Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,188
- 67,755
Hamjamboni wote!
Unapokuwa Mwanasiasa watu ni sehemu ya mtaji katika Kazi yako hiyo. Watu kukukubali ni jambo kubwa na la muhimu kwenye siasa na utawala.
Pesa zinaweza zisiwe na umuhimu Sana mbele ya Kukukubalika kwa Watu.
Sasa kwenye Kukubalika hapa ndipo andiko langu lilipo.
Hapa kuna Makundi matatu:
1. Wanaokukubali Naturally vile ulivyo.
Kuna watu watakukubali vile ulivyo bila hata ya wewe kutumia nguvu yoyote. Yaani wao wamejikuta damu Yao ime-match kwako. Wanakupenda from nowhere. Hawa hata uongee utumbo,ufanye Jambo zuri au baya hawa wapo upande wako tuu.
Kundi Hili wanatoka upande wowote wanaweza kuwa sio wanachama wa chama chako na hata wasiwe na chama
2. Wanaokukubali kwa Sababu mna-share interest, falsafa, mitazamo n.k.
Kundi hili wao hujali zaidi maslahi Yao na kile kinachowaunganisha kama mnafanana falsafa, mitazamo n.k.
Kundi hili wengi huweza kuwa wanachama wenzako.
Lakini kundi hili sio la kudumu Sana kwa Sababu pale vitu vinavyowaunganisha vikiisha basi na ushawishi wako kwao unafikia Kikomo.
3. Wanaokukubali Mpaka uwashawishi.
Hawa ndio wapo wengi zaidi kuliko Makundi mengine.
Na hii ndio hufanya Kazi ya siasa kuwa
ngumu zaidi kuliko Kazi yoyote kwa Sababu ndipo utawala na uongozi wa watu ulipo
Kundi hili ndipo andiko letu litajikitia HAPO!
Ikiwa siasa inahitaji watu hii itamaanisha uwe na uwezo wa kulinda watu wanaokukubali, na kutumia mbinu na mikakati kushawishi wale ambao hawakukubali yaani wale ambao hawakoupande wako
Na hiyo ndio inanifanya niione Siasa ni kama Mchezo wa Draft.
Kwa wale Wachezaji wa Draft mabingwa kama Taikon Master mtakubaliana na Mimi Kuwa Mchezo wa Draft ili ushinde itakupasa uhakikishe unampunja mwenzako kete zake kusudi wewe uwe na kete nyingi kuliko za mshindani wako.
Kanuni ya Pili, ni kuhakikisha unashika Njia kuu za Mchezo ili kumzuia mshindani wako ashindwe kufanya movements zenye madhara kwako. Na Kanuni ya mwisho nikulinda kete zako zisikae katika Hatari ya kuliwa na mshindani wako bila faida. Kwamba ikitokea umeruhusu kete yako kuliwa basi uliandaa Kupata faida kubwa zaidi kupitia Kete hiyo.
Kanuni ya mwisho ni kutega mitego ambayo sio rahisi mshindani wako kuiona kirahisi. Na Jambo hili linawezekana ikiwa utaweza kuweka mitego ya bosheni kumpoteza maboya mshindani wako. Huo ndio Mchezo wa Draft kwa Sisi mabingwa. Unafanana kwa Kiasi kikubwa na michezo ya Siasa.
Kete ni WATU.
Huwezi kushinda kwenye siasa kama huna kete muhimu na hujazipangilia na kuziweka katika Njia sahihi kumiliki Mchezo.
Unahitaji kuwashawishi watu Kwa namna yoyote Ile wawe upande wako.
Kwenye Draft kuna kete zinazoingizwa King. Kete hizo huwa na uwezo wa kuzunguka sehemu yoyote na Kula kete nyingi zaidi
Kwenye siasa lazima utambue watu wenye ushawishi kwa Watu wengine hawa ndio kings wa Mchezo wako ambao ukiwatumia hao unajua nyuma Yao wapo wafuasi wengi ambao watakuwa upande wako.
Sitaki Kuchochora na kusema mambo mengi
Tundu Lisu ni kweli anaushawishi. Lakini ushawishi wake upo kundi la watu wenye mitazamo, falsafa na interests zinazofanana na wale wanaomkubali naturally.
Hii Inamaanisha kuna kundi kubwa la watu ambao wanahitaji awashawishi ili wawe upande wake. Na kwa bahati mbaya kundi Hilo ndilo hubeba watu wengi zaidi kuliko Makundi mengine.
Tundu Lisu pamoja na kwamba anasema Ukweli lakini linapokuja suala la ushawishi kumfanya mtu ambaye hakukubali abadili mtazamo wake juu yako itampasa aongee Ukweli wenye Sanaa ndani yake. Asiongee Ukweli Mkavu Mkavu kama kina Siye Kina Taikon ambao Sisi kwa sasa hatuhitaji kumshawishi mtu yeyote awe upande wetu. Sisi tuna Uhuru wa kuzungumza ukweli wowote kwa namna yoyote.
Ukweli wowote kwa namna yoyote husemwa na Wanaharakati.
Lisu lazima awe na akili ya kujuwa wakati gani awe mwanaharakati na wakati gani awe Mwanasiasa ili Kupata nguvu zaidi.
Ukweli Mkavu Mkavu HAUTAKIWI kwa Watu ambao wapo kinyume na wewe alafu Muda huohuo unawahitaji wawe upande wako. Mambo hayaendi hivyo.
Tundu Lisu anapotoa hotuba zake hujikuta akijisahau na kushindwa kujua ni wakati gani awe Mkali.
Ukali kwenye ushawishi haupogo.
Huwezi mshawishi mtu ambaye yupo upande mwingine kwa kumuonyeshea Ukali.
Ukali wakati usiosahihi unabeba tafsiri ya Udikteta Uchwara.
Watu wasipokuelewa haina maana wao ni wabaya au wanakosea. Unahitaji utumie Mbinu za akili kuwashawishi wakuelewe.
Ukiwa kwenye interviews za kisiasa ni lazima uhakikishe Ukali wako hata kama upo unauhifadhi kwa wakati sahihi.
Ukali mbele za watu huweza KUBEBA tafsiri nyingi hasa kwa wale wasiokukubali hata kama ukali wako unahoja muhimu.
Wengi huweza kuutafsiri kama Ujuaji, kujiona, kiburi au jeuri.
Kufikia hapa Taikon Master Sina la Ziada
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam