Kwanini CHADEMA mnatafuna ruzuku, huku mkiisakama ACT Wazalendo?

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,542
11,930
Siasa ni mfumo wa kushiriki na kuwakilisha fikra na mawazo huru kutokana itikadi tofauti za kiimani katika kuwakilisha hoja tofauti za kutafuta maendeleo kwa ustawi na maisha bora kwa wa jamii husika.

Hivyo basi sio sahihi wala halali kulazimishana kushirikiana mawazo na misimamo ya chama kimoja kwenda kingine.

Hapa pia nasena hili jambo.

Chadema mmepokea Ruzuku kimya kimya na hamjatoa tamko rasmi kwa wafuasi wenu,kwamba kama kwa kufanya hivyo ndio mmeutambua rasmi ule mliouita "Uchafuzi"
Kisha niseme sasa mada yangu rasmi.

Jana ilikuwa siku nyingne ya kihistoria nchini kwenye nyanja za kisiasa za vyama vingi.kulikuwa na uchaguzi mdogo sehemu kadhaa nchini ikiwemo huko mkoani kigoma.

Uchaguzi ambao Chadema kama chama cha siasa, kilikuwa hakikuweka wagombea.

Lakini ACT wao walikuwa wameweka wagombea na walishiriki.

Kulitokea vurugu huko baada ya wafuasi wa ACT-wazalendo kuituhumu CCM kuhusika na kile ambacho kiliaminika kuwa jaribio la CCM kuingiza kura bandia katika baadhi ya vituo vya kupigia "kura".

Sasa mimi hapa nitaongelea hoja tofauti na hilo tukio maana lenyewe bado linahitaji mambo ya kisheria zaidi kwa uthibitisho.hususan ushahidi kamili.

Mimi nitaongelea kuhusu Chadema kuisakama ACT kwa maamuzi yake ya kushiriki uchaguzi ule na kwamba walihitaji ACT iwaunge mkono Chadema katika msimamo wao wa kugomea uchaguzi.

Tumeona huko X jinsi viongozi wa Chadema na wafuasi wake,wanavyohangaika kuisakama ACT-Wazalendo kwa kitendo chao cha kushiriki uchaguzi ule.
Ilhali wao kama chama kikuu(kwa wanavyojinasibu wenyewe). Kwamba ACT ilipaswa kujiunga nao kuugomea uchaguzi ule.

Maswali yangu kwa Chadema!

□Je! CHADEMA hamtambuwi kwamba ili chama kikuwe na kupata wafuasi ni lazima kifanye mikutano ya kisiasaikiwemo pia kampeni za uchaguzi,na kisha ndio kijipime ukuaji wake kupitia chaguzi?

□ Je, Chadema hamjui kwamba ACT nayo inapenda kufanya siasa na kujitanua nchini kama ambavyo nyinyi Chadema na vyama vinginevyo ikiwemo CCM vinavyopenda iwe?

□Je, Ni nani anayewapa mamlaka enyi Chadema kuvipangia vyama vinginevyo jinsi ya kufanya siasa zake, ilhali mkijua nyinyi wote ni wapinzani wa kisiasa ambao kila mmoja anaiota "IKULU" .

□ Chadema mnafanya hadaa kwa watanzania ilhali mmechukua 2.7bilions za fedha za kitanzania na sasa mnaogelea kwenye pesa,mnaitisha maandamano nchini mkilipana posho za kujikimu, eti kwemda kuandamana.
Wapi mliona waandamanaji wakilipwa posho za kujikimu Duniani?

□Kama nyinyi Chadema mnajiamini kuwa chama kikuu cha kisiasa nchini kwa sasa.
Kwa nini mlazimishe kuungwa mkono na vyama vingine,badala ya kutumia ukuu wenu na ushawishi wenu,ili kuidhibiti CCM kupitia nguvu yenu binafsi?

Mwisho Chadema nawasihi mfanye siasa zenu kwa kutumia nguvu za hoja na sera.

Badala ya hiki mnachokifanya kwa sasa nchini.kwamba mnalazimisha hoja zenu kuwa ndio misimamo ya vyama vyote vya vya upinzani nchini.

