Sweya Makungu
JF-Expert Member
- Jun 11, 2023
- 482
- 582
Napenda kumshukuru sana Mhe. Rais kwa kuufanyia kazi ushauri wangu nilioushauri kwa Waziri Mkuu mwezi February juu ya suala la kuuza vyakula nje.
👇
Kwa Waziri Mkuu.
Farao hakuuza chakula nje kwa sababu nje kulikuwa na njaa, bali Farao aliuza chakula nje kwa sababu ndani kulikuwa na akiba ya kutosha:
©️ Mwl. Makungu m.s
0743781910
Mfalme Suleiman anasema katika Mithali 6:6>
"Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?"
Mhe. Waziri, kama hatujafikia hatua ya mapinduzi ya kilimo, kwanini turuhusu vyakula vitoke? Kama hatuna akiba ya kutosha, kwanini tutapanye chakula chetu nje?
Waziri Mkuu mwenzako aitwaye Yusufu wa nchi ya Misri chini ya Mfalme Farao wa nyakati hizo, alikuwa na sera ambayo serikali ilihusika moja kwa moja na kilimo bora cha nyakati hizo. Na si hilo tu,serikali ndiyo ikawa mnunuzi mkuu wa mazao ya chakula (nafaka) toka kwa wakulima ndani ya nchi.
Wakulima wote, wafanyabiashara wa mazao wote walitakiwa kuiuzia serikali chakula. Ikawa na akiba ya kutosha san, na ilipofika wakati wa njaa kali, serikali ikawa na uwezo wa kulisha nchi nzima kwa miaka 7 bila mavuno yoyote ndani ya hiyo miaka. Ikawauzia wananchi wake chakula kwa bei ya kawaida.
Na kuonesha ni jinsi gani walikuwa na akiba ya kutosha wakawauzia hadi watu wa nchi ya jirani. Na kwa kuwa njaa ilikuwa kali kwa muda mrefu,hata watu walipoishiwa hela kabisa wakaweka dhamana ardhi zao kwa serikali wakaendelea kupewa chakula. Hata wasiokuwa na ardhi wakaweka dhamana nguvu zao kufanya kaz za serikali wakapewa chakula.
Haya yote yalifanyika kwasababu serikali ilikuwa na akiba ya kutosha.
Hebu tujitafakari sisi Mhe. Waziri; je, tunafanana na chungu au ni wavivu tumelala usingizi?Kama serikali haitaki kujihusisha na ununuzi wa mazao ya chakula na inaijua nchi yetu haijafikia mapinduzi ya kilimo, kwanini itapanye vyakula nje?
Tunatakiwa tufike hatua ambayo tuwe na akiba ya kutosha kiasi kwamba sisi wa ndani tuuziane kwa bei ya kawaida halafu wale wa nje ndiyo tuwauzie bei juu.
Nchi yetu tangu mwaka juzi vyakula vimepanda bei sana na vinazidi kupanda. Siyo kwa sababu hatuna mavuno, bali ni kwa sababu mavuno yanaenda nje na hatuna mapinduzi ya kilimo ya kuleta mavuno ya ziada.
Je, sisi bado ni wavivu tuliolala usingizi?!
Mhe. Waziri, Mafarisayo walimuuliza Yesu, "Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka ya nani?"
Makungu m.s
0743781910
26 February 2023