Mwaka 2016 nenda tuu baba, tumejionea mengi juu yako hatukuchukii ila ujio wako ulikuwa na mbwembwe sana.
kama nilivyo kubali kukupokea pia acha nikubali kukuaga.
nenda tuu baba na maajabu yako ya kuwafanya watanzania wauimbe wimbo wa darasa verse zote kuliko wimbo wa jumuiya ya afrika mashariki.
ulikuja na mengi saana ila ondoka nayo tuu baba.haiwezekani hata Yanga nao wanalia mishahara ya miezii miwili hawajalipwa _*wakati wao ni wa kimataifa wanatumia dollars?*_
nenda tuu baba ukikutana na faru john msalimie mwambie huku bado wanatafuta kaburi lake.
Nimegundua aisee hii miaka inayogawanyika kwa 2 huwa migumu sn kwangu.2014 nilipata tabu balaa,2015 nikafanikiwa japo kidogo, 2016 ni maumivu mpaka natamani niu-forwad uishe.
Mungu msaada na usimamizi wako 2017.