Kwanini familia nyingi za kibongo zinaanza upya ktk utafutaji wa mali?

Shuku_

Senior Member
Sep 26, 2019
141
185
Habari zenu wakuu πŸ‘‹πŸ½ πŸ‘‹πŸ½

Hivi kwann familia zetu nyingi za kitanzania zinaanza upya katika utafutaji wa mali, kutoka kizazi kimoja hadi kingine ktk utafutaji?

Hii kitu imekua ikiturudisha nyuma sana katika utafutaji wa mali hali ambayo inapelekea familia nyingi kuwa masikini sana kizazi hadi kizazi.

1717692454306.jpg
 
Habari zenu wakuu πŸ‘‹πŸ½ πŸ‘‹πŸ½

Hivi kwann familia zetu nyingi za kitanzania zinaanza upya ktk utafutaji wa mali, kutoka kizazi kimoja hadi kingine ktk utafutaji ?

Hii kitu imekua ikiturudisha nyuma sana ktk utafutaji wa mali hali ambayo inapelekea familia nyingi kuwa masikini sana kizazi hadi kizazi.
Swali fikirishi...

...Ni Hayo Tu!!
 
Habari zenu wakuu πŸ‘‹πŸ½ πŸ‘‹πŸ½

Hivi kwann familia zetu nyingi za kitanzania zinaanza upya ktk utafutaji wa mali, kutoka kizazi kimoja hadi kingine ktk utafutaji ?

Hii kitu imekua ikiturudisha nyuma sana ktk utafutaji wa mali hali ambayo inapelekea familia nyingi kuwa masikini sana kizazi hadi kizazi.
Wazazi wanaamini kila mtoto anatakiwa kupambana mwenyewe, yeye jukumu lake ni kukusomesha basi.

Ila mbowe atoke madarakani
 
Sio familia tu hata nchi. Kila mtu, kizazi kinakuja na dira yake, hakuna mipango endelevu ya miaka 20, 40, 50, 75, 100, 250 na kuendana na mabadiliko ya technologia, kibiashara ya kidunia.

Hakuna succession plan. Watoto hawafundishwi toka utotoni jinsi ya kuendesha biashara kiufanisi, nidhamu, uwekezaji kwenye vitu kama bond, gold, gilts, ETF, shares, pension funds, kutanua biashara, na jinsi ya kulinda utajiri wao.
 
1. Ubinafsi
2. Ubinafsi
3. Ubinafsi
Unakuta Mzazi anamwambia mtoto urithi wangu kwako ni elimuπŸ˜‚πŸ˜‚!!.. Mzazi na mtoto wote wanaamini kuajiriwa ni sifa hata Kama analipwa laki 2 kwa mwezi! Generational wealth haiji Kwa kila mtoto kujitegemea! Angalia wahindi wanavyorithisha utajiri kizazi Hadi kizaziπŸ™Œ!
 
Hii akili ya generation zilizopita zinakuja kuondolewa na generation zinazokuja hapo ndio kutakua na mapinduzi makubwa

the Greatest Generation (roughly 1900-1924), the Silent Generation (1925-1945), Baby Boomers (1946-1964), Generation X (1965-1979), Millennials (1980-1994), Generation Z (1995-2012), Generation Alpha (2013-2025) and Generation Beta (2025-2039).

Sasa hao nilio-bold ndio kile kizazi cha nakusomesha ujitegemee urithi wako ni elimu wakiamini kwamba mtoto ukisoma ukimaliza kupata kazi sio kazi ilivyokua kwao maana wao ilikua ukisoma kidogo tu kesho huangaiki kupata kazi kwa hio wamekua na mindset hio hio mpaka kwa vizazi vyao balaa limekuja kuibukia kuanzia kizazi cha Millennials hapo ndio mambo yakaanza kua mtinganya hii nyeusi na hii nyeupe vikaanza kutambulika
 
Habari zenu wakuu πŸ‘‹πŸ½ πŸ‘‹πŸ½

Hivi kwann familia zetu nyingi za kitanzania zinaanza upya katika utafutaji wa mali, kutoka kizazi kimoja hadi kingine ktk utafutaji?

