Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,536
Baada ya jana Baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA) kutoa kauli kuwa watakwenda Dodoma kusaidia CCM kutii sheria bila shuruti, kumetokea mijadala mbalimbali juu ya suala hilo. Wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kinachochea uvunjifu wa amani.

Jana kwenye group moja la Whatsapp Mbunge mmoja wa CCM (simtaji kwa sasa ila akisoma hapa atajifahamu) aliandika "Chadema njooni mtufanyie fujo Dodoma mvunjwe miguu"

Nikamuuliza nani kasema BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya fujo?

Jana nimesikiliza agizo la Makamu Mwenyekiti BAVICHA Patrick Ole Sosopi hakuna popote aliposema wanakwenda Dodoma kuwafanyia fujo CCM. Alisema wanakwenda Dodoma kuwasaidia CCM kutii sheria bila shuruti kwa kuzuia mkutano wao.

Ili kuweka kumbukumbu sawa ikumbukwe kwamba June 7 mwaka huu Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama VYOTE vya siasa, kwa kile kilichoelezwa kuwepo kwa taarifa za kiitelijensia kuwa kutatokea uvunjifu wa amani.

Tarehe 20 mwezi June, mkoani Dodoma jeshi la Polisi likatoa taarifa mpya kuwa zuio linahusu pia Makongamano na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Kwa kutumia hoja hiyo wakazuia mahafali ya CHASO Dodoma, Kilimajaro, na kongamano la ujasiriamali lililokuwa lifanyike ukumbi wa KKKT Bariadi mjini (japo vyote hivyo vilikua vifanyike kama mikutano ya ndani).

Hata hivyo "Mheshimiwa Rais wetu mwema" JPM, akaongezea kuwa kwa sasa shughuli za siasa zisimame kwa muda ili watu wafanye maendeleo. Shughuli za siasa ni pamoja na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo basi shughuli za vyama vya siasa zilizozuiwa hadi sasa ni Maandamano, Mikutano ya hadhara, makongamano ya kisiasa na mikutano ya ndani.

#MaswaliMuhimu

1. Je CCM wanachokwenda kukifanya kipo ktk orodha ya vilivyozuiwa?

2. Je agizo la Polisi limefutwa?

3. Je agizo la Rais kuzuia shughuli za kisiasa limefutwa?

4. Je walichopanga kufanya BAVICHA ni sahihi?

#MAJIBU

1. CCM wanakwenda kufanya mkutano mkuu wa chama chao. Na kwa kuwa mikutano yote ya kisiasa imepigwa marufuku, CCM wamepoteza "legitimacy" ya mkutano huo. Kwa hiyo hadi sasa mkutano huo ni batili (until further notice).

2. Kuhusu agizo la Polisi bado halijafutwa.

3. Kuhusu agizo la Rais bado halijafutwa.

4. Kuhusu kauli ya BAVICHA, hawajakosea. Hii ni kwa sababu kwa maelezo yao hawaendi kufanya fujo. Wanaenda kuhakikisha CCM wanatii sheria bila shuruti.

Nimeona watu wakiuliza eti Polisi wameomba msaada kwa BAVICHA? Swali la hovyo sana hili, na wengi wanaouliza ni wenye uelewa finyu. Lakini majibu yake ni kwamba huhitaji kuombwa na Polisi ili kumkumbusha mwenzio kutii sheria. Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki na wajibu wa kutii sheria na kumkumbusha mwenzie umuhimu wa kutii sheria za nchi.

Kwa hiyo suala la kumkumbusha mwezio kutii sheria ni wajibu wa kikatiba wa kila raia. Haihitaji kuombwa na jeshi la polisi wala jeshi la zimamoto. Kwahiyo BAVICHA wanakwenda Dodoma kutimiza wajibu wao huo kikatiba.

Kuna watu wanafikiri BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya kazi za Polisi. La hasha. Hizi ni fikra nyingine mgando. BAVICHA hawaendi kufanya kazi za polisi.

Wanakwenda Dodoma kama raia kwenda kuwakumbusha raia wenzao (wanachama wa CCM) umuhimu wa kutii sheria bila shuruti. Kwa kuwa Rais amezuia shughuli za kisiasa, CCM wanapaswa kuonesha mfano kwa kutii agizo hilo la Rais. Wasipotii basi BAVICHA watasaidia kutii kwa kuzuia mkutano huo, ili kuondoa "double standards" ktk nchi. Hicho ndicho kinachowapeleka BAVICHA Dodoma.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_Nchi?

1. BAVICHA wapongezwe kwa ujasiri wao.

2. Jeshi la Polisi litumie BAVICHA kama kielelezo cha kuwakumbusha raia umuhimu wa kutii sheria bila shuruti.

3. Mkutano mkuu wa CCM uahirishwe.

4. CCM wapewe onyo kwa kujaribu kuandaa mkutano wa kisiasa kinyume na agizo la Rais hali inayoonesha wanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

5. Yakishindikana hayo manne hapo juu, basi mikutano yote ya kisiasa iruhusiwe kuanzia leo.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_CCM?

