Kwanini CCM inaendelea kushinda chaguzi, licha ya kuwa ndio chanzo cha umasikini wa taifa letu, rushwa na ufisadi?!

Umasikini wa mali na fikra wa watanzania ndiyo mtaji mkubwa wa CCM, sometimes hata kuleta sera mbovu za elimu ni kutaka kudumaza elimu ya tanzania ili waweze kutawala vizazi na vizazi. Kuitoa CCM kwa uchaguzi ambao upo chini ya NEC hiyo ni hadithi iliyosahaulika kwenye hekaya za abunuasi. Na kwa kinachoendelea sahivi ni ndo kabisaa wanajihakikishia wanavunja roots za upinzani ambao hadi uje kuwa stable tena ni miaka 20 mbele
 
Paskali points zako 9 and 10, wapinzani tulio nao Tanzania ni imara sana kuliko wapinzani wote duniani, kwa nini na sema hivi......... mazingira wanayo fanyia kazi ni magumu sana sana, hawashindani na CCM tu bali wanashindana na vyombo vyote vya dola. Ingekua hali hii ya Tanzania iko Kenya au nchi nyingine ya africa, basi kungekua na civil war ya kufa mtu. Vyama vya upinzani Tanzania vinahitaji pongezi kubwa sana kwa ku survive miaka yote hii katika mazingira ya aina hii.

Point ya 10, kama tatizo ni sera, kwa nini CCM inatumia nguvu kubwa ikiasi hiki katika changuzi zote. Kama sera za CCM ni nzuri kwanini CCM wasikubali kufanya uchaguzi ulio uhuru na uwazi kwa kushindanisha sera? Chama chenye sera nzuri na kweli kinapendwa na wananchi hakitumii vyombo vya dola kushinda uchaguzi na kumwaga damu za wananchi wake.
 
Ccm inashinda kwa kua tu hakuna upinzani wa kweli nchini hawa blah blah ni wa kwenye mtandao sababu mjinga unaweza kumuelimisha akaelewa wao miaka 20 hawajaweza kutoa somo!
 
CCM imefanya mabadiliko makubwa sana toka baada ya uchaguzi mkuu uliopita nina uhakika kuwa CCM itaendelea kutawala nchi hii kwa muda mrefu. Vyama vya Upinzani kwasasa havijakomaa kupewa madaraka ya nchi hii.

Ni vyama vichache vya kisiasa duniani ambavyo vinaweza kukubali na kujirekebisha kama CCM. Nina uhakika kiongozi tuliyenaye kwasasa Rais Magufuli tukimpa ushirikiano wa dhati Tanzania itakuwa nchi ya matumaini kwa vizazi vyetu vinavyokuja. Mie binafsi nilikuwa naichukia sana CCM kabla ya 2015 lakini kwasasa ninakiunga mkono kwa asilimia 100.

China wanachama kimoja tu cha kisiasa lakini leo China ndio taifa lenye uchumi mkubwa duniani. Huwezi ukaita demokrasia ndio inaleta maendeleo, chukua mfano Kenya pamoja na katiba yao mpya lakini corruption iliyopo ni kubwa sana.

Hizi kelele za wapinzani hapa Tanzania ni hujuma zinazotengenezwa na watu wasio itakia mema Tanzania
 
Mabadiliko hayo baada ya miaka 30 yatakuja miraculously? Na hiki kizazi cha ki-lumpen kitaisha vipi automatically endapo serikali ya CCM haina nia ya dhati kukiondoa maana ndio mtaji wake na wakati huohuo vyama vya upinzani havina organs of mass mobilizations madhubuti zinazotoa elimu ya siasa bali harakati za kuhamasishana baada ya matukio hasi yanayotedwa na Serikali? Kusubiri hayo mabadiliko ya hiyo miaka 30 bila maandalizi ya kuyafikia ni sawa na kuendeleza hii hii lumpen generation. Kumbuka msemo wa wahenga "things are made to happen".
 
