Kwanini Kamati ya Ulinzi na Usalama inakutana na CCM pekee na si vyama vingine?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,768
56,188
Salaam

Wakuu wa Mikoa na Wilaya ndio Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama.

Ila kila siku naona wanahudhuria Vikao na Mikutano ya Kisiasa ya Chama cha Mapinduzi lakini si vyama vya Upinzani.

Kwanini vyama vya Upinzani havishirikishwi kwenye vikao vya Ulinzi na Usalama wa Nchini?

Je, ushirikiano na Ummoja katika Nchi unahusu vitu gani?
Je, ndo maadui wa Tanzania?
Je, hawaaminiki?
Je, hawana jukumu la kulinda Usalama?
Je, ni taratibu gani zilizopo kwaajili ya vyama vya Upinzani za kufikisha taarifa inayotetelesha usalama kwahiyo kamati wakati hawashirikishwi?

Je, vyama vya upinzani vina mchango gani wa kuhamasisha wafuasi wao walinde Nchi dhidi ya Wavamizi?
 
Back
Top Bottom