juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,463
Huyu jamaa Benjamin Sitta ni diwani wa kata ya Msasani, kabla ya uchaguzi wa ndani wa vyama huyu jamaa hakuwa anakubalika hata na chama chake kabisa, ipo wazi na anajua hilo, ila sijui ilikuwaje hadi akapitishwa yeye? Mi na wewe hatujui lakini pia baada ya kupitishwa akapata upinzani mkali kutoka UKAWA, kulikuwa na wagombea wawili wenye nguvu sana wa CUF na CHADEMA ambapo CUF ilikuwa na mzee maarufu lakini haijajijenga kichama, huku CHADEMA kukiwa na kijana aliyejiwekea mizizi miaka mitano nyuma ila ndani ya chama chake kukiwa na makundi ya wanaomtaka na wasiomtaka, hatimaye likapita jina lake.
Sasa hapo ndipo kukatokea sintofahamu kubwa, CUF hawataki kuachia kata na CHADEMA hawataki kuachia kata,na hili kosa namlaumu sana Halima Mdee (mbunge wa Kawe) ikatokea kipindi chote cha kampeni yule mzee wa CUF akaenda kuhiji huko Maka, huku mwenzie Ben Sitta akimaliza mitaa kwa kampeni (sisemi alivyokuwa anatoa, ila Mungu anajua na yeye anajua) baada ya hapo ndipo CHADEMA wakaanza kufanya kampeni kimyakimya kuona mwenzao wa CUF hayupo, mgombea wa CHADEMA hakuondoa jina lake NEC kwa hiyo kata ikawa na wagombea watatu(CCM, CUF na CHADEMA)
Ila taarifa za huyu Ben Sita kuutaka Umeya zilikwepo kabla ya uchaguzi, ikasemekana jamaa anautaka Umeya wa Kinondoni na wala shida si Udiwani zilienea sana hizi taarifa hatimaye sasa imetimia na hata wagombea wa UKAWA zikaenea taarifa kwamba jamaa ndie aliyewagawa ili apite kiuraini kwa sababu bila CUF na CHADEMA kuweka wagombea wote basi Ben sitta Udiwani aliusikia kwenye bomba maana zile kura za CUF na CHADEMA ukizichanganya CCM waliachwa mbali, sasa maswali ya kujiuliza ni je kwanini huyu jamaa anautaka umeya wa Kinondoni sana? Au ndio harakati za kuutaka ubunge wa Kinondoni 2020? Au kuna ajenda gani kubwa kwake?