Umeandika mambo mengi lakini point Namba 6 ndio ya maana.
Watanzania ni wajinga wana umaskini wa elimu ya uraia.
Na Ukifuatilia watu wajinga wajinga wote wapo CCM, akili ndogo ndogo zimetamalaki huko.
CCM mtaji wake wa kisiasa ni raia wasiojielewa.
Endapo Watanzania wengi ni wajinga na maskini na CCM inawafikia hao na kuwatumia kama mtaji wake kisiasa basi somehow politically iko strategic maana moja ya kipaumbele no 1 ya chama chochote cha siasa kinachojitambua ni Mass mobilization sasa kama kuna the so called opposition parties na vinashidwa kuwafikia hao waitwao kuwa wajinga na na masikini ambao ndio Idadi kubwa inayounda jamii basi hivyo vyama vimeshindwa siasa kiasi kikubwa.
 
You have a point. Organs of mass mobilization... zinakuwa suppressed na regime and amss mobilization ni mikutano ya kisiasa kuwaeleza lumpen hao wajitambue. Unafanyaje hata kama mikutano ya ndani inazuiwa? It is an uphill task
 
Utasubiri sana kuziona fujo unazotamani zitokee.
Kama ni fujo zingetokea enzi zile CHADEMA imejaa mioyoni mwa watu kabla UMMA haujasalitiwa na akina Mbowe.
Kwani lini vijana walikuwa na ajira mkuu? Na Ngosha kazipeleka wapi sasa?
Hoja ya usaliti ni mufilisi. ila CCM mnaitumia sana ili kuficha kile hasa mnachofanya.
Anyway, maisha yanaendelea japo ya wengine mnayakatisha kila iitwapo leo.
tutafika tu.
 
Chintu hujawahi kuwa CHADEMA bhana cjui kwanni mtu mpaka udanganye chama chako ili ionekane hoja ina mashiko miaka yote wewe umekuwa ukitetea watawala pamoja na kwamba ndio wametufikisha hapa tulipo

Sawa tukubali upinzani ni dhaifu na kwamba baada ya kuja lowassa wananchi wakaisusa CHADEMA sasa basi naomba unisaidie kuna uhusiano gani kati ya mfumo mbovu wa uchaguzi na wananchi kuichoka CHADEMA

Yaani kwakuwa mshafahamu CHADEMA haikubaliki kivp hamuweki chaguzi zisizo na figisu figisu kma tulizoona kinondoni na Siha???
 
Bwana Pascal Mayalla, nadhani umefika mahali kama Watanzania, tujadili hiki kitu kinachoitwa "Umaskini Uliotopea" wa Watanzania. Maana yake nini na Uhusiano wa umaskini huu na TANU/CCM, Imefanya nini kusababisha umasikini huu. Kwamba kama Chama hakijafanya nini kuwafanya watu kuondokana na umaskini huu uliotopea?

Mwalimu JK Nyerere alizungumzia "Pesa sio msingi wa maendeleo" Bali "Kazi" na kwa miaka ile ya awali, Ardhi kwa maana ya Kilimo na sera/mazimio yake vilitegemewa kuwaondoa watu ktk umaskini. Je TANU/CCM ilitamka hali ikiwazuia watu kutumia Ardhi yao kujiletea maendeleo hata ikawa hadi leo bado tukawa na umaskini uliotopea?

Tumefika mahali nchi INA Shule za msingi kila Kata, huku msisitizo wa serikali kila mtoto mwenyewe umri wa kwenda Shule aende, wengine wanashtakiwa kwa kutowapeleka watoto wao Shule, Lakini bado tunaitana Wajinga, huu ujinga na wakipimo gani na hawa TANU/CCM wanaotulazimisha tupeleke watoto Shule wanachangiaje Ujinga wetu unasababisha *umaskini" uliotopea?
Tumekuwa na wasomi wasomi wa kuhitimu Havard, Makerere, Urusi, UDSM, Makerere, China mpaka miaka ya 2000 kulipoibuka utitiri wa vyuo vya elimu ya huu. Hawa wote hawajanufaika na elimu hiyo bado tunawajinga tu? Upanuzi huu was wigo wa elimu bado tuwajinga tu hata tukawa na umaskini uliotopea?
 
Umeandika mambo mengi lakini point Namba 6 ndio ya maana.
Watanzania ni wajinga wana umaskini wa elimu ya uraia.
Na Ukifuatilia watu wajinga wajinga wote wapo CCM, akili ndogo ndogo zimetamalaki huko.
CCM mtaji wake wa kisiasa ni raia wasiojielewa.
Ninge kupa like 5.
Elimu ya uraia nitatzo hakuna kingine hapo pascal sijui anataka chama gani stable.
 

