Wadau nawasalimu
Hivi ninavyowaandikia nipo home nina ED ya siku 4, nimepigwa vibaya na watu nisiowafahamu baada ya kunishutumu kutembea na mke wao
Ni hivi
Kuna msichana tumefahamiana kama wiki Tatu zilizopita, nimenunua ka usafiri kangu hivyo nikamkuta siku moja amesimama pale kondo bahari beach asubuhi akisubiri dala dala za ununio makumbusho mida ya saa kumi na mbili asubuhi nikampa lift, kwa kweli ni mkali mno ndio maana niliona nijaribu Bahati yangu, mambo yetu yakaenda vizuri, siku chache mbele tukawa wapenzi, hadi napigwa juzi tuna wiki tatu, nimetembea nae mara mbili tu
Jumapili, on that fateful day, nikamuita sehemu tunywe, then tuingie guest maana Pana bar na guest hapo hapo, tukawa tunakunywa huku tukitazama mpira wa simba na toto Africa, kulikua na watu wengi hapo
Nashangaa linatokea kundi la watu kama sita hivi na kutufuata tulipokaa na bibi yangu na mmoja wao kumuuliza yule bibi yangu kuwa "hapa unafanya nn na huyu ni nani, " kumbe wewe ndie unatembea na mke wangu,?
Kabla sijajibu wakaniinua kwenye kiti na kuanza kunichangia wakinipiga ngumi mfululizo, usoni, tumboni mbavuni na kila sehemu, watu wakawa wanashangaa wanatazama tu badala ya kunisaidia, baadae waungwana wakajitokeza kuniamulia na kunikingia kifua, wakaondoka na yule mwanamke wangu
Tangu jumapili nakunywa uji tu, taya limevimba kung'ata chakula siwezi, Jana na leo Hali ndio nafuu, imeanza kuimarika
Hivi kwa nn huyu mwanamke alishindwa kunieleza ukweli kuwa ameolewa?
Wanawake kwa nn mnakua hivi?
Kwa nn usimweleze mtu kama umeolewa? Ningeuawa Je?
Nimemuuliza kwa nn ulinidanganya eti anadai alishaachana na huyo jamaa lakini yy bado anamfuatilia tu
Sio vizuri kwa kweli
Ngoja nipone, mm huyo jamaa nitamtafuta tu na watu wangu at any cost