Wakuu salaam,
Kwa uelewa wangu kampeni huanza rasmi kwenye tarehe inayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na hii huwa ni kwenye mwaka wa uchaguzi kwa ngazi ya Wabunge.
Lakini pia baada ya mbunge kuchaguliwa, wewe unakuwa mbunge wa wananchi wote, kama unahutubia wananchi inamaanisha una-address wananchi wa vyama vyote na kuwahudumia wote kwa usawa.
Kwanini Waziri Mkuu unavaa jezi ya chama yenye picha ya Rais Samia na kauli mbiu yake? Hapo si unaendesha kampeni? Kwanini uvae nguo za chama kwenye mkutano wa wananchi? Ungekuwa ni mkutano wa chama tusingeuliza, hapa una address na wananchi wote bila kujali vyama vyao, kuvaa jezi za chama ina maana gani?
Naomba elimu hapa wajuvi. Majaliwa akihutubia wananchi kama mbunge anaruhusiwa kuvaa jezi za mama zinazotumiwa kufanya uhamasishaji wa kumkubali Rais.
Yaani anaenda hapo mama kafanya hivi, mama kafanya vile, serikali hii ya sasa ni aibu! Turudi kuwauliza kama mchungaji yule aliyeuliza, kama kila kitu kafanya Rais wao wanafanya nini? Majaliwa umefanya nini kwa wananchi?
#KataaMachawa
#KataaUozo2025
#KataaRushwa2025