Kwa wanaoagiza mchanga au kokoto tunaibiwa aisee kumbe uwa wanapunguza njiani kuna vituo

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
513
1,132
Yaaani leo kuna kitu nimejifunza kwa wale wajengaji hii sijui kama mnaijua aya malori liwe la mchanga au kokoto yana utaratibu wana vituo njiani.

Wanapunguza mzigo ule ambao wewe uliagiza na ushalipia yaaani wanaoaki wanatoa turubai wanapunguza mzigo wa kutosha wakija site kwako wanafikia kumwaga kumbe mzigo haujajaa kwenye bodi aisee kila Kona watu wanapiga
 
Yaaani leo kuna kitu nimejifunza kwa wale wajengaji hii sijui kama mnaijua aya malori liwe la mchanga au kokoto yana utaratibu wana vituo njiani. Wanapunguza mzigo ule ambao wewe uliagiza na ushalipia yaaani wanaoaki wanatoa turubai wanapunguza mzigo wa kutosha wakija site kwako wanafikia kumwaga kumbe mzigo aujajaa kwenye bodi aisee kila Kona watu wanapiga
Hiyo inafanyika sana mkuu wewe kama unajenga na uko maeneo wanayopitia hao jamaa kabla ya kufika mjini usiwape order subiri wakati anapita amepiga lumbesa yake wewe mpige mkono mwambie nahitaji trip moja hapa chap, haachi utakushushia mchanga au kokoto. Akikiuliza unataka mwingine mwambie hapana akipita mwingine naye fanya hivo utajikuta ukinunua trip mbili unakuwa umepata tatu. Mimi huwa nafanya hivo tu hawanioi shida.
 
Anaenunua kapiga hela za dili, anaeuza kapigwa na trafiki, na wewe kakupiga kidogo,

Vikifika site una mpiga fundi kwenye leba chaji na yeye anakupiga kwenye material! Wenye viwanda wanakupiga kwenye vipimo vya material, yaaani KUPIGWA NI STAIL YA MAISHA KAMA MPIRA HADI USHINDI UPATIKANE!
Ukiona mtu hapigi huyo hayupo mchezoni
 
Kwanini mkinunua msiwe kuna kijana mmoja mnamuagiza anaenda nao.
Ukienda nao machimboni huna tofauti na ule unoletewa site hawatajaza mpaka juu waishia mwisho wa bodi. Labda ukodishe gari uende machimboni ununue mchanga ambao huwa ni elfu 20 mpaka 30. walipe wapakiaji hapo utakuwa na faida.
 
Yaaani leo kuna kitu nimejifunza kwa wale wajengaji hii sijui kama mnaijua aya malori liwe la mchanga au kokoto yana utaratibu wana vituo njiani. Wanapunguza mzigo ule ambao wewe uliagiza na ushalipia yaaani wanaoaki wanatoa turubai wanapunguza mzigo wa kutosha wakija site kwako wanafikia kumwaga kumbe mzigo aujajaa kwenye bodi aisee kila Kona watu wanapiga
Ukiniletea trip KUMI,trip zote unazomwaga Niko site....NAKAGUA KILA LORI UNALOLETA...
 
Kila mahali ufisadi. Huo ndiyo utanzania usishangae. Unakula Kwa urefu wa kamba yako
 
Anaenunua kapiga hela za dili, anaeuza kapigwa na trafiki, na wewe kakupiga kidogo,

Vikifika site una mpiga fundi kwenye leba chaji na yeye anakupiga kwenye material! Wenye viwanda wanakupiga kwenye vipimo vya material, yaaani KUPIGWA NI STAIL YA MAISHA KAMA MPIRA HADI USHINDI UPATIKANE!
Ukiona mtu hapigi huyo hayupo mchezoni
Kila mtu ashinde mechi zake!
 
"Ukiona mtu hapigi huyo hayupo mchezoni"

Mwisho WA kunukuu
 
Tofali na mawe ndio wanaiba sana

Kuna jinsi ya kupanga tofali na kama sio mtaalamu utaumia mapema sana
 
Ni hatarii sana hadi Matofali pia wanapunguza njiani na wakifika site wanajifanya wana haraka na kupanga ovyo ili ushindwe kuhesabu.
Tuwe makini la sivyo tunawafaidisha wao.
 
Back
Top Bottom