Kwa utafiti huu: Ni hakika hawa jamaa wa (WCB) wananunua views

Pi Network

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
290
319
Diamond na wimbo wake "Salome" ambao leo ni miezi minne tu tangu wimbo huo uachiliwe hewani, tayari huko Youtube una views 12 Million.
Wimbo wenyewe hata hauna ujumbe wowote yaani; mara anasema ooh! "chambua kama karanga" sasa anatwambia sisi ili tufanye nini?

Wakati Darassa na wimbo wake "Music" ambao ume-hit sana ndani na nje ya nchi na kuteka vituo vyote vya radio na television nchini, wakati huo huo, wimbo huo ukiwa umebeba ujumbe mzito, na wenye kuzua lengo kwa msikilizaji. Wimbo ambao hadi leo (yaani hivi tunavyo ongea) umevunja ndoa za watu na kusababisha baadhi yao kutupwa gerezani.

Lakini cha kushangaza zaidi kama si kusikitisha, huko Youtube wimbo huo ambao una miezi 2 na zaidi una views 3.9 Million! Si mchezo!



 
watu makini tu!
ndio watagundua kuwa wewe ni shabiki wa Diamond..!

However, kutoa hit-song ni jambo moja, kuufanyia mziki wako biashara ni jambo lingine la msingi. Kuwa na views nyingi youtube sio jambo la kutoa hit-song moja tu na kukaa kuanza kuhesabu views zako youtube.
Diamond ameshafanya kazi kubwa huko nyuma, kiasi kwamba leo akitoa ngoma yoyote ile, haiwezi kulingana youtube viewers na msanii yeyote wa bongo.

Huyo Darasa ndiyo kwanza anaanza, akikazana sana ipo siku atafikisha viewers kama hizo za Diamond.
 
yawezekana ikawa kweli mkuu,lakini kumbuka wimbo wa darasa una mahadhi ya kitanzania,wa salome una mahadhi ya kiafrika kwa hyo pia unaweza vutia hata wasio watanzania kuucheki,tofauti na wimbo wa darasa japo unapendwa na wemgi hasawa Tz na sio wa nje ya Tanzania,pia kumbuka Diamond Anauza brand na sio wimbo,wimbo unaweza kua mbaya jina likambeba,binafsi hata mimi wimbo wa Salome siupendi kabisa,ila una Identity ya kiafrika
 
Inawezekana na wewe unajiita ni "mchambuzi" wa muziki wa bongo fleva.
Kwani uongo sasa jaman kuwa aje kiba kasimama peke yake lkn salome mond kasimama na rayvanny so kuna mashabiki wa mond na rayvanny kwny izo viewz
 
Kwani uongo sasa jaman kuwa aje kiba kasimama peke yake lkn salome mond kasimama na rayvanny so kuna mashabiki wa mond na rayvanny kwny izo viewz
Kwani wimbo alioshirikishwa M.I ni upi ....... (basi kwa akili yako ILIVYO NDOGO utasema kwenye video hayupo) Lakini pia kama (5m /8 =kitu kama laki 7 kwa mwezi) wakati huo huo 12 milioni gawa kwa 2 = 6m /4 = 1.5m kwa mwezi,bado SALOME IKO JUU HATA UKISEMA MASHABIKI WA RAY NA MOND WAKO SAWA.
 
Kwani uongo sasa jaman kuwa aje kiba kasimama peke yake lkn salome mond kasimama na rayvanny so kuna mashabiki wa mond na rayvanny kwny izo viewz
Impact ya rayvany in ndogo sana kwenye viewers za diamond apo rayvany ndo kanufaika kuonekana kwa mashabiki wa diamond
 
Naomba kufundishwa jinsi ya kununua viewers youtube, kila nikijaribu nashimdwa.
 
Kama huu nao ni utafiti, basi utafiti hauna maana...
Vyanzo vya data ni vya uongo(nyimbo za Alikiba na Mr Blue ) hazijaangalia akaunti sahihi za wanamuziki.

Na hapana cha maana zaidi ya dhihaka kwa watu wanaotafuta vyao kwa nguvu na akili zao.
 
Aje ni solo project

Salome ni collaboration project
We unatka kutuambia rayvan Ndo kamfanya mondapate viewers wengi daah eti collab Sasa mbona kajiandae ni wimbo wa alikiba X dimpoz lakini kiba anaukimbia nakujifanya kama haumhusu baada YA kuona haufanyi vizri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…