MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,181
- 5,429
Umuofia kwenu wapendwa,
Katika takwimu za afisa elimu huyo za mwaka huu wa 2023 ameutangazia umma kuwa watoto 49000 kati ya 112000 hawajafanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi uliomalizika juzi.
Takwimu hizi amezipata kupitia maafisa elimu wake ngazi za wilaya, kata na shule. Je kwa takwimu hizi kweli kuna wasimamizi wa elimu katika mkoa huo?.
Ikiwa takwimu ni kubwa kiasi hiki hawa maafisa elimu na wadau wengine wa elimu wanasimamia elimu gani katika mkoa wa kigoma?.
Mafanikio siku zote hayaombwi bali hulazimishwa kama kotapini ya baiskeli. Katika takwimu hizi hata katibu tawala wa mkoa anatawala nini ikiwa takwimu zimekaa kwa sura hii.
Natoa mapendekezo yafuatayo kwa idara ya elimu mkoa wa kigoma:
1. Wazazi wote ambao watoto wao hawakushiriki kufanya mtihani wa September 2023 wakamatwe na kufungwa jela miezi 6 bila huruma kwa kuwa wao ndiyo wanaostahili kusimamia elimu ya mtoto.
2. Afisa elimu mkoa. Huyu ndiye yupo kwa niaba ya wizara ya elimu. Anasimamia mfumo wote wa utoaji na upatikanaji wa elimu mkoani kigoma kwa niaba ya serikali. Ameshindwa kuwasimamia wote walio chini yake kwa kuwa HATOSHI. Anyang'anywe madaraka hayo na ashushwe chini ikibidi arudi darasani kufundisha.
3. Wanafunzi wote walioshindwa kufanya mtihani wapatikane walipo na wapewe adhabu ya viboko 10 kila mmoja na warudishwe shule kwa hati maalumu ktk shule walizokuwa wameandikishwa.Walimu wakuu ktk shule zilizoongoza kwa kuwa na watoro wengi waondolewe kuwa walimu wakuu kwa barua ya onyo na karipio hawatoshi.
4. Wenyeviti wa vijiji. Kila mwenyekiti wa kijiji ambaye watoro wamevunja rekodi aende jela miezi 3 maana hajui maana ya kuongoza jamii ameshiriki kuangamiza kizazi hiki. Mwenyekiti yupo kwa niaba ya jamii.Jamii yote lazima iwajibike ktk malezi ya watoto.
5.Walimu
Kwa kuwa walimu ni wajibu na haki lakini wajibu usio na matokeo chanya ni wajibu uliokufa hapa walimu pia wameshindwa kutekeleza na kutimiza wajibu kamili ingawa kufeli kwa watoto hakuwezi kuwapotezesha kazi. Ninashauri waonywe kwa mdomo.
Mwisho takwimu za upungufu wa madawati na miundombinu mingine lazima ziwe na dosari. Wizara ijitafakari siyo kukimbilia posho na kujilipa mipesa mingi wakati hakuna ufuatiliaji wowote.
Tuache kuchekeana takwimu hizi za Mkoa wa kigoma katika elimu ni ishara mbaya kwa elimu ya Tanzania na wadau wote wa elimu.