchi kwa kukamata wenye hoja tofauti na zao na kuwambakia kesi za uongo za uhaini..?

##Je, hatuwezi kutumia njia salama na za kiungwana kumaliza mkwamo na mzozo huu wa kisiasa..?

##NO REFORMS NO ELECTION
##FreeTunduLissu now
 
CCM kushindana kwa hoja walishashindwa zamani sana. Ufisadi na uwizi ulishaondoa uwezo wao wa kufikiri.

Kama chama kinaweza kugawa rasilimali zote kwa wageni unadhani wanaweza kuwa na hoja gani?

Dola ndio silaha pekee waliobaki nayo ndio maana kama Taifa tunataka
Reforms bila ya hIzo basi uchaguzi haupo
 
CCM kushindana kwa hoja walishashindwa zamani sana. Ufisadi na uwizi ulishaondoa uwezo wao wa kufikiri.

Kama chama kinaweza kugawa rasilimali zote kwa wageni unadhani wanaweza kuwa na hoja gani?

Dola ndio silaha pekee waliobaki nayo ndio maana kama Taifa tunataka
Reforms bila ya hIzo basi uchaguzi haupo
Huu ndio ugonjwa wao..

Na watakuja mbwa na chawa wao na kusema "CHADEMA na Tundu Lissu" ni vichaa. Hatuwezi kusikiliza vichaa.

Hizi ndizo hoja zao. They never see and face reality...

Walishaoza na kunuka kwenye akili zao...

They are walking in the destructive road..
 
Sasa kama hujui kama siasa Ndio inaweza kuamua KILA jambo!! Ni kweli tusichoshane!.
Kwahiyo akiri yako, siasa ndo kila kitu siyo? Unahitaji kutafakari tena, ni sawa naweza nikawa mpuuzi kwako, ila kila mtu na njia zake. Tusichoshane mkuu
 
Sasa kama hujui kama siasa Ndio inaweza kuamua KILA jambo!! Ni kweli tusichoshane!.
Mkuu najua siasa ndo kila kitu, sikatai. Ila kwa baadhi yetu na kwa ulimwengu wa sasa si kila kitu. Najua ni ngumu kunielewa mkuu ikiwa unaamini hivo, naheshimu sana unachoamini mkuu.
 
CCM ishapotezaga uthamani yao kwa wanachi, hawawezi kufanya chichote kile kinapasua anga - zaidi wanachoweza ni ukibaka wa kura.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom