Kwa wale anti-Electical Vehicle: Unaijua ZEV Mandate?

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
25,430
72,651
Wakuu kwema. Kusave muda, hii ni kwa wapenda Hybrid na Electric Cars.

Haya, Zero Emission Vehicle Mandate (ZEV Mandate) ni "sheria" waliojiwekea nchi za US, EU na China ambapo wana lazimisha makampuni yanayotengeneza au kuingiza magari mapya kwenye izo nchi yatransform kutoka kwenye Internal Combustion Engine (ICE) cars kwenda kwenye Battery Electrical Vehicles (BEV) lengo ikiwa kupunguza greenhouse gasses na kupambana na global warming.

Kwa mfano, Uingeleza waliniwekea kwamba kufika mwaka 2030 kila gari jipya linaloingia au kusajiliwa kwenye nchi yao lazima liwe na EV yaani waachane kabisa na magari ya engine. Ingawa prime minister amesogeza hadi 2035 kwa kuzingatia watu wengi bado hawajazielewa EV na pia gharama za maisha.

Ila sheria ni ngumu kwa makampuni yanayotengeneza. Mfano, kwa mwaka huu 2024 lazima 22% ya magari yanayotengenezwa na kila kampuni yawe ya EV, kufika mwakani 2025 lazima EV ziwe 28%, kufika 2026 iwe 33% kufika 2030 iwe 80% na kufika 2035 iwe 100%. Hope kidogo nimeeleweka.

Tunaona jinsi makampuni makubwa ya magari yalivyoamua (au tuseme yalivyolazimishwa) kwenda kweny EV mfano BMW (i7, i5, i3, iX1, iX2 etc), Audi (e-tron zote mfano Q4, Q6 etc),
images (2).jpeg

Mercedes Benz (EQS, EQE, EQS SUV, EQA nk), Land Rover (wao wanaiita New RR Electric 2024), nk nk nk.
images (6).jpeg


Sasa izo za Ulaya tu imagine USA nao wana hadi Hummer la EV,
images (8).jpeg

Ford zile pick-up F15 Lighting zimeletwa za EV.
images (9).jpeg


hadi Semi za EV naona Tesla ameshaziachia.
images (10).jpeg

Bado kuna Mabasi, pikipiki, quad bike, baiskeli etc etc.

Toyota from Japan nao hawapo nyuma, tunaona Rav 4, bZ4X, Proace etc.
images (11).jpeg


China ndio kaleta balaa, Huawei na Xiaomi wameoana simu hazina faida wameingia sokoni kwenye EV.
188d0b4c14a6b4ebf82e8f05d6bdd219.jpg

Na Huawei nao..
images (7).jpeg


Tanzania zitakuja tu. Tutake tusikate. Sasa wafanyabiashara na mafundi wamejiandaeje?


Kwa kuangalia hivi, dunia inaenda kwenye electrical vehicles. Tupende tusipende. Huu uwe wito kwa mafundi wetu kujiendeleza kimasomo waweze kusolve haya magari.



Kuna hii takwimu ndogo inaonesha jinsi EV zilivoongezeka kutoka 2010 hadi 2022 ukipata bando icheki. Imagine kuanzia 2022 hadi 2024 ambapo tumeona Tesla amepunguza hadi bei ya magari kwa 30% mapya.

Aisee. Imagine unataka kutoka out simu haina chaja, saa haina chaja, gari halina chaja, earpods hazina chaja,.. TANESCO mjiandae.
 
Kwa hapa Tanzania kwa sasa tuna pikipiki za kuchaji
Lakini kwa upande wa magari ya umeme kwa Tanzania bado sana japo tunatarajia maana mabadiliko ya kiteknolojia uwa yanatusomba tu kama mafuriko
Kwa sasa tuendelee kununua hizi hybrid generation za karibuni angalau tufurahie ulaji mdogo wa mafuta.
 
Kwa hapa Tanzania kwa sasa tuna pikipiki za kuchaji
Lakini kwa upande wa magari ya umeme kwa Tanzania bado sana japo tunatarajia maana mabadiliko ya kiteknolojia uwa yanatusomba tu kama mafuriko
Kwa sasa tuendelee kununua hizi hybrid generation za karibuni angalau tufurahie ulaji mdogo wa mafuta.
Hybrid 😍😍😍 Mungu akijalia 2025 nafanya maamuzi magumu.
 
Kwa hapa Tanzania kwa sasa tuna pikipiki za kuchaji
Lakini kwa upande wa magari ya umeme kwa Tanzania bado sana japo tunatarajia maana mabadiliko ya kiteknolojia uwa yanatusomba tu kama mafuriko
Kwa sasa tuendelee kununua hizi hybrid generation za karibuni angalau tufurahie ulaji mdogo wa mafuta.
Dar zipo mbona
 
Mchawi luku
Magari mengi ya EV (ya kuanzia 2016 kuja juu) yanatumia 0.25kWh (unit) kwenda 1.5 km on average. Kwahiyo kwa wastani kama unaendesha Kilometa 100 kwa siku, utatumia Unit 16 hivi.

Unit moja ni Tsh 350/= kwahiyo unit 16 ni Tsh 5600/= tu.

Kwahiyo kwa Tsh 5600 unaenda kilometa 100 wakati ungenunua mafuta kwenye IST ungepata lita 3 average ambazo unaenda kama kilometa 60 (assume IST inatumia 20km/L kitu ambacho sio kweli).
 
Africa ngoja tuendelee na Internal Combustion Engine

Kwenye trucking hata South Africa matajiri wananunua roli mpya za mwaka 2023/24 kufanya long haulage ya copper kutoka Congo DRC kwenda Durban Port na Port Elizabeth hawataki hizo Electric Vehicle mazingira sio rafiki hata kama ni nafuu kuzidi Diesel
 
Back
Top Bottom