Hii kitu imekua ikiturudisha nyuma sana katika utafutaji wa mali hali ambayo inapelekea familia nyingi kuwa masikini sana kizazi hadi kizazi.

View attachment 3192553
Kwangu mie sababu ni kuwa watu wengi wakianzisha biashara wanatumia mfumo wa kuendesha biashara kwa kujikimu..

Mfano baba kaanzisha biashara hata kama kaisajili kama kampuni bado anaiendesha biashara kama
Anatafuta pesa za kujikimu hana ndoto ya kuogeuza kuwa kuna a nationawide bussiness.. mfano mtu anaanzisha biashara ya duka la jumla. Hatawaza hata siku moja kugeuza hilo duka kuwa kama walmart au shoppers.. hata afanikiwe vip utakuta atafungua duka lingine sehem nyingine ila mfumo wa uendeshaji utakuwa ule ule wa ku centrallize ( yeye au mtu wake wa karibu ndio kila kitu

Au hata akanunua mabasi hataigeuza hiyo biashara kuileta kwenye standard ya kikampuni.. inaweza ikawa imesajiliwa kama kampuni ila uendeshaji ukawa ule ule wa "kila kitu yeye". Nje ya hapo kuwe na mtoto au mtu wa karibu ambaye ndio atakuwa subornate wake basi ineisha hiyo

Ndo maana mwenye mali akifa na biashara inakufa sababu hakutengeneza mfumo wa biashara kujisimamia bila yeye kuwepo

Na ndo matajiri wengi tulionao.. ndo maana mtu ana biashara na mali lakini hawezi kufurahia utajiri wake maana bado mafanikio ya biashara yanategemea yeye kila dakika kuanzia supplier wake na wateja wake

Makampuni makubwa ya ulaya na asia watu walianza kama private own bussiness au familiy bussness. Ila iliposimama tu wakazipekeka public watu wanunue hisa au wakashawishi watu wachache wawekeze kwenye biashara yake lengo ni kuhakikisha anaifanya biashara ijiendeshe

Mfano mmiliki wa amazon, mfano mmiliki wa tesla, mfano mmiliki wa walmart,
 
Habari zenu wakuu πŸ‘‹πŸ½ πŸ‘‹πŸ½

Hivi kwann familia zetu nyingi za kitanzania zinaanza upya katika utafutaji wa mali, kutoka kizazi kimoja hadi kingine ktk utafutaji?

Hii kitu imekua ikiturudisha nyuma sana katika utafutaji wa mali hali ambayo inapelekea familia nyingi kuwa masikini sana kizazi hadi kizazi.

View attachment 3192553
umaskini ni mfumo, Utajiri ni mfumo utachagua uishi wapi.
 
Hii inatokana na familia zetu kuwa na ubinafsi an umimi mwingi...

Kingine ni umaskini tuu ila kwa matajiri hayo mambo hakuna....

Mi nitawekeza katika mishangazi hata wanangu watakulia huko
Nilijua huwezi andika comment iwe na pwenti mwanzo mwisho
 
Habari zenu wakuu πŸ‘‹πŸ½ πŸ‘‹πŸ½

Hivi kwann familia zetu nyingi za kitanzania zinaanza upya katika utafutaji wa mali, kutoka kizazi kimoja hadi kingine ktk utafutaji?

Hii kitu imekua ikiturudisha nyuma sana katika utafutaji wa mali hali ambayo inapelekea familia nyingi kuwa masikini sana kizazi hadi kizazi.

View attachment 3192553
1.Ubinafsi tu.
2.Kutokuwandaa watoto.
3.Migogoro ya familia.
4. Uchu wa Mali ya Baba na kukosa uaminifu
 
Back
Top Bottom