Hata ACT nao wana haki ya kutafuta uungwaji mkono nchini kote na hatimae kuwa chama chenye wabunge nchini na hivyo kupata ruzuku ya kukiwezesha kujitanua zaidi.

Kwamba Chadema acheni wivu wa kisiasa!
 
Nini kikusikitishacho hapo wewe jamaa?Umeguswa na ruzuku au chaguzi za kihayawani?Unahangaikaaaaa!
Mbweha wa baharini wewe!ninakuuliza pia ni nini kinawasikitisha Chadema wanapoiona ACT ikishiriki?
Mnataka Zitto mliemfukuza aje tena kuwaunga mkono watesi wake?
Ndio maana mnaitwa majina ya kihayawani saa ingine!
Kuhusu Ruzuku pia ni pesa zetu walipa kodi wa nchi hii kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo makato toka mishahara yetu.
Ni halali kujua matumizi yake,pia ni vema Chadema kuacha siasa za kihuni kwa wafuasi wake.
Kupokea ruzuku mkono wa nyuma huku mkono wa mbele ukiwa juu ....piiiipooooss!
 
Chadema wanailaumu ACT kushiriki uchaguzi bila katiba mpya wakati wenyewe nao watashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu bila hiyo katiba mpya

Ni haki yao kuikosoa ACT kama wanaona maamuzi yao sio mazuri, lakini ACT wanapoikosoa Chadema, Chadema inawatukana na kuwaita ni tawi la CCM
 
Mbweha wa baharini wewe!ninakuuliza pia ni nini kinawasikitisha Chadema wanapoiona ACT ikishiriki?
Mnataka Zitto mliemfukuza aje tena kuwaunga mkono watesi wake?
Ndio maana mnaitwa majina ya kihayawani saa ingine!
Nakushauri acha matusi.Halafu,unataka CHADEMA ikupe maono,mikakati na mbinu watakazozitumia mbeleni hapa JF?Una funza kichwani si bure.Subiri ufike wakati upigwe tukio la kushtukiza.
 
Nakushauri acha matusi.Halafu,unataka CHADEMA ikupe maono,mikakati na mbinu watakazozitumia mbeleni hapa JF?Una funza kichwani si bure.Subiri ufike wakati upigwe tukio la kushtukiza.
Kwa hiyo Chadema mnayo matukio ya kushtukiza sio?
Halafu mkishashtukizana mnaigeuzia lawama CCM na serikali yake?
Sasa tunaanza kuwaelewa!

Halafu samahani sijakutukana bali nimekufananisha na mbweha wa baharini anayewinda kwenye theruji majia ya baridi na kuwinda nchi kavu kipindi cha mapukutiko!
Mfumo unaotumiwa na chama chenu kudandia matukio kuendana na nyakati husika.
Unaweza kudhani ni tusi kumbe ni utovu wako wa uelewa!
 
Naomba urekebishe kwenye andiko lako ulipoandika viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake wanaisakama CHADEMA kwa kushiriki uchaguzi.maana naona ulimaanisha CHADEMA ndio inaisakama ACT wazalendo
 
Naomba urekebishe kwenye andiko lako ulipoandika viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake wanaisakama CHADEMA kwa kushiriki uchaguzi.maana naona ulimaanisha CHADEMA ndio inaisakama ACT wazalendo
Ana wahka/panic ya kuandika harakaharaka huku kanuna ataachaje kukosea?Awe mtulivu.Aulizapo ina maana anataka majibu na siyo yeye aje na majibu yake.Atachezewa akili mpaka aimbe kikwao.
 
Naomba urekebishe kwenye andiko lako ulipoandika viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake wanaisakama CHADEMA kwa kushiriki uchaguzi.maana naona ulimaanisha CHADEMA ndio inaisakama ACT wazalendo
Kama umelewa ruzuku huwezi kuelewa!
Halafu kawaida ya nyumbu asubuhi huwa ni poor sited....
nimekuonesha kosa kwenye uandishi wako, lakini ulivyojaa kebehi na matusi hujaliona hili kosa.

haya luca na yeye kakuonesha hapo.
 
Back
Top Bottom