Kwanini CCM Inarudia Kura Za Maoni Zanzibar

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kura za maoni za uwakilishi na udiwani ndani ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar ili kupata wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015 zilifanyika mapema mwaka jana, na wagombea walipatikana. Aidha mgombea wa urais CCM alipatikana pia.

Lakini pia historia inaonyesha kwamba katika chaguzi zote zilizopita vyama pekee vinavyoshinda kwenye nafasi zote za urais, uwakilishi na udiwani huko Zanzibar ni CCM na CUF pekee. Maana yake ni kwamba kama moja kati ya vyama hivyo viwili hakishiriki uchaguzi basi kingine ni kama kinashinda bila kupingwa.

Kwa kuwa Chama cha Wananchi CUF kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio wa tarehe 20/03/2016 ni kama CCM imeshashinda nafazi zote za urais, uwakilishi na udiwani - kwa maana ya wale waliopitishwa kwenye kura za maoni. Kwa hiyo tarehe 20/03/2016 ni kama kufanya uchaguzi kwa wale wale waliokwishapita kwenye kura za maoni za CCM, wakiwa peke yao.

Ndiyo maana najiuliza kwanini CCM wanataka kurudia kura za maoni tarehe 20/03/2016, tena kwa kutumia mabilioni ya fedha za wananchi?

Kwanini wasiwatangaze tu hawa makada waliokwishashinda kura za maoni kwamba ndio rais, wawakilishi na madiwani ili kuokoa mabilioni ya fedha ambazo zingetosha kuboresha hospitali, zahanati na shule za wananchi?

Dr. Milton Makongoro Mahanga
 
kiukweli ccm wamechanganyikiwa. Uchaguzi wa marudio march 20, 2016 ni uchaguzi wa kutafuta viongozi wa ccm na sio wawakilishi wa wananchi.
 
Hii akili tope ya kusema kwamba vyama ni CCM na CUF peke yako mtaijua Tarehe 20.
Mtoa uzi mwenyewe ni Chadema,na hakuna watu wabovu ambao hawaijui Zanzibar kama hao,na hao hao ndio kimbelembeleee kusemea Zanzibar na kila siku wanaumbuka.

Ungehsngaa kwanza wakati Bara nako ni Chadema na CCM lakini NCCR wamepotea na ACT wazalendo kimeanza juzi tu na kipo zaidi yao NCCR.

Kuweni wapooole,uchaguzi hauwezi kupanga humu JF,tarehe imetoka povu liwatoke ngoma uwanjani.
Mtaisoma tu,Zanzibar shwaaarriiii wadanganyika wanapiga zogoooo
 
Aisee. Mhe waziri mstaafu. Kwan nan alitangazwa mshindi na ni nani mwenye jukumu hilo la kumtangaza mshindi. Kama CUF wameamua kutoshiriki sawa ni haki yao ya kidemocrasia kama ww ulivoamua kuondoka CCM kwa kisingizio kuwa eti hujapandishwa cheo. Sijui sasa ndo umepandishwa uko uliko. Unajua kila chama kinachoamua kutoshiriki sijui kwann kinataka maamuzi yake yawe ndo maamuzi ya kila mwananchi. Mbona ww hukupigiwa kelele ulivoondoka. Mbona akina kingunge hawakupigiwa kelele. Ndo democrasia hiyo. Kila mtu aamue anachoona kinamfaa maadam havunji sheria. Kama kuna mtu anahisi fulani kavunja sheria ana haki ya kwenda Mahakamani. Tulalamikie utendaji wa mahakama na vyombo vingine lakini tusilazimishe mawazo yetu ndo yawe maamuzi ya Wananchi wote.
Hakuna akiyezuiliwa kuchukua his/her own direction. Wala hakuna aliyetishiwa maisha kwa maamuzi yake hayo. Nyie ndo mlimtishia maisha dr Slaa alipoamua kuchukua maamuzi yake. Hii ni democrasia so acheni kulia lia. Acheni kila mtu achukue maamuzi yake maadamu havunji sheria. Mkileta fyokofyoko mtabomolewa na msilalamike mkianza kubomolewa
 
Mbaya zaidi kwani mnashindana na nani?
 
Yaani hawa jamaa wanatamani enzi ya chama kimoja irudi tena. Kwa maana wamejaa uroho na uchu wa madaraka. Eti uchaguzi wa Meya wa Dar kila siku unapigwa danadana, kisa wanatamani kushinda. Hivi watashindaje wakati wapiga kura wao ni wachache kuliko wale wa Ukawa? Wataahirisha uchaguzi mara 100 lakini wakumbuke tu kwamba siku wakiridhia ufanyike watapigwa kama paka kidokozi. Yaani mijitu hata haina haya.
 
Nakubaliana na mwandishi ninavyoelewa mshindani akikosa wa kushindana naye hutangazwa Kuwa ni mshindi au wanachukulia vyama matawi yao ndiyo washindani ionekane demokrasia imetendeka kwa serikali inayojali mapato yake haiwezi kukubali upuuzi kama huo lakini kwa vile ni wao wafanye watakavyo na upuuzi huo
 
Pumbavu wewe sisi ndio tunaamua nani atawale huko nyie hamna uwezo wa kuweka mtu ndio maana hata Hugo mliyenae tuliamua sisi kanda ya kati
 

DR HII NI POINT YA MSINGI SANA NA HASA UKIZINGATIA KUWA RAIS MAGUFULI AMEKUWA AKIJINASIBU NA KUZUIA MATUMIZI YA SIO YA LAZIMA NA KUYAHAMISHIA PALE PENYE SHIDA NA MAHITAJI ZAIDI KWA MFANO PESA ZA SHEREHE YA KULIHUTUBIA BUNGE (TENA KWA PESA ILIYOCHANGWA), SHEREHE ZA UHURU NK. SISEMI NI JAMBO BAYA LA HASHA NI JEMA SASA NATARAJI NIONE HAYA MABIIONI YANAWASAIDIA WATANZANIA KWA MAMBO YA MSINGI MAANA TUNAJUA NANI ATAKUWA MSHINDI TAYARI.

WAU WANAWEZA DAI NI BUDGET YA ZANZIBAR AMA YA JECHA. HAPA NDIPO KATIBA HAIZINGATIWI BALI INATEGEMEA MATAKWA NI YAPI.
 

NI KWELI KABISA UCHAGUZI NI WA CCM NA VIBARAKA WAO TU PERIOD.
 
Lakini pesa zakufanya sherehe ya ccm zilikuwepo lakini si lakurusha bunge live
 
Siku zote MAPINDUZI DAIMA. Chama kisichoamini hilo, ije mvua lije jua hakishindi, iwe kwa kura au vyovyote. CUF waweke MAPINDUZI DAIMA kwenye katiba yao ya chama wapewe nchi. Kinyume chake HAWAPATI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…