Kwanza nikupe pongezi, Mkuu Paskali kwa bandiko refu, unalodai ni elimishi.

Pili nikupongeze kwa kujikubali kuwa, wewe kama Mtanzania, kinachokuongoza kumchagua mwakilishi wako ni umasikini na ujinga wako, na pia na wewe ni mateka wa rushwa na ufisadi.

Tatu, sikubaliani na wewe hizo sababu ulizozitoa za kwa nini CCM inaendelea kuchaguliwa. Soma majibu yangu, katika maandishi mekundu, ndani ya bandiko lako.

Wasalaam,

mwengeso
 

Ukweli ni kwamba viongozi wa upinzani wanatumia nguvu nyingi, za kila aina, ikiwa ni pamoja na ahadi hewa, pesa na vitisho, kuhamasisha vijana, kufikia malengo yao ya kisiasa, iweje uje na hoja kama hiyo (maandishi mekundu)!!
 
Ivi Pascal ata wewe kama haukumchagua JPM katika uchaguzi uliopita, Nita amini akilizako hazipo sawaswa.

Wewe ukiacha kuwa Maarufu kwenye Media, Ni mkongwe kwenye tasnia ya habari.
Ivi tukiacha utani na siasa za kipuuuzi, ivi kwenye upinzani uliokuwepo 2015 au kwasasa nani unaweza ukampambanisha na JPM? Ki uhalisia hakuna Mtanzania mwenye mwenye uelewa wa mambo awe amesoma au hajasoma, kwa safu ya upinzani iliyopo kuwapa nafasi ya kushika Dola/Serikali litakua Jambo la ajabu sana.

Mimi kwa namna ninavyo ona kwenye Ubunge, Udiwani hakuna shida kama yupo mpinzani anaye eleweka wananchi wamchague haina shida. Si kwanafasi ya urais, ii itakua kutaka kuifanya nchi hii Sacco's.

Watu hawana ata ofisi ya Chama kwa miaka zaidi ya 20 na wanapokea mabilioni ya walipakodi wanapata kama ruzuku.Viongozi wanagawana nafasi ki ngonongono na kifamilia hivi tutafika?
 
Kaka umenadika vizuri saana lakini katika yooote hapo point Number (8) ndio ya msingi wa matatizo unayodahnia kwamba yapo. Kama kifungu number (8) kingekuwa sio kikwazo leo usingeandika hizo point zoote na ndipo ungegundua kwamba Upinzani Tanzania upo na ni imara saana. Kwa ufupi tu ukitaka kujua hilo jaribu kufuatilia baada ya Uchaguzi wa Kinondoni na Siha ni Groups ngapi za Whatsap (achilia yale ya Wanalumumba and its allies), mitandao ya kijamii zilishadadia matokeo hayo na je kama Chadema ingekuwa imeshinda majimbo hayo yote mawili unadhani hali ingekuwa hivyo hivyo? au msiba wa Akwilini ungefunika hizo shamrashamra za matokeo pamoja na kwamba hayo majimbo awali yalikuwa ni ya chadema?
 
1. Wazee waliokuwepo enzi za Uhuru bado wapo hai. Hivyo wanaamini kutokipigia kura ccm ni kuisaliti nchi

2. Nguvu ya vyombo vya dola kwa baadhi ya maeneo ambayo wananchi wana uelewa

3. Utengano wa vyama vya upinzani. Kura nyingi za upinzani zinagawanywa. Ilitakiwa waunde chama kimoja

4. NEC ni tatizo kubwa. Tatizo hili ni kwasababu inateuliwa na walioadarakani. Nitatolea mfano Zanzibar uchaguzi mkuu wa 2015. Kila mtu anajua kilitokea nini

Ccm itang'olewa kuanzia miaka 20 ijayo. Kipindi ambacho wazee wengi waliokuwepo enzi za uhuru watakua wameshapotea na kitabaki kizazi cha ya hivi karibuni
 

Wameshaanza, kila leo utasikia diwani wa chana kile kauwawa nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…