Kwanini huitwa Chuo Kikuu Mzumbe na sio Chuo Kikuu cha Mzumbe?

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
3,669
9,868
Embu tuelelewesheni utofauti hapa kwanini hii Taasisi inaitwa Chuo kikuu Mzumbe na isiwe Chuo kikuu Cha Mzumbe.

Kama ilivyo kwa Chuo Kikuu Cha Dodoma, au Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam n.k
 
Kwa sababu kwa Kiingereza kinaitwa Mzumbe University sio University of Mzumbe kama ilivyo kwa

University of Dar es Salaam au University of Dodoma. Pia The Open University of Tanzania kinaitwa Chuo
kikuu Huria cha Tanzania.
 
Embu tuelelewesheni utofauti hapa kwanini hii Taasisi inaitwa Chuo kikuu Mzumbe na isiwe Chuo kikuu Cha Mzumbe.
Kama ilivyo kwa Chuo Kikuu Cha Dodoma, au Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam n.k
Yote kifasihi yako sawa. Ni jukumu la taasisi husika kuamua watumie 'Chuo Kikuu cha......' au '........ Chuo Kikuu'
 
Kwamba Makerere University useme kifasihi ipo sawa na University of Nairobi? Kwa maana gani hata kama

Sijabobea kwenye Kiswahili. Kwa sababu pamoja na taasisi kuamua itumie namna ipi
lazima ilete maana sahihi.
 
Hata ukipeleka maneno hayo kwenye Kiingereza hamna shida. Kwa ufupi tumekopa toka kwa wao walioanzisha taasisi hizo kubwa za elimu. Hakuna sheria iliyovunjwa ukiita University of Warwick au Warwick University. Wewe tu uamuzi wenu ni ipi ina-flow vizuri. Hivyo tu hakuna aliyepatia wala kukosea.
 
Ni sawa lakini kuna jina official yani jina la usajili wa Chuo.

Kinatambulika kama Mzumbe University sio University of Mzumbe.
 
Embu tuelelewesheni utofauti hapa kwanini hii Taasisi inaitwa Chuo kikuu Mzumbe na isiwe Chuo kikuu Cha Mzumbe.

Kama ilivyo kwa Chuo Kikuu Cha Dodoma, au Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam n.k

Ni namna tu ya kuita na hata kingeitwa University of Mzumbe bado ingekuwa sahihi...
 
Back
Top Bottom