Kwanini ATMs, branches pamoja na mawakala wa NMB hawawezeshwi kutoa huduma za TTCL-PESA ilhali serikali inamiliki hisa nyingi sana pande zote mbili?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,892
16,413
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu Jamii Forums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier ni mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Kwanini ATMs pamoja na mawakala wa NMB hawawezeshwi kutoa huduma za TTCL-PESA ilhali serikali inamiliki hisa nyingi pande zote mbili? Je, kufanya hivi hakutawezesha kupanua huduma za T-PESA na hatimaye kukuza shirika letu hili la umma?

Ukijaribu kuangalia screenshot hapo chini utaweza kuona number 7 ambapo Bank ya NMB wamewezesha wateja wake kuweze kutuma pesa straight from their accounts to TTCL Mobile Wallet. Sasa kwanini wateja wa TTCL-PESA washindwe kujihudumia kwenye ATMs pamoja na mawakala wa NMB wakati mmiliki ni mmoja?

IMG_20191120_121136_611.jpg


Kama kwa mteja wa Vodacom pamoja na Airtel anayetumia M-PESA pamoja na Airtel Money anaweza kutoa pesa kwenye ATMs pamoja na branches za CRDB, kwanini wateja wa TTCL-PESA washindwe kutoa pesa kwenye braches, ATMs pamoja na mawakala wa NMB ilhali wote hawa ni watoto wa mama mmoja ambaye ni serikali?

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Anayetakiwa kufanya hivyo sio NMB, Ni TTCL.

Ila hapa taratibu mkuu usije ukashtaki watu, Tigopesa na MPESA unaweza kutoa kwenye ATM kitambo so this is nothing new ila ni uzembe wa TTCL.
 
Kwahiyo tu-assume serikali inamiliki 2%!! Kwahiyo nyingi ni anything above 1, ndo unaamini serikali ina sauti mbele ya majority shareholders sio?!
Mkuu, kuna sehemu nimeandika kuwa ninaamini kuwa serikali ina sauti? Please Don't misquote me
 
Mkuu, kuna sehemu nimeandika kuwa ninaamini kuwa serikali ina sauti? Please Don't misquote me
Kama usingeamini ina sauti usingezungumzia habari za kumiliki "hisa nyingi! Na kila anayefahamu haya mambo, pia anafahamu kwamba idadi ya hisa ni determinant ya mwenye nazo kuwa na sauti kwenye taasisi husika!!
 
Nina wasiwasi na home work yako kama umefanya vizuri? Maelezo pia yanajichanganya au labda mimi nachangayikiwa bado niko kitandani ss hivi. Lawama unapozipeleka siko.
 
Back
Top Bottom