Kwanini kipindi cha Orijinal Komedi hakionyeshwi kwenye luninga siku hizi? Joti asema haya

HOMBOY

JF-Expert Member
May 16, 2016
1,431
924

Kwako mfwatiliaji wa mabingwa wa kuchekesha wanaoishikilia rekodi ya wachekeshaji waliotazamwa sana kwenye TV nchini Tanzania kuanzia time hiyo ya Ze Comedy mpaka Orijino Komedi walivyokuwa wanawafanya watu wawahi TV zao kila Alhamisi jioni.

Ni kitambo kidogo hatujawaona Orijino Komedi kwenye TV (TBC 1) na inawezekana maswali tuliyonayo ni mengi lakini hakuna hofu tena maana tumempata Joti na amekubali kuongelea kwa ufupi.

‘Kama kundi tuna taratibu zetu na ndio maana tumejaribu kutumia muda wa mwaka mmoja kupumzika maana toka tuanze kufanya kazi hatujawahi kupumzika, tulivyopumzika pia sio kukaa kimya tukaangalia project za kila mtu binafsi na ndio maana unaona kila mtu na shughuli zake‘ – Joti

‘Ukimfatilia Mpoki kuna shughuli zake anafanya na inajulikana, Masanja pia vivyo hivyo… na mimi nimefungua Youtube channel yangu ya Joti TV, nafikiri mwaka huu tunaweza kurudi kazini pia.

Je mazungumzo ya huyu bwana mdogo yana ukweli? au baada ya huu utawala wa kiimla walipigwa stop,mpaka watakapopangiwa vyakuigiza. karibuni kwa mjadala
 
Haya mambo mkwere alikuwa anayapenda,tuburudaniburudani hivi tustarehe sasa ameondoka na twenyewe tumesepa,kwa nini wasiwe wawazi tuu kua ngosha ni full hiphop,mgumu hahahah
Hahahahaaaa, niko kwenye daladala naelekea home, ila kwa koment hii uvumilivu umenishinda imebidi nicheke tu, mengi zaid nawaachia wataalam waendelee kutililika.
 
Waliwatowa kwa Mengi iliwapige lakini nia kuwamaliza ndio wamekwisha
Cc Diamond
 
Hata na hizi comedi comedi zilizobaki sasaivi ambazo bado zinaonyeshwa kwenye matv nazo watu hawana muda nazo, ukibaatika kumkuta MTU anaangalia ataishia tu kuguna na kuondoka, unamkuta mchekeshaji anatumia nguvu nyingi kuchekesha lakini waapyi!! Labda mizengwe ndio bado watu hajaichoka,
 
Bora kujiangalizia zako Churchill Show kuliko huu uchafu wa kina Joti
 
EastAfrica tv walikuwa na uhuru wa kuigiza mambo mengi sana....

Lakini kwa TBC ni ngumu kuigiza unachoona wewe kinafaa...


EastAfrica Tv kila kitu kwao ni burudani... TBC kila kitu kwao ni dhambi...
 
Hiyo ndio ishatoka kama hawakupata enzi za ujana wao basi wajiandae na wao kuitwa waliofulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…