1. Rais afute agizo lake la kuzuia shughuli za kisiasa kwa muda (anaweza kuruhusu agizo hilo liendelee baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

2. Polisi wafute agizo lao la kupiga marufuku mikutano, maandamano na makongamano ya kisiasa (wanaweza kuendelea na marufuku hiyo baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

3. CCM waamue kufanyia mkutano wao nje ya nchi.

NB: Kukumbushana umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ni wajibu wa kila raia. Tuwapongeze BAVICHA kwa kuliona hili.!

Malisa G.J
 
Mlisema chadema mtafanya mikitano kwa nguvu ,lakini hadi leo kimya! mlisema mtaandamana hadi Leo kimya, mlisema mtalinda kura hakuna hata mmoja aliyejotokeza, Leo mmekuja na nyimbo mpya.

Nakuhakikishia hyo tarehe 23 hakuna hata bavicha mmoja atayeenda huko.

NARUDIA; HAKUNA HATA BAVICHA MMOJA ATAYETHUBUTU KWENDA HUKO!!
 
CCM ndio chama kilichopewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi. Ni chama dola. Na ndio maana mambo yanayoandaliwa na CCM na Serikali yake yanaenda vizuri. Maonesho ya sabasaba yanaendelea. Yanga wamecheza na TP Mazembe hawajazuiliwa. Kagame kawasili nchini. Ukiwa mtawala maana yake unatawala kila kitu. Nyie Bavicha Nendeni Dodoma mkavunjwe miguu
 
Rais alisema siasa zifanywe na wanasiasa mahali waliposhinda uchaguzi na si kufanya siasa mahali ambapo hamkushinda uchaguzi. Lengo likiwa ni kurahisisha watanzania kupima utendaji wa waliochaguliwa utendaji wao ifikapo 2020.

CCM wameshinda ushindi wa jumla mkoani Dodoma. Hivyo wana haki ya kufanya Mkutano hapo Dodoma. Kama Bavicha wamepanga kufanya hayo, watakuwa wanakosea. Godlisten washauri wasifanye hivyo.

>Nawaza kukueleza hivyo Malisa .
 
Hao BAVICHA wao ni polisi wawe na uwezo wa kuzuia CCM? Maana ake wanaenda kufanya fujo, wao wadeal na polisi sio chama kingine cha siasa, rais hakukataza wanasiasa aliwaomba wafanye Katika majimbo yao weka video yake tuone, kama nyie ni wagumu kuelewa peke enu sio wote
 

Hilo hawawezi kukujibu. Huyu Malisa ndiye aliyemtuma yule kijana kumtukana Rais kwenye Facebook. Kijana alipohukumiwa kulipa faini, huyu Malisa akachangisha fedha ii kijana atolewe. Nasubiri nini kitatokea
Lizaboni unaweza kudhibitisha kuwa mimi ndiye niliyemtuma huyo uliyemuita "kijana aliyemtukana Rais?"
 
Mimi kuna kitu uwa sielewi hivi kuwa kiongozi chadema lazima utokee kaskazini?

Mwenyekiti Mbowe wa huko huko, mwenyekiti baraza wanawake Mdee wa huko huko.. Jana nimeshangaa huyo mwenyekiti wa Bavicha kavaa kimasai kabisa yani hiki chama na yule dogo aliyekuwa mwenyekiti wa kuchaguliwa ni kama kapinduliwa tayari majukumu yote sasa kapewa mkaskazini mwenzao.

Aisee awa jamaa wakigusa Dodoma hakuna rangi wataacha kuiona watataja koo zao zote za mareale mushi msuya ndossi mpaka ukoo wa mleta mada malisa.
 
Walichotakiwa chadema kufanya ni wao pia kuitisha mkutano wa ndani,siku hiyohiyo tena ikiwezekana dom hapohapo,halafu waone kama watazuiwa ama vipi
Huwezi kutoa kibali cha mikutano miwili ya vyama katika eneo hilo hilo...kumbuka ratiba za kampeni.

Hivi UVCCM wakiamua kutia maguu Dodoma kwa kazi maalum ya kuwadhibiti Bavicha itakuwaje??
 
Dah aisee mnaumizaga kichwa ukawa.. Hii awamu nyingine take care... Sisi tupo busy tunadai risiti na Kulipa kodi tujenge nchi yetu nyie bado Mnataka siasa...
 
kwa hali ilivyo ccm na jeshi la polis ndo wanahamasisha uvunjifu wa amani. vyama vyote vya siasa ni sawa bila kujali chama tawala ama lah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…