Kwa upepo unavyoenda, kuna dalili zote Donald Trump kuswekwa jela kama hatoshinda uchaguzi

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
861
2,330
Habari zenu wanabodi,

Kwa namna siasa za marekani zinaendelea ni dhahiri shahiri kuwa Trump ana mengi sana ya kupoteza iwapo atashindwa kuingia pale White House mwaka kesho.

Siku ya Ijumaa, Jaji kutoka jimbo la New York alitangaza kuahirisha kutoa hukumu kwa Donald Trump.

Jaji Merchant alitangaza kwamba atatoa hukumu Novemba 26, kipindi ambacho tayari uchaguzi wa Marekani utakuwa umeshafanyika.

Ikumbukwe kuwa, Donald Trump alipatikana na hatia kutokana na mashtaka kwamba alimlipa Stormy Daniels, mwanamke muigizaji wa filamu za ngono karibu dola 130, 000 ili kumnyamazisha, inayofahamika kama "hush money" kabla ya uchaguzi mkuu wa 2016.

photo_5978616690059100780_x.jpg

Wachambuzi wengi wa siasa za Marekani ikiwemo Alan Dershowitz, Harvard Law professor, amesema kuwa Jaji Merchant ameahirisha kesi makusudi ili aweze kumsweka ndani Trump, kama hatashinda uchaguzi kwani hawezi kutoa hukumu hiyo sasa hivi kwa sababu bado Trump ni mgombea wa urais.

Soma pia: Mahakama ya Juu Marekani yatoa uamuzi kuwa Trump ana kinga katika kesi ya Januari 6

Alan Dershowitz, amedokeza akiongea na Newsmax amedokeza kuwa "I think he (the judge) might suspend the sentence, but I think he's going to say this conviction warrants imprisonment,"

Narudisha kwenu swali wakuu, mnadhani mahakama inaweza kumfunga Trump, iwapo hatoshinda uchaguzi
 
USA siyo kama Afrika ambavyo jaji anaweza some time kuamua kwa matakwa yake, Trump huyo huyo ambaye impetchment zilishindwa ndio afungwe kwa kesi hizo za kutengeneza, kwani kumpa pesa ili anyamaze kusema hiyo siyo kesi ya kumfunga mtu, huyo alipewa pesa kama ni mtoto sawa lakini kama ni mtu mzima kwanini alipokea hiyo pesa, democratic wanajua kutoboa ni vigumu mbele ya Trump
 
Wanasema hiyo pesa iliwekwa kimakosa kwenye vitabu vya accounting vya Donald Trump.

Waliiweka hiyo hush money kama campaign fund, ambayo ni kinyume cha sheria za New York
 
Back
Top Bottom