SoC04 Kwanini hatunufaiki sana na ubunifu wa Watanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

cilla

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
372
299
KWANINI HATUNUFAIKI SANA NA UBUNIFU WA WATANZANIA

Ubunifu Ni uwezo alionao mtu au kikundi cha watu,kuvumbua/kugundua kuanzisha kitu Fulani kipya au cha tofauti chenye kuleta tija kwa jamii. Profesa Bessant ubunifu ni kile unachofikiria nakukifanya unavyotaka, ni kipawa alichonacho mtu.Ubunifu unaweza kuwa katika Nyanja za teknolojia, biashara, uongozi na mavazi.

Tanzania tumebarikiwa sana kuwa na watu wabunifu katika Nyanja mbalimbali na hasa katika sayansi na teknolojia.Kila mtu ni shahidi kupitia vyombo vya habari na mashindano mbalimbali tumeona kazi mbalimbali za ubunifu katika sayansi na teknolojia zilizofanywa na watanzania wenzetu.sio hilo tu,tumeshuhudia hata vyuo vyetu vimekuwa sehemu za bunifu mbalimbali kupitia tafiti wanazofanya.​

Kwa nini bunifu nyingi za watanzania tunazoziona kwenye maonesho hatuzioni tena baada ya hapo?

Tatizo kubwa la watanzania wabunifu ni uwezo mdogo wa kiuchumi.Uchumi mdogo wa wabunifu wetu unawafanya washindwe kuzalisha bidhaa nzuri kwa wakati na kwa wingi unaohitajika.

Wabunifu wengi wanatumia muda mrefu sana katika kuunda bidhaa itokanayo na ubunifu wao na changamoto kubwa imekuwa ni upatikanaji matirio,kukosekana kwa vifaa sahihi vyakumuwezesha kuunda kwa haraka na mtaji wa fedha kumwezesha kununua baadhi ya vitu.Hii husababisha wabunifu wengi kuchukua muda mrefu sana kuunda bidhaa moja tu.Mbunifu anatumia miaka au mwaka mzima kwa kutengeneza alichokibuni.jambo hili ni kikwanzo kikubwa kwa wabunifu na kusababisha wengi wao kutoendelea kabisa ama kutonufaika na ubunifu wao.

Vyuo vyetu vinafanya tafiti nyingi za ubunifu lakini kwa sehemu kubwa nyingi zimewekwa kwenye makabati kutokana na ukosefu wa fungu maalumu la uendelezaji wa tafiti hizo.Hivi karibuni kati ya tafiti nyingi za chuo cha DIT tumeshuhudia ubunifu wao wa ufungaji wa mfumo wa magari unatumia gesi ya asili lakini cha kushangaza ubunifu huu mpaka unafanyika Dar es salaam na vituo vyakujazia gesi bado vinapatikana Dar es salaam tu wakati mahitaji ni makubwa nchini.Ubunifu kama huu serikali ilipaswa kuweka nguvu kubwa ya kifedha ili kuhakikisha vituo vya kujazia gesi nchini vinakuwepo vya kutosha na kuzalisha maeneo mengi yakuweka mifumo ya gesi kwenye magari.

Kama ubunifu huu wa kufunga mfumo wa gesi kwenye magari ungekuwa umewezeshwa na serikali na kuchukuliwa kwa uzito, basi sasa hivi tungekuwa tumeanza kulishika soko la nchi jirani na kunufaika nalo kabla wengine hawajatuwahi.Kama tunataka kuwa nchi ya viwanda sayansi na teknolojia tunapaswa kuzichangamkia fursa kwa kukimbia na kuteka soko mapema.Lakini kwa mtindo huu wakuzalisha bidhaa taratibu hata wakati wa mahita makubwa tutabaki tukijisifia tu kwamba tunawabunifu nchini lakini hatuoni matokeo makubwa ya ubunifu wao.

Pale manyara tuna mbunifu mmoja amevumbua Automatic Modified Neonatal Incubator kwaajili ya kuwasaidia watoto njiti.anatambulika sana hapa nchini kwa sababu ya tuzo aliyowahi kupata.Incubator hiyo inasemekana imesaidia watoto njiti si chini ya 2000.Wajibu wa watu kama hawa ni serikali kuubebe ubunifu huu kama moja ya utambulisho unaoweza kututambulisha kimataifa tukawa soko la bidhaa hii.Mbunifu kama huyu serikali inapaswa kumpa usaidizi na kumjengea uwezo isiwe mtu tena iwe ni kiwanda aajiri watu zaidi na kuwarithisha ujuzi watanzania kwa lengo la kuzalisha zaidi mpaka nje ya mipaka ya nchi yetu.Kwa kufanya hivyo tutapiga hatua kwenye viwanda na teknolojia kirahisi kwa sababu ni ubunifu wetu.

Kama tunataka kuwa na viwanda na kuzalisha kwa wingi lazima serikali iwekeze katika kuwafanya wabunifu kuwa na uwezo wakuzalisha kwa wingi na kwa muda mfupi na kutanua soko kimataifa.

Kama mbunifu anatengeneza kifaa kimoja kwa miaka miwili au minne hiyo ina maana mbunifu huyo hataweza kumudu soko na kuendeleza kipawa chake.

Tanzania tuitakayo Tusiishie tu kuonyesha kazi zao za ubunifu katika matamasha na majukwaa ya ubunifu, cha msingi ni uendelezaji wa kile wanachokifanya kwa kuwapatia mitaji itakayowawezesha kununua malighafi, kuajiri na kununulia vifaa vyakufanyia kazi ilikuzalisha kwa haraka bidhaa zao.​

SERIKALI IWAKUMBATIE WABUNIFU, IWALEE IWASAIDIE, WAZALISHE ZAIDI NA KWA UBORA UNAOTAKIWA.
 
Vyuo vyetu vinafanya tafiti nyingi za ubunifu lakini kwa sehemu kubwa nyingi zimewekwa kwenye makabati kutokana na ukosefu wa fungu maalumu la uendelezaji wa tafiti hizo
Hii inasikitisha asee

Tanzania tuitakayo Tusiishie tu kuonyesha kazi zao za ubunifu katika matamasha na majukwaa ya ubunifu, cha msingi ni uendelezaji wa kile wanachokifanya kwa kuwapatia mitaji itakayowawezesha kununua malighafi, kuajiri na kununulia vifaa vyakufanyia kazi ilikuzalisha kwa haraka bidhaa zao.​
SERIKALI IWAKUMBATIE WABUNIFU, IWALEE IWASAIDIE, WAZALISHE ZAIDI NA KWA UBORA UNAOTAKIWA.
Sawa sawia C

Natumai soko la hizo bidhaa likiwa kubwa pia itamsaidia mbunifu kuzalisha zaidi.

Mfano kuna ule mtindo wa pre orders, mtu anaonesha ubunifu. Watu wanaulipia halafu unakuwa mtaji wa kuwazalishia na baada ya hapo anakuwa ameshapata moto basi anaendeleaa na kasi mpya ya uzalishaji
 
Back
Top Bottom