Kwanini inakubaliana na hiki wanachofanyiwa wapinzani

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,605
Upinzani bora unapatikana baada ya kupitishwa katika Moto. Dhahabu safi hupatikana baada ya kupitishwa katikati ya moto mkali sana. Lengo la Moto sio kuiunguza Dhahabu bali ni kuunguza Uchafu ambao bila moto kamwe hautatoka na kuiacha dhahabu iliyo safi.

Wakati mwingine ninaweza nisieleweke, naibu spika anaonekana kama Moto wa kuwasafisha wanasiasa wa upinzani huku wa chama tawala wakibaki unrefined.

Ninaouna Uchafu wa Matusi, Ishara Ovu zisizo na nidhamu, Uchafu wa jazba, Taarifa za Uongo, Ugomvi, Uchafu wa Hofu, Uchafu wa kutokujua sheria, Uchafu wa Kuongea bila kujizuia, Uchafu wa kutokujitambua, uchafu wa kauli zisizochakatwa. wakati hili linaendelea Upande wa pili wako vile vile.

Wachina wanausemi WEI ZEI yaani katika kila DHAHAMA Kuna Fursa. Hiki mnachokiona ni Fursa kwenu, acheni kulalamika onyesheni mna kitu gani bora zaidi ya hiki tunachokiona.
 
Tanzania hatuna upinzani ,tuna waganga njaa tu.

Vyama Vya upinzani vimejaa udikteta wa kutisha kiasi kwamba ukimkosoa mfalme Mbowe unaitwa msaliti na kufukuzwa kwenye chama.
 
Tanzania hatuna upinzani ,tuna waganga njaa tu.

Vyama Vya upinzani vimejaa udikteta wa kutisha kiasi kwamba ukimkosoa mfalme Mbowe unaitwa msaliti na kufukuzwa kwenye chama.
Kuzuia kukosoa (constructively) ni kuzuia ukuaji katika vizio vipana. Udicteta unaleta Hofu, Hofu inapunguza uwezo wa kufikiri, na hupelekea maamuzi fyongo na ya kujipendekeza yasiyo ya kiweledi wala kitaaluma. Kama tabia hii ipo inabidi Wakue kuvuka hapo.
Tanzania upinzani upo Mil8 VS Mil6, ni kipofu tu ndie anaweza kusema hakuna upinzani.
 
tatizo tunaenda mbele hatugeuki kuangalia tunapotoka. huku upinzani katika vyama ni madudu matupu na hasa hivi vyama vikubwa. ni sheeeda. nadhani katika masuala ya ukandamizaji wa demokrasia, haki za binadamu na udikteta upinzani unaongoza ndani ya vyama. chukulia mfano tu matukio machache ambayo yametokea chadema na hasa pale tu inapotokea mtu anahoji masuala fulani fulani ya uendeshaji.kwa mfano watu kama kina Mwigamba, Prof Mkumbo, Zito, hata Chacha Wangwe, kina Said Arfi, na wengineo wengi. yaliyowatokea kila mtu anajua. lakini ni matokeo ya ukandamizaji wa demokrasia ambayo tunaita ni matendo ya kidikteta
pale katika kutafuta kiongozi kwa njia ya demokrasia, rejea jinsi kiongozi mgombea urais alipatikanaje. ni kwa mabavu na udikteta. haiwezekani ujio wa watuhumiwa wa ufisadi wakapokelewa na kusafishwa na kupewa vyeo vya ndani ndani ya chama ghafla. angalia leo hii imani kwa wanachama imepotea kabisaa. kiasi cha kufanya kina Dr Slaa kutimka. ni baada ya uhuru wao wa kidemokrasia kukandamizwa. ni hatari kwa mwwnyekiti Mbowe na watu wachache kufanya matendo yanayofanana na kidikteta namna hii.
leo hii nashangaa kina Lissu wanalalamika eti uongozi wa Dr Magufuli unakandamiza demokrasia. inashangaza kabisa. wakati Lissu mwenyewe anajua kabisa kuondoka kwa Dr Slaa alikuwa karibu atoe chozi la damu. kwa namna kiongizi mahili kama yule alivyotendewa ndivyo sivyo. Lissu hakuweza kumhoji Mbowe kwa sababu hiyo ya ukandamizaji. hata hicyo maskini Lissu hakuwa na cha kufanya kwa sababu pale ndipo ugali wake unapatikana. hana jinsi. hana pa kukimbilia maana akiharibu imekula kwake.
ifike mahali tuambizane ukweli na sio kulea na kuficha maovu. hatutabadilika. tulizungusha mikono ya mabadilikoooo. ni lazima yaanzie nakwetu wwnyewe na si vinginevyo
 
Naamini bila kuvuka level za kweli hizo ulizotaja hapo, bado upinzani utaendelea kuwa teketeke.
 
Hakuna wapinzani Tanzania. Wengi ni waganga njaa tu. Sasa wamekuja na mbinu mbadala za kujipatia fedha kutoka kwenye vyama vyao. Wanatoa kauli zenye utata kwa makusudi ili waweze kupelekwa mahakamani. Wakishapelekwa mahakamani wanapata posho ndefu kutoka kwenye vyama vyao kwa kisingizio cha kusimamia au kumsindikiza mtuhumiwa. Wanachokifanya ni maigizo tu, lengo lao kubwa (vinara wa chama) ni kujipatia fedha.
 
watakuja kukujibu maoni yako.
 
Tanzania hatuna upinzani ,tuna waganga njaa tu.

Vyama Vya upinzani vimejaa udikteta wa kutisha kiasi kwamba ukimkosoa mfalme Mbowe unaitwa msaliti na kufukuzwa kwenye chama.
Mbona haumuongelei dikiteta uchwara, hata kumwabia kuwa anakosea anakupeleka kisutu.
 
Tangu link mwanachama mtiifu wa ccm kama wewe ukaitakia mafaniko chadema?
 
Daah! Unafikiri wananjaa kama wewe? Rejea binge la katiba.
 
Tanzania hatuna upinzani ,tuna waganga njaa tu.

Vyama Vya upinzani vimejaa udikteta wa kutisha kiasi kwamba ukimkosoa mfalme Mbowe unaitwa msaliti na kufukuzwa kwenye chama.
Upinnzani upo kwa kuwa kuna chama tawala. Upinzani ni kwa hoja si maguvu. Mbabe aweza kutumia ubabe kusema hana mpinzani kwa sababu ya kulimbikiza nguvu zilizopitiliza kwa hilo unaweza kuwa sawa.
Ni sawa na kusema Marekani hana mpinzani kwa kigezo tu cha maguvu lakini kiuhalisia wapinzani wapo! Falsafa inatuambia kila kitu kina kinyume chake bila hivo ni vigumu dunia kuwepo! think big acha ushabiki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…